Jumatatu, 4 Juni 2018
TABIA MUHIMU ZA MWANADAMU KUFIKIA MAFANIKIO
Kila niangaliapo na kuzichunguza tabia za watu fulani hunipa jibu kuwa kuna tofauti kubwa za tabia za watu katika maisha ya mafanikio.Tabia hizo huonekana pale ambapo mtu anapopata pesa nyingi na pia anapokosa pesa.Wahenga walisema "Pata pesa ujue tabia yako"Hii inamaanisha kuwa watu wengi wakipata pesa hubadilika tabia,hubadilika staili ya mavazi,hubadilika kuongea kwao,hubadilika kutembea kwao.
Leo katika makala haya nimekuletea tabia kuu tatu ambazo mwanadamu anazo wakati akipata pesa.Tabia hizi zinaakisi mwenendo mzima wa maisha ya wanadamu wote na ndio tabia kuu zilizoidhinishwa na Chuo kikuu cha kimataifa cha Havard.
1:MTUMIAJI
Huyu ni mtu ambaye akipata pesa huwaza kutumia kwa anasa na mambo mengine ambayo hayana maaana katika maisha yake.
Mtu huyu hajui ya kesho wala hajui kuwa kuna kukosa hivyo hudumia pesa yake kwa anasa za kila aina ambazo hazina faida katika maisha yake.
Kama ulishawahi sikia stori za mtu akikuambia kuwa
"Hapo zamani nilikuwa nahudhuria katika baa ya DDC kila siku ya jumamosi na jumapili"
"Nilikuwa nalipwa Shilingi ELfu hamsini,mshahara wangu ulilingana na mshahara wa mkurugenzi"
Chunguza maisha ya mtu huyo aliyekuwa akihudhuria Baa kila siku za mapumziko kuwaangalia Jazz Band na kucheza muziki,Juhudi alizoweka kuangalia Muziki ngeweka kuatika uweklezaji angekuwa na mali nyingi pengine kuliko alizonazo sasa.
2: MTUNZAJI
Huyu ni mtu yule ambaye anaenda kutunza pesa benki kwa muda mrefu pasipo kumzalishaia kwa Lugha ya uswahilini watu hawa wanaitwa "wabahili" Mara nyingi watu hawa husikitika sana pale wanapoona pesa zao zikitumika kwa uzalishaji,hufikiri kuwa pesa ikiwekezwa inaweza kupotea na asiipate nyingine tena.
Mara kwa mara watu hawa hutunza pesa zao kwenye maroba,mabenki au huchimbia chini ya ardhi,huishi maisha ya kawaida kabisa ambayo si rahisi mtu mwingine kumjua kama ana kiasi kikubwa cha pesa.
3: MWEKEZAJI
Mtu mwenye tabia hii ndio mwenye mafanikio makubwa,watu hawa ndio wanaoongoza dunia,ndio wanaomiliki mali nyingi na kumiliki viwanda vikubwa ambavyo ndio hutoa ajira nyingi.Watu wenye tabia hii hutamani kuwekeza kila pesa inayopita mikononi mwao,wako tayari kuwekeza pengine wasibakiwe hata na shilingi mikononi mwao.
Hizi ndio tabia kuu tatu ambazo mwanadamu amezaliwa nazo,tabia hizi zinaweza kubadilika kulingana na mazingira uliyonayo ingawa haziwezi kufutika kabisa.
Mara nyingi tabia hizi hubadilika na kukomaa pale unapoambatana na mwenye tabia kama yako,hushindwa kukomaa na hubadilika kutoka kwenye tabia nyingine pale unapoambatana na mtu mwenye tabia isiyofanana na tabia yako.
Asante sana wako Bundala Abely Izengo
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni