Jumamosi, 9 Julai 2016

CLINTON NA TRUMP WAZUNGUMZIA MAUAJI MAREKANI



Clinton na Trump

Wagombea wawili wa kiti cha Urais nchini Marekani wametoa maoni yao kuhusu yale yaliyotokea katika mji wa Dallas ambapo polisi watano waliuawa na sita kujeruhiwa.

Hillary Clinton amesema kuwa mauaji hayo yanastahili kumshangaza kila raia wa Marekani.

Amesena kuwa Marekani ni lazima ifanye jitihada zaidi, kuwa na mipangilio kuhusu matumizi ya nguvu kupitia kiasi kutoka kwa maafisa wa polisi na pia kuwalinda polisi.


Maafisa wa polisi mjini Dallas

Naye Donald Trump alitoa video akisema kuwa mauaji hayo yamelitikisa taifa hilo.

Alisema kuwa Waamerika ni lazima waonyeshe uzalendo kwa polisi lakini akaongeza kwa vifo vya wanaume wawili weusi mikononi mwa polisi, vinaonyesha bayana jinsi kazi kubwa inastahili kufanywa kumwezesha kila Mmarekani kuhisi kulindwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni