Jumamosi, 11 Juni 2016

SHIGONGO ATAJWA KUWA MMOJA WA MABILIONEA AFRICA

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers and Enterprises Limited, Eric James Shigongo ametajwa kwenye makala ya African Billionaires kuwa yumo kwenye orodha ya miongoni mwa mabilionea wa Afrika ambapo katika orodha hiyo yumo pia bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote wa Nigeria.

Katika makala hiyo inayoandaliwa na Stella Monica Mpande, Phd na kurushwa kupitia Chaneli ya Ndiho Media ya Uganda iliangazia zaidi kuhusu ubunifu katika biashara na teknolojia, imeeleza kuwa, Eric Shigongo ni miongoni mwa wafanyabiashara wabunifu zaidi na wanaoendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.

Aifrican Billionaires imeeleza kuwa, miongoni mwa biashara zilizompatia mafanikio zaidi Shigongo ni vyombo vya habari ikiwemo uchapishaji wa magazeti ya Amani, Championi, Ijumaa, Risasi, pamoja na Uwazi. Biashara za hoteli, nyumba za kupangisha, pamoja na kilimo.

Aifrican Billionaires pia imetaja sababu za mafanikio ya Shigongo kuwa ni mtu mwenye uthubutu, kujituma, kubuni vitu vipya na kuviendesha kwa ufanisi. Kuwasaidia watu wenye shida pamoja na kuwa mwalimu mahili wa ujasiliamali na mhamasishaji ndivyo vimemfanya afanikiwe kutoka kwenye umaskini hadi utajiri.

Shigongo ameingia kwenye orodha ya Mabilionea wa Afrika ambao wamo bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote  wa Nigeria anayemiliki viwanda na kuendesha biashara ya saruji, na sukari sehemu mbalimbali duniani.

Yumo pia  Gordon Wavamunno raia wa Uganda anayemiliki vyombo vya habari, usafiri na shule na Tribert Rujugiro Ayabatwa, Mrwanda  anayemiliki maduka ya super market, viwanda vya saruji, chai na tumbaku.
Najihisi mwenye furaha mtu wangu wa mfano/kuigwa kutajwa kuwa ni mmoja wa matajiri Afrika,MUNGU ENDELEA KUMPATIA ZAIDI NZ ZAIDI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni