Jumamosi, 18 Juni 2016

KANUNI ZA MAFANIKIO


Kanuni ni desturi,taratibu au kaidi ambazo hazina budi kufuatwa ili uweze kupata matokeo fulani ambayo umekusudia.Kanuni za mafanikio ni taratibu ambazo unatakiwa kuzifanya ili kuweza kupata matokeo mazuri katika jambo au ndoto fulani.

Nilipokiwa mdogo,nilijua kuwa mafanikio ni kuwa na magari mengi,majumba,ng'ombe au mashamba.Kumbe maana halisi ya mafanikio ni kupanda kutoka hatua moja kwenda nyingine kiuchumi,kiimani na kimasomo.

Kila kukicha watu wamekuwa wakitafuta mafanikio kwa kufanya kazi kwa bidii sana lakini hujikuta wakilalamika kuwa wameshindwa kupata mafanikio makubwa kwa sababu ya kushindwa kufuata utaratibu na kanuni za kupata mafanikio.Sababu nyingi zinaweza kuzuilika kwa mfano matumizi mabaya ya pesa,matumizi mabaya ya Muda n.k.
Matumizi mabaya yapesa yamekuwa ni kilio kikubwa kwa watu wengi ambao wamekuwa wakifanya manunuzi ya vitu bila kufikiria faida na hasara ya vitu hivyo?

Ni ukweli usio na shaka kuwa vijana wengi wamekuwa wakifanya matumizi makubwa kwa sababu ya kumuangalia mtu fulani anacho au sababu ya msanii fulani kavaa hivi bila kupima faida na hasara za kitu kile.Mfano Ninamiliki komputer mpakato na kamera kwa sababu ni mwandishi wa habari,vitabu,blog nk bila vifaa hivyo siwezi kufanya lolote.Nahisi huo ndio mfano mzuri amabao unaweza kukusaidia.
Ili kufanikiwa katika maisha ni lazima ufuate kanuni na taratib zifuatazo.

1. Tambua kuwa maisha ni kanuni

Hakuna aliyezaliwa na kuanza kutembea au kukimbia,jinsi maisha ya mtoto mchanga anavyopitia katika hatua ya kupakatwa mikononi,kukaa,kutambaa,kutembea,kukimbia na mwisho wa siku kupaa kulingana na imani yake ndivyo ilivyo hata katika kanuni ya Mafanikio.(Soma MFANANO WA KANUNI ZA MAFANIKIO NA UKUAJI WA MTOTO)kwenye makala zijazo.

Maisha ya mafanikio ya kweli na ya kuduma huja kwa mtiririko huo unaofananishwa na ukuaji wa mtoto mdogo,hata leo hii kuna wengine wanalelewa,wengine wanakaa,wengine wanatambaa,wengine wanakimbia na wengine walishapaa.

Hakuna aliyewahi kuruka kanuni hiyo hata moja na kuendelea kuwa tajiri milele.Ni juhudi peke yake zinaweza kukutoa hapo kwenye kutambaa au kukimbia na kukupeleka kwenye kupaa.

2. TUMIA KICHACHE WEKA KINGI

Kanuni hii ndio ambayo watu wengi inawashinda,hata mimi ilinisumbua sana na kushindwa kuelewa pesa niliokuwa naipata imekwenda wapi.Niliwaza mengi mpaka nilihusisha imani za kishirikina na kumsingizia mdudu mmoja ambae ana jina linalosifika la CHUMA ULETE.

Kumbe katika maisha hakuna chuma ulete,chuma ulete ni matumizi yako mwenyewe.Niliweza kutatua changamoto hii kwa kusoma vitabu mbalimbali vya ujasiliamali,kuhudhuria semina na kuendelea kujifunza zaidi kwa waliofanikiwa.

3. UJASIRI

Kuwa na mafanikio makubwa si lelemama,inahitaji ujasiri mkubwa sana katika maamuzi ya kuwekeza katika miradi mbalimbali.Hakuna tajiri ambaye aliwahi kuwa milionea bila kuwa jasiri wa kuthubutu,hebu jiulize msomaji wangu usingethubutu kuingia Darasani na kujifunza kusoma pengine hata kusoma makala hii usingeweza,hivyo basi bila ujasiri kusingekuwepo na matajiri duniani.

