Shinyanga. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Mika Nyange amesema vimeokotwa vipande vya miili ya binadamu Mtaa wa Butengwa, baada ya makaburi ya Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga kufukuliwa na fisi.
“Baada ya taarifa kupatikana askari walifika eneo la tukio na kujionea makaburi yakiwa yamefukuliwa, hivyo tukawataka wananchi kushirikiana kufukia miili hiyo,” amesema Nyange.
Mjumbe wa Mtaa wa Butengwa, Peter Joseph amesema alipewa taarifa ya kuonekana kwa miili hiyo ikiwa inatafunwa na mbwa.
Mjumbe wa Mtaa wa Mageuzi, Kata ya Ngokolo, Mhoja Pius amelalamikia Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kutosimamia vizuri mazishi ya watu wasiokuwa na ndugu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni