Alhamisi, 16 Juni 2016

KAMA UNAOGOPA HAYA HUWEZI KUFANIKIWA


Kila mtu katika maisha yake anataka kufanikiwa. Kutokana umuhimu huu wa mafanikio kila mtu hujikuta akiweka juhudi kwa kile anachokifanya ili kufikia mafanikio hayo.

Lakini pamoja na juhudi zote hizo wengi wetu huwa wanashindwa kufikia mafanikio hayo kutokana na kuogopa mambo fulani fulani ambayo hawakutakiwa kuyaogopa kabisa. Kwa kuyaogopa mambo hayo na kuyakuza husababisha kushidwa kufikia mafanikio.

Hili ndilo kosa kubwa ambalo wengi wamekuwa wakifanya kwa kuogopa kitu ambacho hawakutakiwa kukiogopa  na matokeo yake husababisha kushindwa kufanya kitu ama kuchukua hatua. Kama wewe ni mjasiriamali na unayetaka mafanikio makubwa acha kuogopa kabisa mambo haya:-

 1. Kushindwa.

Mjasiriamali yoyote mwenye nia ya kufika kwenye kilele cha mafanikio siku zote haogopi kushindwa. Kama ameshindwa katika jambo hili atajaribu hili na lile mpaka kufanikiwa. Lakini siyo rahisi kuacha njia ya mafanikio eti kwa sababu alishindwa kwa mara ya kwanza.

Hiki ni kitu muhimu sana kukijua katika safari yako ya mafanikio ili we mshindi. SOMA; Mambo 6 Unayolazimika Kuyaacha Mara Moja Ili Kufanikiwa.

2. Kukosolewa.

Watu wenye mafanikio siku zote hawaogopi kukosolewa. Hawa ni watu wa kufanya mambo ambayo wanaamini yatawafanikisha na siyo kinyume cha hapo. Kama ikitokea utawakosoa, wao mara nyingi hawajali sana, zaidi wanashikilia misimamo yao. Kitu cha kujifunza hapa, acha kuumia sana na kukosolewa kwako.
Amini unachokifanya kisha songa mbele.

3. Mafanikio ya wengine.

Siku zote wajasiriamali wa kweli hawagopi mafanikio ya wajasiriamali wengine. Wanajua mafanikio ni hatua na wao watafika huko tu.
Hivyo hawatishiki sana, zaidi wanafuata mipango na malengo yao mpaka kuifanikisha. Kutokuogopa mafanikio ya wengine ni silaha kubwa sana ya kutufikisha hata sisi kwenye kilele cha mafanikio hayo, ila kwa kujiamini.

4. Kuacha kile unachokifanya.

Mara nyingi ili ufanikiwe ni lazima uwe king’ang’anizi. Sasa inapotokea mambo hayaendi sawa kama unavyotaka hakuna njia nyingine zaidi ya kuacha kile unachokifanya. Wajasiriamali wenye mafanikio makubwa huwa siyo waoga sana kuacha vile wanavyofanya.
Lakini hufanya hivyo mpaka wakishagundua hakuna mafanikio wanayaona kabisa na siyo kuacha kirahisi tu.

5. Kutengeneza pesa nyingi.

 Ili uweze kufanikiwa zaidi ni lazima ujue umuhimu wa kutengeneza pesa zaidi. Ikiwa unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa acha kabisa kuogopa kutengeneza pesa zaidi na zaidi tena na zaidi.
Inapotokea fursa ya kutengeneza pesa itendee haki kwani huo ndio msingi wa mafanikio yako makubwa ambayo unayatafuta.

6. Kujifunza.

Hauwezi kufanikiwa kwa viwango vya juu bila kujifunza. Wajasiriamali wote wenye mafanikio makubwa ni watu wa kujifunza kwenye maisha yao. Na hujifunza kupitia wenzao waliofanikiwa au kupitia vitabu.

Huu ndiyo ujasiri walionao katika hili na hawaogopi kitu. Inapotokea kuuliza, wanauliza mpaka kufanikiwa. Unaweza ukajifunza mengi na kuyashangaza ambayo watu wenye mafanikio hawaogopi kuyafanya katika maisha yao.

Chukua hatua  yakubadili maisha yako na kuanzia sasa amua kuwa miongoni mwa wana mafanikio.Ni mimi kocha wako mzoefu Bundala Izengo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni