Jumanne, 12 Julai 2016
MGONJWA AFARIKI BAADA YA KUKOSA SHILINGI 2,000 YA CHETI
Patamambo imepata taarifa kuwa huko Tandale Hospitali Dar es salaam mgonjwa aliyetoka nje ya hospitali na kukaa nje ya hospitali na akalala nje usiku kucha, mashuhuda wanasema hospitali walipopewa taarifa hawakujali.
Mashuhuda wanadai kuwa alishindwa kuhudumiwa kwa sababu alikuwa hana shilingi 2000 ya kadi na mpaka anakata roho alikuwa nje ya hosptali hiyo,tukio hili la kusikitisha limetokea baada ya mgonjwa huyo kuzidiwa na umauti kumkuta.
Mmoja wa mashuhuda amesema kuwa……….>>>’kaja toka jana kaingia ndani baada ya kuingia ndani kwa kuwa alikuwa hajiwezi alivyotoka akafikia akakaa hapa, basi alipofikia akalala mpaka leo asubuhi, tukawa waoga, tukaenda kituo cha polisi tukatoa taarifa, akaja polisi akamwangalia nae akaondoka, mwenyekiti akarudi tena nae akaondoka, mpaka inafikika saa 6;30 akawa anang’ata ulimi anakufa’
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni