Ijumaa, 29 Aprili 2016

ZIJUE FAIDA NA HASARA ZA UVAAJI WA BIKINI

Vazi la bikini limekuwa ni vazi maarufu sana duniani,vazi hili limekuwa likivaliwa katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea na huvaliwa sehemu maalumu kama ufukweni,clab,michezo ya kuogelea,riadha,tenesi,chumbani nk.


Bikini iligunduliwa 5 July 1946 na mbunifu wa mavazi wa ufaransa Lous Reard.Vazi la bikini lilioneshwa kwa mara ya kwanza na mwogeleaji Milcheline Bernadini kwenye mashindano ya kuogelea  Prscine Malitor katika jiji la Paris.

Vazi hili limekuwa likipingwa vikali katika nchi mbalimbali hasa za Afrika kwani limekuwa likidharirisha jinsia ya kike hasa linapotumika sehemu ambayo si mahali pake.Vazi hili limekuwa likiachia maungo ya mwanamke hadharani na kuleta msisimko wa mwili kwa wanaume wenye maadili mema.

Wanaume wengi wamekuwa wakivutiwa na vazi hili na kupatwa na msisimko zaidi pale anapomuona mwanamke akiwa katika vazi hili na kufikiria kuwa wanawake wanovaa vazi la ndani la bikini  ni wazuri zaidi ya wanaovaa chupi/nguo za ndani za kawaida hivyo wengi hujikuwa wakiingia katika uchaguzi mbaya wa wachumba kwa sababu ya kuangalia mavazi.

                             YAFUATAYO NI MADHARA YA KUVAA BIKINI

  • Japokuwa wanasayansi na watafiti wa mambo ya mavazi wamethibitisha kuwa hakuna madhara makubwa yanayotokana na uvaaji wa bikini,lakini vazi hili likivaliwa mahali ambapo si mahali pake linaweza kusababisha madhara yafuatayo
  • Wanaume wengi ni wadhaifu,miili yao ni myepesi kushikwa na ashki hivyo unaweza kusababisha akashindwa akujizuia akakubaka. 
  • Usumbufu hasa kwa wanaume ambao ni wepesi kushikwa na ashki.
  • Wanawake wengi wanaovaa bikini hujikuta na michubuka hasa katika sehemu za mifereji ya juu ya hajakubwa. 


                             FAIDA ZA KUVAA BIKINI

  •  Kwa wale waliolewa,wachumba bikini huleta ushawishi mkubwa hasa kwa wanaume wa kufanya tendo la baba na mama.
  • Husaidia kupunguza joto ambalo linaweza kuleta fangazi sehemu za siri.
Kama una faida au hasara za ziada,maoni na ushauri kuhusu makala haya andika maoni yako nitayafanyia kazi. Tuma kwenye watsap no 0656669989

Ijumaa, 22 Aprili 2016

ZIJUE SIFA KUU ZA UPENDO WA KWELI

Sifa kuu nne (4) za Upendo wa Kweli


  • Hauangalii hali ya mtu ya nje.
  • Hauna masharti yoyote ya kupenda.
  • Hauna kipimo au kiwango cha kupenda.
  • Hauna mwisho au kikomo cha kupenda.

NB.Aina hizi za upendo zinatumika katika maisha ya mwanadamu kila siku,mfano upendo wa kimahaba Ero’s ni upendo ambao ni muhimu katika ndoa,shauku yenye kina kirefu na urafiki Phileo huimarika kati ya wanandani na huimarishwa na upendo Agape ambao hustawisha na  kuimarisha mahusiano mema kati ya wanadamu.

UPENDO WA KWELI HUJENGWA NA MAMBO YAFUATAYO.

  • Una nguvu ya kuwa na shauku ya ashki 
  • Upendo hutaka kutoa
  • Lengo kuu ni kumtii Mungu
  • Hujinyima ili kuwatanguliza wengine
  • Upo tayari kungoje wakati wa Mungu atakaporuhusu
  • Kusubili wakati
  • Uko tayari kuchukua majukumu yanayoendana  na ashki ya kumpenda yeye,pamoja na watoto wake,familia yake kwa maisha yote.Upendo ni maisha ambayo yako tayari kujitoa kwa kila hali.
  • Kutafuta furaha na wema kwa mtu ambaye anapendwa.
  • Upendo hautaki na hautaleta aibu kwa yule ambaye anapendwa.
  • Upendo ni baraka kutoka kwa Mungu.
  • Upendo unadumu maisha yote.

UPENDO NA TAMAA YA MWILI

  • Ina nguvu ya kuwa na ashki
  • Hutaka kupokea tu 
  • Kutaka kumuasi Mungu
  • Hujinufaisha kutaka kuwatangulioza
  • Haungojei wakati wa Mungu
  • Hauko tayari kuchukua majukumu ambayo yanaendana na ashki.
  • Hutafuta kujifurahisha
  • Hajali kama italeta aibu kwa mtu mwingine
  • Ni laana mbaya ya dhambi
  • Hutoweka baada ya jambo kutokea.

Jumatano, 20 Aprili 2016

JE NI UPENDO WA KWELI AU TAMAA ZA MWILI?

U hali gani mpendwa msomaji wa patamambo karibu katika makala haya,kwa upande wangu mimi ni mzima wa afya njema,namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuamka salama na mwenye afya bora kabisa. Kilichonishawishi zaidi mpaka kuandika makala haya ni mahusiano feki ambayo yanaanzishwa na vijana baada ya kuona maono feki yanayosukumwa na tamaa za mwili.

 UPENDO WA KWELI Upendo ni hali ya kuvutiwa au kuingiwa moyoni na mtu au kitu,mtu hutamani kupendwa anapozaliwa hadi kufa,mtu huishi kwa furaha anapopendwa na hata hudhoofika na kufa asipopendwa. Tangu dunia kuumbwa hakuna aliyeweza kutoa maana halisi ya neno upendo,hii ni kwa sababu upendo ni hisia ambayo iko ndani ya moyo wa mtu hivyo ni vigumu kuelezea jinsi anavyompenda mtu fulani.

 Bwana Haleni Limbark ni mtaalamu wa saikolojia na mapenzi anaelezea upendo kuwa ni pale mtu anapomjali mwenzake na kusimama kwa ulinganifu katika jambo lolote linalohitaji uaminifu. Upendo una heshima, hukufanya kumsaidia mtu katika hali zote za maisha yake, kumhifadhi kutoka kwa maadui, na kujua kuwa akili ya kila moja kati ya wapendanao ipo hapo kwa asilimia mia moja, kujisikia salama kwake, kujivuna unapokuwa naye, kushirikishana katika matarajio na ndoto za kila mmoja na mambo yote mazuri.

 Upendo wa kweli ni upi huo? Upendo wa kweli hauchoshi, upendo wa kweli ni mwema,upendo wa kweli hauna husuda,Upendo wa kweli hauwazii mambo yako mwenyewe bali na ya wengine,upendo wa kweli hauna hasira, hauhesabu mabaya,upendo wa kweli haujifichi,upendo wa kweli ni kuaminiana kwa kila jambo,Upendo wa kweli humwamini ampendae,upendo ni kuvumilia yote,upendo hauna kisasi na husamehe yote. Upendo ni kitendo cha kufikirika ambacho huonyeshwa na mtu kwa matendo mema anayoyafanya juu ya mtu /kitu.

Zijue sifa kuu tatu za upendo wa kweli,Mambo yanayojenga upendo wa kweli na Mambo yanayojenga Upendo wa Mwili,Usikose mfululizo wa Makala haya hapahapa kwenye blog yako ya patamambo katika mfululizo tembembelea mara kwa mara gonga Like na toa maoni yako ili niweze kuboresha zaidi.

Jumapili, 17 Aprili 2016

TUNDAMANI APATA AJALI YA GARI

Msanii wa bongo fleva tundamani amepata ajali mkoani Iringa iliyohusiha gari binafsi na roli. Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man amesema ‘Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki‘ Tunda Man anamalizia kwa kusema ‘Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo.

Jumamosi, 16 Aprili 2016

VIKUKU NI UREMBO UNAOPOTEA KILA KUKICHA

Asili ya urembo huu ni huko nchini Uingereza baada ya kugunduliwa miaka ya 80,wanawake walivaa cheni shingoni na shanga kiunoni kama urembo,uvaaji wa cheni ulikua na mambo makuu mawili,uvaaji wa cheni kama urembo na uvaaji wa cheni kama ishara.Mwanamke wa Kiingereza alikuwa akivaa shanga(kikuku)mguuni akimaanisha kuwa yupo singo/mjane.Hapa Tanzania Asili ya urembo huu ni kutoka umasaini,tangu enzi za mababu akina Mama wa Kimasai walikuwa wakifunga shanga miguuni,mikononi na shingoni.Katika miaka ya karibuni Kikuku kimekuwa kikivaliwa na akinadada wengi hata wasio wamasai kwa ajili ya urembo katika miiliyao,urembo huu wa vikuku umekuwa gumzo kwa vijana wengi wa kitanzania kwani wamekuwa wakiwahisia wavaaji kuwa ni makahaba,waendao kinyume na maumbile nk.Kutokana na hali hii uvaaji wa vikuku umekuwa ukififia kutokana na hisia hizo ambazo hazina mashiko wala ukweli wowote.Asanteni xna

EDEN HAZARD ATARUDISHA HESHIMA YAKE LEO?

Guus Hiddink amesema hajawahi kuona mchezaji aliyeanhelseaguka vibaya kiwango kama Eden Hazard midfielder wa chelsea, amemtaka nyota huyo kuamka katika mechi ya leo kati ya
Chelsea dhidi ya Man City!

KANDANDA LA KUNOGA KATI YA

Chelsea V Mancity! Nani atakuwa mshindi leo, Costa au Aguero?