Klabu ya FC Barcelona ya Hispania leo July 12 2016 imetangaza kukamilisha usajili wa mchezaji mwingine atakayejiunga na klabu yao kuanzia msimu wa 2016/2017, Barcelonakupitia tovuti yao wametangaza kumsajili Samuel Umtiti kutoka klabu ya Olympique Lyonnais.
FC Barcelona imemsajili Samuel Umtiti kwa mkataba wa miaka mitano, kwa dau la uhamisho wa euro milioni 20, Umtiti atajiunga na kikosi cha Luis Enrique na atakuwa akicheza nafasi ya beki wa kushoto au beki wa kati.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni