Jumanne, 12 Aprili 2016

KUKATA TAMAA NI DHAMBI

Katika shughulli zetu za kila siku tumekuwa tukikumbwa na majaribu mbalimbali,majaribu haya yanaweza kuwa ya nadhalia ama vitendo,watu wengi wanashindwa kugundua siri ya kushinda majaribu ambayo ni uvumilivu. Uvumilivu ni hali ya kustahimili machungu(Maana hii kutokana na kamusi ya Kiswahili sanifu) Lakini tunaweza kusema uvumilivu ni hali ya kuhimili matatizo mbalimbali yanayotukumba katika maisha yetu ya kila siku. Tumekuwa tukikumbwa na kila aina ya matatizo,majaribu na uonevu ambao unapelekea kukata tamaa ama kuamua kufanya jambo ambalo litamuacha mdomo wazi yule aliyekuwa akikuamini,kukuwazia mazuri na aliyekuwa akitegemea msaada wa mawazo ama kifedha. Majaribu haya yamekuwa yakipelekea baadhi yetu kufanya maamuzi magumu ya kujinyonga,kumeza dawa,kutumia madawa ya kulevya ama kupigana,wengine tumekua tukijiapiza kuwa hatutaweza tena kurudia kazi,biashara ama mahusiano ambayo yameleta mpasuko katika moyo wako. Nimekuwa nikisikia kauli nyingi zenye sauti ya kukata tamaa na zilizokuwa na miungurumo ya kukosa uvumilivu huku zikinakshiwa na maamuzi ya kutisha,utasikia ‘Sitafanyi tena kazi hii’ ‘Sitaki kuolewa tena’ ‘Sitarudi tena’Sauti hizi za kukata tamaa na kukosa uvumilivu zilizo na ngurumo ya kukosa neno la Mungu zimekuwa zikitamkwa na watu mbalimbali ambao wamejeruhiwa mioyo yao. Tumesahau kuwa yupo aliyetuumba na anatuangalia katika kauli zetu za kukata tamaa huku tukisahau kumwita Mungu katika shida zetu.Tumekuwa tukilaumu kwa sauti zilizokosa uvumilivu na zilizokata tamaa. Hata tukirejea katika vitabu vya Mungu,mtume Paulo aliweza kuvumilia katika hali ya dhiki,njaa,kupungukiwa na kushiba pia,si huyu tu bali Mungu aliweza kumfanya Ayubu kuwa maskini wa kutupwa wakati alikuwa ni tajiri lakini kwa yote hayo Ayubu alivumilia. Hata wewe pia uliyekata tamaa ya kufanya biashara,kusoma,kufanya kazi kutafuta mchumba eti kwa sababu umeshindwa kufanikiwa katika malengo yako kwa kusikia sauti za “Nimeshindwa mimi sijui kama utaweza”ama utasikia “Kazi hiyo ni ngumu inawafaa akina Fulani”Chukua hatua sasa achana na dhana ya umaskini wa mawazo na ukosefu wa uvumilivu kwa kile unachokifanya,songa mbele huku ikiimba wimbo wa ushindi kwa kila jambo. Uvumilivu ndio unapelekea mtu kufanikiwa kwa kila anachokifanya na kuwa na maisha mazuri katika siku zake za kuishi hapa duniani.Asanteni kwa muda wenu Tuonane katika makal ijayo

Maoni 1 :