4. ISHI MAISHA YA KAWAIDA

Tatizo hili liko sana katika nchi za ulimwengu wa tatu hasa Afrika,kuishi maisha ya kawaida ambayo mtu wa kawaida anaishi inasaidia kwa mbaya wako kushindwa kujua kuwa unamiliki mali nyingi na una mafanikio makubwa.

Pia itakusaidia kujifunza mengi juu ya mambo mbalimbali ya jamii inayokuzunguka.
Mfano niliwahi kumuona tajiri mwenye magorofa kariakoo sikuamini macho yangu,kuongea kwake,kuvaa kwake kutembea kwake hakutofautiana na watu wengine hata kidogo.

5.AMINI KUWA UNAWEZA

Imani ni kuwa na hakika ya mambo uyatarajiayo baina ya mambo yasiyoonekana.Imani inajengwa katika akili ya mtu/moyo wa mtu kwanza ndipo inapelekwa katika vitendo.Kama ndoto yako ni kujenga nyumba kubwa amini hivyo na ishi ukiiwaza nyumba hiyo.

Watanzania wengi tumekuwa ni wepesi wa kukata tamaa  na kulalamika huku  tukijiwekea mikwamo ya kimaendeleo katika mioyo yetu na maneno yetu.Katika kuliangazia hilo nilituma picha ya nyumba nzuri ya ghorofa nne kwenye magroup mawili ya whatsap nikaandika ujumbe huu "Kama unaamini kuwa Mungu yupo na anaweza kupindua matokeo na ukajenga nyumba nzuri kama hii".

Group la kwanza hawakuwa na matumaini kabisaa ya kujenga nyumba kubwa yenye ghorofa 4,group la pili walijitokeza wachache waliokuwa hawana matumaini lakini waliokuwa na matumaini walikuwa ni wengi zaidi.

Ukifuatilia katika maisha yao kati ya magroup haya mawili ni ukweli usiopingika kwamba wale ambao walikuwa na hamasa ya kujenga nyumba kama hiyo wataweza kujenga angalau ya kufanana au ndogo yahiyo,wale ambao hawana hamasa kabisa wataishia kusema mimi sina mipango,mimi sio mwajiriwa,mimi siwezi na kusihia kulalamikia serikali juu ya mfumo wa ajira asanteni kwa muda wenu ANZA SASA ILI UFIKIE  NDOTO ZAKO.

"Mafanikio ni kupambana na kukuza wigo wa kipato chako."
Ni mimi kocha wako mzoefu Bundala Izengo.
 

Alhamisi, 16 Juni 2016

KAMA UNAOGOPA HAYA HUWEZI KUFANIKIWA


Kila mtu katika maisha yake anataka kufanikiwa. Kutokana umuhimu huu wa mafanikio kila mtu hujikuta akiweka juhudi kwa kile anachokifanya ili kufikia mafanikio hayo.

Lakini pamoja na juhudi zote hizo wengi wetu huwa wanashindwa kufikia mafanikio hayo kutokana na kuogopa mambo fulani fulani ambayo hawakutakiwa kuyaogopa kabisa. Kwa kuyaogopa mambo hayo na kuyakuza husababisha kushidwa kufikia mafanikio.

Hili ndilo kosa kubwa ambalo wengi wamekuwa wakifanya kwa kuogopa kitu ambacho hawakutakiwa kukiogopa  na matokeo yake husababisha kushindwa kufanya kitu ama kuchukua hatua. Kama wewe ni mjasiriamali na unayetaka mafanikio makubwa acha kuogopa kabisa mambo haya:-

 1. Kushindwa.

Mjasiriamali yoyote mwenye nia ya kufika kwenye kilele cha mafanikio siku zote haogopi kushindwa. Kama ameshindwa katika jambo hili atajaribu hili na lile mpaka kufanikiwa. Lakini siyo rahisi kuacha njia ya mafanikio eti kwa sababu alishindwa kwa mara ya kwanza.

Hiki ni kitu muhimu sana kukijua katika safari yako ya mafanikio ili we mshindi. SOMA; Mambo 6 Unayolazimika Kuyaacha Mara Moja Ili Kufanikiwa.

2. Kukosolewa.

Watu wenye mafanikio siku zote hawaogopi kukosolewa. Hawa ni watu wa kufanya mambo ambayo wanaamini yatawafanikisha na siyo kinyume cha hapo. Kama ikitokea utawakosoa, wao mara nyingi hawajali sana, zaidi wanashikilia misimamo yao. Kitu cha kujifunza hapa, acha kuumia sana na kukosolewa kwako.
Amini unachokifanya kisha songa mbele.

3. Mafanikio ya wengine.

Siku zote wajasiriamali wa kweli hawagopi mafanikio ya wajasiriamali wengine. Wanajua mafanikio ni hatua na wao watafika huko tu.
Hivyo hawatishiki sana, zaidi wanafuata mipango na malengo yao mpaka kuifanikisha. Kutokuogopa mafanikio ya wengine ni silaha kubwa sana ya kutufikisha hata sisi kwenye kilele cha mafanikio hayo, ila kwa kujiamini.

4. Kuacha kile unachokifanya.

Mara nyingi ili ufanikiwe ni lazima uwe king’ang’anizi. Sasa inapotokea mambo hayaendi sawa kama unavyotaka hakuna njia nyingine zaidi ya kuacha kile unachokifanya. Wajasiriamali wenye mafanikio makubwa huwa siyo waoga sana kuacha vile wanavyofanya.
Lakini hufanya hivyo mpaka wakishagundua hakuna mafanikio wanayaona kabisa na siyo kuacha kirahisi tu.

5. Kutengeneza pesa nyingi.

 Ili uweze kufanikiwa zaidi ni lazima ujue umuhimu wa kutengeneza pesa zaidi. Ikiwa unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa acha kabisa kuogopa kutengeneza pesa zaidi na zaidi tena na zaidi.
Inapotokea fursa ya kutengeneza pesa itendee haki kwani huo ndio msingi wa mafanikio yako makubwa ambayo unayatafuta.

6. Kujifunza.

Hauwezi kufanikiwa kwa viwango vya juu bila kujifunza. Wajasiriamali wote wenye mafanikio makubwa ni watu wa kujifunza kwenye maisha yao. Na hujifunza kupitia wenzao waliofanikiwa au kupitia vitabu.

Huu ndiyo ujasiri walionao katika hili na hawaogopi kitu. Inapotokea kuuliza, wanauliza mpaka kufanikiwa. Unaweza ukajifunza mengi na kuyashangaza ambayo watu wenye mafanikio hawaogopi kuyafanya katika maisha yao.

Chukua hatua  yakubadili maisha yako na kuanzia sasa amua kuwa miongoni mwa wana mafanikio.Ni mimi kocha wako mzoefu Bundala Izengo.

Jumapili, 12 Juni 2016

JE WAIJUA CHACHU YA MAFANIKIO?

Je, umeshawahi kujiulia chachu  ya mafanikio inapatikana wapi? Hili ni swali muhimu sana kwako kwa sababu kuna wakati katika maisha, kwa sababu ya changamoto mbalimbali huwa tunajikuta tunakosa nguvu na mwelekeo wa kusonga mbele na kushindwa kujua tufanye nini? Inapofika hali hii, wengi hukata tamaa na kusahau kuitumia nguvu kubwa ya mafanikio waliyonayo kuwafanikisha.

Kama hali hii imekukuta huna haja ya kukata tamaa tena, unaweza kutumia cachu hii kubwa uliyonayo kukufanikisha. Je, unaijua chachu hii inapatikanaje hadi kukufanikisha? Sikiliza, mafanikio yoyote unayoyatafuta yapo Kwenye Kuanza. Kama kuna jambo unataka kulifanikisha ni lazima ulianze na sio kulisubiria.

Chachu kubwa ya kuendelea na kusonga mbele inapatikana kwa kuanza. Unapokuwa unaanza jambo, sio tu unakuwa na chachu ya kuweza kulifanya bali chachu hiyo inakuwa inaongozeka siku hadi siku. CHUKUA HATUA MARA MOJA ILI KUFANIKIWA. Moja kati ya wanasayansi waliopata kuwepo katika hii dunia, Isack Newton aliwahi kulieleza hili vizuri katika sheria yake ya mwendo kwamba kitu chochote kikiwa kwenye mwendo kitaendelea kuwa kwenye mwendo huo na kitu chochote ambacho kipo katika hali ya kutulia au utulivu, kitaendelea kutulia siku zote mpaka itokee nguvu nje ya hapo ya kubadili hali hizo.

 Tafsiri au maana yake ni nini hapa? Ni kwamba kama utaamua kuchukua hatua juu ya maisha yako, utazidi kupata nguvu/chachu ya kukufanikisha kwenye mafanikio unayoyahitaji. Chochote unachotaka kukifanya kwenye maisha yako hata kiwe kikubwa vipi, siri kubwa ya kukifanikisha ipo kwenye kuanza. Mafanikio yote makubwa chini ya jua yalianza kwa kufanya kwanza na sio kusubiri. Kumbuka   ”DO THE THINGS YOU WILL HAVE THE POWER TO ACCOMPLISH IT.”

Kama kuna jambo unataka kulifanya, wewe lifanye tu acha kujiandaa sana, wala kusubiri sana kwani chachu/nguvu ya kufanikisha jambo hilo itapatikana wakati unafanya. Kama ni uzoefu mkubwa utaupata kwa kuanza.

Hivi ndivyo mafanikio makubwa yanavyopatikana kwa kuchukua hatua za utekelezaji. Tumia kanuni hii bora ikusaidie kufanikiwa kwa viwango vya juu, kumbuka siku zote unalo jukumu la kuhakikisha unakuwa bora kila siku.

FANYA MARA NYINGI,SHINDWA MARA NYINGI,JIFUNZE MARA NYINGI,UTAFIKIWA MARA NYINGI. Asanteni sana  kocha wako mzoefu Bundala Izengo.

Jumamosi, 11 Juni 2016

UINGEREZA YAJIANDAA KUZINDUA DACTARI ROBOTI



Daktari Roboti duniani karibia kuzinduliwa nchini uingereza, na mamlaka za matibabu zinasema zimeweka nia ya mashine hiyo kuanza kazi.

Daktari mwenye akili bandia (artificial intelligence) atashiriki katika mashindano na madaktari binadamu ili kupima yupi kati ya hawa wawili ana uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana kwa ufanisi zaidi kwa kupima matatizo ya afya ya kawaida kati ya wagonjwa.

Matokeo ya shindano hili yatakuwa na athari kubwa juu ya mustakabali wa afya nchini Uingereza na nje ya nchi.

Dailymail.co.uk ripoti kwamba:
British start-up firm Babylon Health itajaribu programu yake, ambayo inajulikana kama angalia tofauti kwa daktari
na muuguzi katika mashindano yakuona yupi kati yao anaweza kukabiliana kwa haraka zaidi na kwa ufanisi katika matatizo ya kawaida ya afya.

Application ya smartphone imeundwa ili kutenda kama muuguzi, ikiuliza mfululizo wa maswali, na kushauri kama tatizo alilonalo mgonjwa alina shida kitabibu, na kama itakupasa kuonana na daktari, au kama jambo hilo linahitaji msaada wa 999.
Haitoi utambuzi rasmi.

Ila watengenezaji wa app hii, wanaamini uwezo bandia utabadilisha utabibu katika miaka ijayo, walisema wanauhakika asilimia 100 programu yao itakuja kuwa juu.
Babylon Health boss Ali Parsa alisema Roboti yao inaweza kuchambua maelfu ya matatizo katika ufanisi mkubwa.

'Ni sahihi zaidi kuliko binadamu yeyote, kama vile kompyuta ilivyo zaidi kuliko binadamu yeyote, "alisema.
Algorithm yake ilitengenezwa kwa msaada wa madaktari zaidi ya 100, ambao walikuwa wakirudia kuijaribu mara kwa mara na haikutenda kosa la kujirudia.

Steve Hamblin, mkuu wa timu ya Babylon artificial intelligence, alisema: "Si kwamba ni kwa ajili ya kuchukua nafasi ya madaktari, ilo sio lengo letu. Mimi sipo katika biashara ya kuweka daktari nje ya biashara. Mimi nipo katika biashara ya kuwa-boost. '

SHIGONGO ATAJWA KUWA MMOJA WA MABILIONEA AFRICA

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers and Enterprises Limited, Eric James Shigongo ametajwa kwenye makala ya African Billionaires kuwa yumo kwenye orodha ya miongoni mwa mabilionea wa Afrika ambapo katika orodha hiyo yumo pia bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote wa Nigeria.

Katika makala hiyo inayoandaliwa na Stella Monica Mpande, Phd na kurushwa kupitia Chaneli ya Ndiho Media ya Uganda iliangazia zaidi kuhusu ubunifu katika biashara na teknolojia, imeeleza kuwa, Eric Shigongo ni miongoni mwa wafanyabiashara wabunifu zaidi na wanaoendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.

Aifrican Billionaires imeeleza kuwa, miongoni mwa biashara zilizompatia mafanikio zaidi Shigongo ni vyombo vya habari ikiwemo uchapishaji wa magazeti ya Amani, Championi, Ijumaa, Risasi, pamoja na Uwazi. Biashara za hoteli, nyumba za kupangisha, pamoja na kilimo.

Aifrican Billionaires pia imetaja sababu za mafanikio ya Shigongo kuwa ni mtu mwenye uthubutu, kujituma, kubuni vitu vipya na kuviendesha kwa ufanisi. Kuwasaidia watu wenye shida pamoja na kuwa mwalimu mahili wa ujasiliamali na mhamasishaji ndivyo vimemfanya afanikiwe kutoka kwenye umaskini hadi utajiri.

Shigongo ameingia kwenye orodha ya Mabilionea wa Afrika ambao wamo bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote  wa Nigeria anayemiliki viwanda na kuendesha biashara ya saruji, na sukari sehemu mbalimbali duniani.

Yumo pia  Gordon Wavamunno raia wa Uganda anayemiliki vyombo vya habari, usafiri na shule na Tribert Rujugiro Ayabatwa, Mrwanda  anayemiliki maduka ya super market, viwanda vya saruji, chai na tumbaku.
Najihisi mwenye furaha mtu wangu wa mfano/kuigwa kutajwa kuwa ni mmoja wa matajiri Afrika,MUNGU ENDELEA KUMPATIA ZAIDI NZ ZAIDI

Alhamisi, 9 Juni 2016

MTI WA AJABU WAONEKANA TANGA

Hali ya kushangazi imejitokeza mkoani Tanga na kusababisha mjadala mzito katika mitandao ya kijamii baada ya kuibuka swala la mti kufanana na Mwalimu Nyerere  na upande wa pili mama maria Nyerere mkoani Tanga maeneo ya Tangamano... Embu jionee mwenyewe kama kunaukweli juu ya swala hili..
 

Jumanne, 7 Juni 2016

FUNGA KWA KUZINGATIA HAYA

Utangulizi

Sifa zote njema zinamstahikia Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na sala na salamu zimfikie Mtume wake (Swalla Allahu alayhi Wasallam) pamoja na ndugu na maswahaba zake.Baada ya kumshukuru  Allah (Subhaanahu Wata’ala)  na kumtakia rehma na amani Mtume Muhammad (Swalla Allahu alayhi Wasallam) pamoja na ndugu zake na maswahaba zake wote, basi kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu (Subhaanahu Wata’ala)  amejaalia kwa waja wake  miongo [misimu] ya kuzidisha ndani yake matendo mema  na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala)  huzidisha pia malipo ya matendo hayo kwa waja wake, na miongoni mwa miongo hiyo ni huu  mwezi mtukufu wa Ramadhani.Basi katika makala haya nitaelezea kwa ufupi juu ya funga na yale yanayoambatana nayo ikiwa ni pamoja na  hukumu, fadhila na adabu zake.

Ninamwomba Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)  awanufaishe Waislamu kwa yale nitakayoyaelezea, na aturuzuku ikh-laswi [kutaka radhi zake pekee] katika matendo yetu yote,  amiiin.
Kwake pekee ndiyo kwenye mafanikio ya dunia na akhera.Maana ya FungaNeno swaumu ambalo ni funga katika lugha ya Kiswahili,   kilugha lina maana ya  kujizuilia.

Ama katika sheria, funga [swaumu] ni kumuabudu Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala)  kwa kujizuilia na vyenye kufuturisha [kufunguza] kuanzia kudhihiri alfajiri  [ya pili] mpaka kuchwa [kuzama] kwa jua na kwa kunuilia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala).

Historia ya Funga

Kwa hakika funga si ibada ngeni, bali ni ibada iliyofaradhishwa kwa umati zilizotangulia na pia kufaradhishwa katika umati huu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {{Enyi mlioamini! mmelazimishwa kufunga [saumu] kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu}} (2:183).Ama katika umati huu wa Muhammad (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) funga  ilifaradhishwa katika mwezi wa Shaaban mwaka wa pili baada ya Hijrah (2H).

Funga kwa kuombea mafanikio
Ewe ndugu katika imani hii,unapoingia mwezi huu wa Ramadhani funga kwa toba,kuombea mafanikio katika maisha yako,familia yako na taifa lako naye Mungu  (Subhaanahu wa Ta’ala) atakusikia na kutimiza ndoto zako za kila siku.

NAKUTAKIA MFUNGO MWEMA NA MUNGU AKUONGOZE.