- Hauangalii hali ya mtu ya nje.
- Hauna masharti yoyote ya kupenda.
- Hauna kipimo au kiwango cha kupenda.
- Hauna mwisho au kikomo cha kupenda.
NB.Aina hizi za upendo zinatumika katika maisha ya mwanadamu kila siku,mfano upendo wa kimahaba Ero’s ni upendo ambao ni muhimu katika ndoa,shauku yenye kina kirefu na urafiki Phileo huimarika kati ya wanandani na huimarishwa na upendo Agape ambao hustawisha na kuimarisha mahusiano mema kati ya wanadamu.
UPENDO WA KWELI HUJENGWA NA MAMBO YAFUATAYO.
- Una nguvu ya kuwa na shauku ya ashki
- Upendo hutaka kutoa
- Lengo kuu ni kumtii Mungu
- Hujinyima ili kuwatanguliza wengine
- Upo tayari kungoje wakati wa Mungu atakaporuhusu
- Kusubili wakati
- Uko tayari kuchukua majukumu yanayoendana na ashki ya kumpenda yeye,pamoja na watoto wake,familia yake kwa maisha yote.Upendo ni maisha ambayo yako tayari kujitoa kwa kila hali.
- Kutafuta furaha na wema kwa mtu ambaye anapendwa.
- Upendo hautaki na hautaleta aibu kwa yule ambaye anapendwa.
- Upendo ni baraka kutoka kwa Mungu.
- Upendo unadumu maisha yote.
UPENDO NA TAMAA YA MWILI
- Ina nguvu ya kuwa na ashki
- Hutaka kupokea tu
- Kutaka kumuasi Mungu
- Hujinufaisha kutaka kuwatangulioza
- Haungojei wakati wa Mungu
- Hauko tayari kuchukua majukumu ambayo yanaendana na ashki.
- Hutafuta kujifurahisha
- Hajali kama italeta aibu kwa mtu mwingine
- Ni laana mbaya ya dhambi
- Hutoweka baada ya jambo kutokea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni