Je, umeshawahi kujiulia chachu ya mafanikio inapatikana wapi? Hili ni swali muhimu sana kwako kwa sababu kuna wakati katika maisha, kwa sababu ya changamoto mbalimbali huwa tunajikuta tunakosa nguvu na mwelekeo wa kusonga mbele na kushindwa kujua tufanye nini? Inapofika hali hii, wengi hukata tamaa na kusahau kuitumia nguvu kubwa ya mafanikio waliyonayo kuwafanikisha.
Kama hali hii imekukuta huna haja ya kukata tamaa tena, unaweza kutumia cachu hii kubwa uliyonayo kukufanikisha. Je, unaijua chachu hii inapatikanaje hadi kukufanikisha? Sikiliza, mafanikio yoyote unayoyatafuta yapo Kwenye Kuanza. Kama kuna jambo unataka kulifanikisha ni lazima ulianze na sio kulisubiria.
Chachu kubwa ya kuendelea na kusonga mbele inapatikana kwa kuanza. Unapokuwa unaanza jambo, sio tu unakuwa na chachu ya kuweza kulifanya bali chachu hiyo inakuwa inaongozeka siku hadi siku. CHUKUA HATUA MARA MOJA ILI KUFANIKIWA. Moja kati ya wanasayansi waliopata kuwepo katika hii dunia, Isack Newton aliwahi kulieleza hili vizuri katika sheria yake ya mwendo kwamba kitu chochote kikiwa kwenye mwendo kitaendelea kuwa kwenye mwendo huo na kitu chochote ambacho kipo katika hali ya kutulia au utulivu, kitaendelea kutulia siku zote mpaka itokee nguvu nje ya hapo ya kubadili hali hizo.
Tafsiri au maana yake ni nini hapa? Ni kwamba kama utaamua kuchukua hatua juu ya maisha yako, utazidi kupata nguvu/chachu ya kukufanikisha kwenye mafanikio unayoyahitaji. Chochote unachotaka kukifanya kwenye maisha yako hata kiwe kikubwa vipi, siri kubwa ya kukifanikisha ipo kwenye kuanza. Mafanikio yote makubwa chini ya jua yalianza kwa kufanya kwanza na sio kusubiri. Kumbuka ”DO THE THINGS YOU WILL HAVE THE POWER TO ACCOMPLISH IT.”
Kama kuna jambo unataka kulifanya, wewe lifanye tu acha kujiandaa sana, wala kusubiri sana kwani chachu/nguvu ya kufanikisha jambo hilo itapatikana wakati unafanya. Kama ni uzoefu mkubwa utaupata kwa kuanza.
Hivi ndivyo mafanikio makubwa yanavyopatikana kwa kuchukua hatua za utekelezaji. Tumia kanuni hii bora ikusaidie kufanikiwa kwa viwango vya juu, kumbuka siku zote unalo jukumu la kuhakikisha unakuwa bora kila siku.
FANYA MARA NYINGI,SHINDWA MARA NYINGI,JIFUNZE MARA NYINGI,UTAFIKIWA MARA NYINGI. Asanteni sana kocha wako mzoefu Bundala Izengo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni