Jumamosi, 16 Aprili 2016
VIKUKU NI UREMBO UNAOPOTEA KILA KUKICHA
Asili ya urembo huu ni huko nchini Uingereza baada ya kugunduliwa miaka ya 80,wanawake walivaa cheni shingoni na shanga kiunoni kama urembo,uvaaji wa cheni ulikua na mambo makuu mawili,uvaaji wa cheni kama urembo na uvaaji wa cheni kama ishara.Mwanamke wa Kiingereza alikuwa akivaa shanga(kikuku)mguuni akimaanisha kuwa yupo singo/mjane.Hapa Tanzania Asili ya urembo huu ni kutoka umasaini,tangu enzi za mababu akina Mama wa Kimasai walikuwa wakifunga shanga miguuni,mikononi na shingoni.Katika miaka ya karibuni Kikuku kimekuwa kikivaliwa na akinadada wengi hata wasio wamasai kwa ajili ya urembo katika miiliyao,urembo huu wa vikuku umekuwa gumzo kwa vijana wengi wa kitanzania kwani wamekuwa wakiwahisia wavaaji kuwa ni makahaba,waendao kinyume na maumbile nk.Kutokana na hali hii uvaaji wa vikuku umekuwa ukififia kutokana na hisia hizo ambazo hazina mashiko wala ukweli wowote.Asanteni xna
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni