Utangulizi
Sifa zote njema zinamstahikia Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na sala na salamu zimfikie Mtume wake (Swalla Allahu alayhi Wasallam) pamoja na ndugu na maswahaba zake.Baada ya kumshukuru Allah (Subhaanahu Wata’ala) na kumtakia rehma na amani Mtume Muhammad (Swalla Allahu alayhi Wasallam) pamoja na ndugu zake na maswahaba zake wote, basi kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu (Subhaanahu Wata’ala) amejaalia kwa waja wake miongo [misimu] ya kuzidisha ndani yake matendo mema na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) huzidisha pia malipo ya matendo hayo kwa waja wake, na miongoni mwa miongo hiyo ni huu mwezi mtukufu wa Ramadhani.Basi katika makala haya nitaelezea kwa ufupi juu ya funga na yale yanayoambatana nayo ikiwa ni pamoja na hukumu, fadhila na adabu zake.
Ninamwomba Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) awanufaishe Waislamu kwa yale nitakayoyaelezea, na aturuzuku ikh-laswi [kutaka radhi zake pekee] katika matendo yetu yote, amiiin.
Kwake pekee ndiyo kwenye mafanikio ya dunia na akhera.Maana ya FungaNeno swaumu ambalo ni funga katika lugha ya Kiswahili, kilugha lina maana ya kujizuilia.
Ama katika sheria, funga [swaumu] ni kumuabudu Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa kujizuilia na vyenye kufuturisha [kufunguza] kuanzia kudhihiri alfajiri [ya pili] mpaka kuchwa [kuzama] kwa jua na kwa kunuilia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala).
Historia ya Funga
Kwa hakika funga si ibada ngeni, bali ni ibada iliyofaradhishwa kwa umati zilizotangulia na pia kufaradhishwa katika umati huu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {{Enyi mlioamini! mmelazimishwa kufunga [saumu] kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu}} (2:183).Ama katika umati huu wa Muhammad (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) funga ilifaradhishwa katika mwezi wa Shaaban mwaka wa pili baada ya Hijrah (2H).
Funga kwa kuombea mafanikio
Ewe ndugu katika imani hii,unapoingia mwezi huu wa Ramadhani funga kwa toba,kuombea mafanikio katika maisha yako,familia yako na taifa lako naye Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) atakusikia na kutimiza ndoto zako za kila siku.
NAKUTAKIA MFUNGO MWEMA NA MUNGU AKUONGOZE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni