Jumanne, 12 Aprili 2016
HUYU NDIE EDWARD MORINGE SOKOINE
Edward Moringe sokoine alizaliwa 1Augost 1938 katika miji ya Monduli Arusha Tanzania.Alisoma elimu ya msingi Monduli na shule ya sekondari Umbwe katika miaka ya 1948 - 1958.Mwaka 1961 alijiunga na chama cha
siasa cha TANU,Alifanikiwa kwenda kuchukua masomo ya uongozi nchini Ujerumani ilikuwa 1962 -1963 baadae alikaa kama afisa mtendaji wa wilaya ya Masai na kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo hilo.1967 alichaguliwa na Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa naibu waziri wa mawasiliano usafiri na kazi 1972 alihamishwa na kuwa waziri wa usalama.1977 alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM mnamo 1977 alichaguliwa kuwa waziri mkuu kisha mwaka 1982 alipumzika katika nafasi hiyo na mwaka 1983 alirudi ofsini kwake akiwa na nembo ya Uwaziri mkuu Mpaka alipofariki 12April 1983,"NDUGU wananchi, leo saa saba mchana; ndugu yetu na kijana wetu. Ndugu Edward Moringe Sokoine; alipokuwa safarini kutoka Dodoma kuja Dar es Salaam, gari yake ilipata ajali. Amefariki dunia.’ mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina"Ilikuwa ni hotuba fupi ya mwalimu JK iliyoacha vilio na simanzi kwa watnzania.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni