U hali gani mpendwa msomaji wa patamambo karibu katika makala haya,kwa upande wangu mimi ni mzima wa afya njema,namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuamka salama na mwenye afya bora kabisa. Kilichonishawishi zaidi mpaka kuandika makala haya ni mahusiano feki ambayo yanaanzishwa na vijana baada ya kuona maono feki yanayosukumwa na tamaa za mwili.
UPENDO WA KWELI
Upendo ni hali ya kuvutiwa au kuingiwa moyoni na mtu au kitu,mtu hutamani kupendwa anapozaliwa hadi kufa,mtu huishi kwa furaha anapopendwa na hata hudhoofika na kufa asipopendwa.
Tangu dunia kuumbwa hakuna aliyeweza kutoa maana halisi ya neno upendo,hii ni kwa sababu upendo ni hisia ambayo iko ndani ya moyo wa mtu hivyo ni vigumu kuelezea jinsi anavyompenda mtu fulani.
Bwana Haleni Limbark ni mtaalamu wa saikolojia na mapenzi anaelezea upendo kuwa ni pale mtu anapomjali mwenzake na kusimama kwa ulinganifu katika jambo lolote linalohitaji uaminifu. Upendo una heshima, hukufanya kumsaidia mtu katika hali zote za maisha yake, kumhifadhi kutoka kwa maadui, na kujua kuwa akili ya kila moja kati ya wapendanao ipo hapo kwa asilimia mia moja, kujisikia salama kwake, kujivuna unapokuwa naye, kushirikishana katika matarajio na ndoto za kila mmoja na mambo yote mazuri.
Upendo wa kweli ni upi huo? Upendo wa kweli hauchoshi, upendo wa kweli ni mwema,upendo wa kweli hauna husuda,Upendo wa kweli hauwazii mambo yako mwenyewe bali na ya wengine,upendo wa kweli hauna hasira, hauhesabu mabaya,upendo wa kweli haujifichi,upendo wa kweli ni kuaminiana kwa kila jambo,Upendo wa kweli humwamini ampendae,upendo ni kuvumilia yote,upendo hauna kisasi na husamehe yote. Upendo ni kitendo cha kufikirika ambacho huonyeshwa na mtu kwa matendo mema anayoyafanya juu ya mtu /kitu.
Zijue sifa kuu tatu za upendo wa kweli,Mambo yanayojenga upendo wa kweli na Mambo yanayojenga Upendo wa Mwili,Usikose mfululizo wa Makala haya hapahapa kwenye blog yako ya patamambo katika mfululizo tembembelea mara kwa mara gonga Like na toa maoni yako ili niweze kuboresha zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni