Jumamosi, 2 Juni 2018

KUWA MWANDISHI WA FILAMU YA MAISHA YAKO



Uandishi ni moja ya kazi ambayo inahusu kukusanya habari na kuzichambua kwa kina kwa dhumuni la kutaarifu umma,lakini kwenye makala haya namwelezea mwandishi wa filamu ambaye anaandika filamu ya muongozo wa maisha yake ambaye ni wewe,ndio wewe ni mwandishi mzuri au mbaya wa filamu ya maisha yako.

Mwandishi mjuzi wa filamu huandaa mwongozo mzuri kuanzia mwanzoni na mwisho wa filamu yake,hupangilia wahusika katika vipengele mbalimbali vya filamu husika.Mwandishi huandaa muongozo wa filamu ambayo huanza kumpa picha halisi kabla ya kuanza kuicheza filamu hiyo.

Katika kuandika filamu ya maisha yako,wewe kama mwandishi ni lazima uwe na washiriki wakubwa watatu ambao ndio hukamilisha sinema ya maisha yako.

1)MTAZAMAJI

Huyu ni mtu ambaye anatizama jinsi ambavyo sinema ya maisha ya wengine inavyoendelea, huyu hukubali na kupongeza baadhi ya vipande vya maisha ya wengine na kuviponda au kuvikosoa baadhi ya vipande hivyo.Aina hii ya watu ni watu wa kwenye vijiwe vya kahawa,bao au kamali huwa ni watu wa kutoa maoni juu ya maisha ya watu,hawa ni watu walio duni katika maisha yao,watu wasio kuwa na ndoto katika maisha yao.

Ni watu ambao hawajuo kupambanua nyakati hukosoa juhudi za watu wengine.

Mfano "Fulani kanunua gari amehongwa na mtu fulani:" autasikia

"Huyu ana nyumba nzuri ameibia kampuni fulani"
Epuka vikao vya watazamaji hawa ambao wanatazama filamu za wengine zikiendelea mbele.

2) MWIGIZAJI

Mwigizaji ni mhusika mkuu katika filamu ya maisha na anajua kuwa yeye ni mhusika mkuu na anaweza kuongoza sehemu kubwa ya filamu ya maisha yake.Anaweza kujenga au kubomoa filamu ya maisha yake kwa jinsi ambayo anaweza kuuvaa uhusika katika maisha na jinsi ambavyo anaweza kuusaliti uhusika wake.

Mwigizaji huwa na furaha katika maisha yake kwa sababu anajua kuwa yeye ni mshindi na ufurahia maisha ya aina yoyote ile pia hufahamu kabisa kuwa filamu ya maisha yake inaweza kuisha kwa namnna yeyote ile na yuko tayari kwa lolote.

3) MWANDISHIA MWIGIZA

Huyu ni mtu yule ambaye haangalii tu na haigizi tu lakini ni yule ambaye anatengeneza sinema kutoka kichwani kwake.anajua nini ataongea,atafanya kipi na mwisho wa sinema utakuaje .

Mtu huyu ana uwezo mkubwa wa kuendesha maisha yake na anajua kabisa maisha yake yatakuwa mazuri au mabaya.

Mtu huyu huwa makini sana katika kujenga maisha yake.Watu wengi waliofanikiwa wapo katika kundi hili,ni waandishi,waigizaji na waongozaji katika sinema za maisha yao.

Swali la kujiuliza

Je wewe ni mtizamaji?

Je wewe ni mwigizaji ambae unaigza kwenye filamu usiyoijua mwisho wake?

Au wewe ni mwandishi na mwongozaji wa filamu ya maisha yako?

Maisha yako, yako mikononi mwako ni wajibu wako sasa kutengeneza au kubomoa,kuwa mwandishi,mwigizaji au mtazamaji.

Asante sana kwa muda wako kwa kusoma makala haya.

Ndimi Bundala Izengo 0656669989.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni