Jumamosi, 18 Juni 2016

KANUNI ZA MAFANIKIO


Kanuni ni desturi,taratibu au kaidi ambazo hazina budi kufuatwa ili uweze kupata matokeo fulani ambayo umekusudia.Kanuni za mafanikio ni taratibu ambazo unatakiwa kuzifanya ili kuweza kupata matokeo mazuri katika jambo au ndoto fulani.

Nilipokiwa mdogo,nilijua kuwa mafanikio ni kuwa na magari mengi,majumba,ng'ombe au mashamba.Kumbe maana halisi ya mafanikio ni kupanda kutoka hatua moja kwenda nyingine kiuchumi,kiimani na kimasomo.

Kila kukicha watu wamekuwa wakitafuta mafanikio kwa kufanya kazi kwa bidii sana lakini hujikuta wakilalamika kuwa wameshindwa kupata mafanikio makubwa kwa sababu ya kushindwa kufuata utaratibu na kanuni za kupata mafanikio.Sababu nyingi zinaweza kuzuilika kwa mfano matumizi mabaya ya pesa,matumizi mabaya ya Muda n.k.
Matumizi mabaya yapesa yamekuwa ni kilio kikubwa kwa watu wengi ambao wamekuwa wakifanya manunuzi ya vitu bila kufikiria faida na hasara ya vitu hivyo?

Ni ukweli usio na shaka kuwa vijana wengi wamekuwa wakifanya matumizi makubwa kwa sababu ya kumuangalia mtu fulani anacho au sababu ya msanii fulani kavaa hivi bila kupima faida na hasara za kitu kile.Mfano Ninamiliki komputer mpakato na kamera kwa sababu ni mwandishi wa habari,vitabu,blog nk bila vifaa hivyo siwezi kufanya lolote.Nahisi huo ndio mfano mzuri amabao unaweza kukusaidia.
Ili kufanikiwa katika maisha ni lazima ufuate kanuni na taratib zifuatazo.

1. Tambua kuwa maisha ni kanuni

Hakuna aliyezaliwa na kuanza kutembea au kukimbia,jinsi maisha ya mtoto mchanga anavyopitia katika hatua ya kupakatwa mikononi,kukaa,kutambaa,kutembea,kukimbia na mwisho wa siku kupaa kulingana na imani yake ndivyo ilivyo hata katika kanuni ya Mafanikio.(Soma MFANANO WA KANUNI ZA MAFANIKIO NA UKUAJI WA MTOTO)kwenye makala zijazo.

Maisha ya mafanikio ya kweli na ya kuduma huja kwa mtiririko huo unaofananishwa na ukuaji wa mtoto mdogo,hata leo hii kuna wengine wanalelewa,wengine wanakaa,wengine wanatambaa,wengine wanakimbia na wengine walishapaa.

Hakuna aliyewahi kuruka kanuni hiyo hata moja na kuendelea kuwa tajiri milele.Ni juhudi peke yake zinaweza kukutoa hapo kwenye kutambaa au kukimbia na kukupeleka kwenye kupaa.

2. TUMIA KICHACHE WEKA KINGI

Kanuni hii ndio ambayo watu wengi inawashinda,hata mimi ilinisumbua sana na kushindwa kuelewa pesa niliokuwa naipata imekwenda wapi.Niliwaza mengi mpaka nilihusisha imani za kishirikina na kumsingizia mdudu mmoja ambae ana jina linalosifika la CHUMA ULETE.

Kumbe katika maisha hakuna chuma ulete,chuma ulete ni matumizi yako mwenyewe.Niliweza kutatua changamoto hii kwa kusoma vitabu mbalimbali vya ujasiliamali,kuhudhuria semina na kuendelea kujifunza zaidi kwa waliofanikiwa.

3. UJASIRI

Kuwa na mafanikio makubwa si lelemama,inahitaji ujasiri mkubwa sana katika maamuzi ya kuwekeza katika miradi mbalimbali.Hakuna tajiri ambaye aliwahi kuwa milionea bila kuwa jasiri wa kuthubutu,hebu jiulize msomaji wangu usingethubutu kuingia Darasani na kujifunza kusoma pengine hata kusoma makala hii usingeweza,hivyo basi bila ujasiri kusingekuwepo na matajiri duniani.

4. ISHI MAISHA YA KAWAIDA

Tatizo hili liko sana katika nchi za ulimwengu wa tatu hasa Afrika,kuishi maisha ya kawaida ambayo mtu wa kawaida anaishi inasaidia kwa mbaya wako kushindwa kujua kuwa unamiliki mali nyingi na una mafanikio makubwa.

Pia itakusaidia kujifunza mengi juu ya mambo mbalimbali ya jamii inayokuzunguka.
Mfano niliwahi kumuona tajiri mwenye magorofa kariakoo sikuamini macho yangu,kuongea kwake,kuvaa kwake kutembea kwake hakutofautiana na watu wengine hata kidogo.

5.AMINI KUWA UNAWEZA

Imani ni kuwa na hakika ya mambo uyatarajiayo baina ya mambo yasiyoonekana.Imani inajengwa katika akili ya mtu/moyo wa mtu kwanza ndipo inapelekwa katika vitendo.Kama ndoto yako ni kujenga nyumba kubwa amini hivyo na ishi ukiiwaza nyumba hiyo.

Watanzania wengi tumekuwa ni wepesi wa kukata tamaa  na kulalamika huku  tukijiwekea mikwamo ya kimaendeleo katika mioyo yetu na maneno yetu.Katika kuliangazia hilo nilituma picha ya nyumba nzuri ya ghorofa nne kwenye magroup mawili ya whatsap nikaandika ujumbe huu "Kama unaamini kuwa Mungu yupo na anaweza kupindua matokeo na ukajenga nyumba nzuri kama hii".

Group la kwanza hawakuwa na matumaini kabisaa ya kujenga nyumba kubwa yenye ghorofa 4,group la pili walijitokeza wachache waliokuwa hawana matumaini lakini waliokuwa na matumaini walikuwa ni wengi zaidi.

Ukifuatilia katika maisha yao kati ya magroup haya mawili ni ukweli usiopingika kwamba wale ambao walikuwa na hamasa ya kujenga nyumba kama hiyo wataweza kujenga angalau ya kufanana au ndogo yahiyo,wale ambao hawana hamasa kabisa wataishia kusema mimi sina mipango,mimi sio mwajiriwa,mimi siwezi na kusihia kulalamikia serikali juu ya mfumo wa ajira asanteni kwa muda wenu ANZA SASA ILI UFIKIE  NDOTO ZAKO.

"Mafanikio ni kupambana na kukuza wigo wa kipato chako."
Ni mimi kocha wako mzoefu Bundala Izengo.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni