Kila ninapojaribu kushirikisha Rafiki zangu Juu ya dhamira yangu ya kufanya mambo makubwa maishani kama vile kuwa kati ya mabilionea wakubwa 10 nchini Tanzania, huwa ninapata Jibu la "Huwezi", kwamba Hayo ninayotaka kuyafanya yanataka mtaji mkubwa sana.
Hata hivyo, nimeapa kutokata tamaa, kwasababu wanasema "mtu akikwambia Huwezi kufanya Hili" Maana yake.
anakwambia yeye hawezi. Ukiuliza ni Kwanini wanasema "Haiwezekani" kufanya mambo makubwa, Jibu lao huwa ni moja tu nalo ni "mambo mazuri yanataka mtaji" .
Suala la kukosa mtaji limetolewa na watu wengi kama sababu moja Kubwa ya wao kushindwa kujikomboa kutoka kwenye janga kubwa la umaskini na hasa umaskini wa kipato. Kutokana na hali hii, watu wengine wemefikia hapo hata ya kuacha kufikiria Kitu Chochote kinachohusu mafanikio.
Wanasema kila wakiwaza kufanya Kitu chochote cha maendeleo au uwekezaji wanagundua Kuwa hawana hata senti moja ya pesa.
Kwahiyo, mtaji kwao umekuwa ni kizuizi cha wao kufikia maisha mazuri. Hali hii ya kujiona hatuna mtaji ni jambo la hisia zaidi kuliko uhalisia (Ukweli) wenyewe.
Tangu tukiwa wadogo tumeaminishwa uongo Kuwa "Huwezi kufanya Kitu cha maendeleo Mpaka upate pesa Kwanza" . Lakini, Baadae imekuja kugundulika Kuwa suala la kuhitajika pesa na upate pesa ni uongo mtupu.
Tumia akili yako vizuri, itakupa pesa.
Najua utajiuliza maswali mengi bila kupata jibu kamili juu ya usemi huu, na hii ni kutokana na kwamba ukweli, kwa miaka mingi umeweza kusikia na kuambiwa na watu wako wa Karibu Kuwa "unahitaji Kuwa na pesa ili kupata pesa".
Kwa vyovyote vile kama umekuwa ukiambiwa maneno haya mara kwa mara, ni wazi kwamba umekuwa muumini mzuri wa maneno haya. Ni vyema leo ukaanza kuhoji juu yako ya imani hii ambayo umekuwa nayo kwa miaka mingi na inawezekana imechangia hata kukukwamisha kufikia mafanikio makubwa ambayo ni haki Yako ya msingi.
Jaribu leo kuipa akili yako changamoto ya kufikiri nje ya ya mazoea siku zote. Na ukiendelea kuipa akili yako changamoto ya kufikiri upya, ninapenda nikushirikishe walau sababu chache za kwanini ni hatari endapo utaendelea kuamini uongo huu wa kwamba unahitaji kuwa na pesa ili kupata pesa.
Imani ya kwamba ni lazima kuwa na pesa kwanza ili kupata pesa ina athari lukuki na ni mojawapo ya kikwazo kikubwa cha sisi kushindwa kufanikiwa, kwanini ni kwa sababu Inaiba matumaini yako yote.
Kwanini matumaini ni muhimu? Kwa sababu kama huna pesa na ukachagua kuamini uongo huu kuliko kuamini kwamba una nguvu. Unajihisi kunaswa kwenye mbio za sakafuni ambazo uishia ukingoni. Matokeo yake unajihisi na kujisikia Kuwa unahitaji pesa, ili kujinasua kwenye mtego wa umaskini.
Kwahiyo, unapoona huna pesa Kwanza unaamua kuendelea na umaskini wako bila kuchukua hatua yoyote kwasababu wewe unaamini umaskini wako utaondoka tu Siku ukipata pesa - kibaya zaidi ni kwamba siku Hiyo haijulikani itafika! lini inakufanya kuwa mchungu.
Kama unaamini kuwa inahitajika pesa kwanza ili kutengeneza pesa, na huna pesa, basi inawezeka kabisa ukajisikia na kujiona mnyonge mbele ya watu wengine na hatimaye kujiona mwenye mkosi au bahati Mbaya kuliko watu wengine.
Kwahiyo badala ya kuwa na hamasa unapoona mafanikio ya wenzako, wewe unaanza kuwachukia walichonacho. Nadhani mtakubaliana na mimi kuwa hapa Tanzania hali hii ya kuwachukia matajiri bila Sababu inazidi kuota mizizi kadiri siku zinavyozidi Kwenda mbele.
Na badala ya kuongeza kujiamini hadi kufikia mafanikio, unaanza kuona mafanikio ya wengine kama tishio la wewe kupata uhuru wa kipato (fedha). Inakupa kisingizio:
Mojawapo ya jambo la hatari Kubwa kuliko zote ni kutumia uongo huu kama kisingizio au sababu ya wewe kushindwa kuboresha na kuongeza elimu yako juu ya uwekezaji, ujasiriamali na fedha. Badala ya kusonga Mbele na kuchukua kila fursa au mwanya wa kujifunza Juu ya fursa mbalimbali zilizopo, unaamua kuacha kuendelea.
Saa utakayokubali kwamba "haiitajiki pesa kupata pesa" , ndipo mara moja utaanza kujipa Nguvu, matumaini na la muhimu Zaidi, utaacha kutoa visingizio kama sababu ya wewe kushindwa kuchukua fursa fulani fulani zinazojitokeza kila Siku.
Hii ddiyo tofauti ya watu ambao wamefanikiwa na wale ambao hawajafanikiwa. Ewe mtanzania mwenzangu, malalamiko juu ya kukosa mtaji hayatakaa yaishe, kwani hakuna watu maalumu ambao wapo kwaajili ya kukugawia mtaji.
Kupata mafanikio makubwa kunahitaji ndoto ya maisha mazuri, muda, mipango au mikakati. Kikubwa zaidi, tunatakiwa kuchambua na kujua tunahitaji nini ili kuishi maisha ya ndoto yetu.
Ukishafahamu nini hasa mahitaji yako, rahisi kujipanga na kutenda kidogo, huku ukichukua hapo hatua moja baada ya nyingine. Endapo utaweza kuwa na ndoto na baadae ukatenda sawa na ukubwa wa ndoto hiyo, basi ujue kuwa siku moja utaweza kufika kwenye mafanikio makubwa uliyokuwa ukitamani kuyapata.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni