Ijumaa, 27 Januari 2017
HAYA NDIO MAAJABU YA CHUNGWA
Chungwa ni tunda linalostawi ulimwenguni kote , lakini haswa tunda hili lilianza kusini mwa bara la Asia, huku likilimwa sana huko nchini China.
Chungwa lina kiwango cha juu cha vitamin C, huku nyama /ngozi nyeupe iliyozunguka kati ya ngozi ya nje na tunda lililomenywa ni chanzo kizuri cha madini ya ‘calcium.’
Mtaalam wa tiba asili kutoka Mandai Herbalist Clinic, Dk Abdallah Mandai anasema kuwa kwa wale wanaosumbuliwa na mafua wanaweza kuongeza maji ya moto katika juisi ya chungwa kisha mhusika anywe.
Mtaalam huyo, anaeleza kuwa majani ya mchungwa yakipondwa na kisha kuchanganywa na maji ya moto pamoja na asali kidogo, kwa ujumla mchanganyiko huo hutumika kama dawa ya kikohozi.
Aidha, Dk Mandai anafafanua kuwa endapo maua makavu yakisagwa nakuchanganywa katika maji ya moto ni dawa ya shinikizo la mishipa ya fahamu. Huku maganda yake yakisuguliwa usoni huwa ni dawa ya chunusi.
Pamoja na hayo, Dk Mandai anabainisha kuwa kwa ujumla juisi ya machungwa husaidia ugonjwa wa pumu, matatizo ya kifua, kusafisha damu, kupooza, kuungua, matatizo ya meno pamoja na beriberi.
.
Mbali na magonjwa hayo, pia husaidia matatizo ya kizazi, mishipa ya damu, magonjwa ya ngozi, matatizo ya mirija ya uzazi, husaidia usagaji wa chakula mwulini pamoja na kutuliza kichefuchefu kwa wajawazito.
Hizo ndizo baadhi ya dondoo muhumu za faida za machungwa kwa afya
TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU UPATE MAMBO MENGI YANAYOHUSU AFYA NA UREMBO
Alhamisi, 26 Januari 2017
UKISTAAJABU YA MAFUTA YA NAZI UTAYAONA YA TUI LA NAZI
1. Mafuta ya nazi kwa afya ya MoyoMafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.
2. Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakulaHii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida. Anasema Geeta Sidhu Robb, mtaalamu wa lishe na mwanzilishi wa Nosh Detox.
3. Mafuta ya nazi hung’arisha ngoziSiyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha. Pia unaruhusiwa kuyatumia mafuta haya wakati wa masaji.
4. Huongeza nguvu mwiliniMafuta ya nazi ni chanzo kizuri cha nguvu ya mwili kwani yana sifa ya kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu ‘medium chain triglycerides – MCT’ ambapo sifa hii huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa ‘ketones’ ambacho ni chakula cha ubongo. Kwahiyo ikiwa unatafuta lift ya kuinua nguvu yako basi chukua kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi weka kwenye kikombe chako cha juisi au uji na utaona maajabu.
5. Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afyaTofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya. Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!
6. Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyamaSiyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama mubadala kwa siagi au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula. Hii nikwa sababu mafuta ya nazi hubaki kuwa magumu hata katika joto la kawaida la chumba tofauti na mafuta mengine.
7. Huzuia maradhi mengi hatari mwiliniKama ilivyo katika kuipunguza kolesteroli, mafuta ya nazi yanao uwezo mkubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa mengine sababu ya kuwa na kiasi kingi cha asidi iitwayo lauric acid.Utafiti mwingi umeendelea kuthibitisha kuwa hii lauric asidi hubadilishwa kuwa asidi mafuta nyingine ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘monolaurin’ ambayo inayo sifa ya kudhibit na kuvizuia baadhi ya virusi ikiwemo vile vya ukimwi kuziingia na kuzidhuru seli za mwili na kusababisha maradhi mwilini. Ili kutibu virusi vya ukimwi inashauriwa kunywa glasi 4 za tui la nazi kila siku kwa muda wa miezi mitatu mpaka minne na utaona maajabu.
8. Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbuHii inaweza ikakushangaza kidogo unapoisikia kwa mara ya kwanza lakini tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo kuziamusha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo kutasaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
9. Hutumika kulainisha uke mkavuMafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu, kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake tena bila madhara yeyote hasi.
10. Husaidia katika ugonjwa wa alejiTukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza, moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.MHIMU:Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani ile ya asili. Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima utajing’ata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.
Ijumaa, 28 Oktoba 2016
MWANAUME MWENYE MALENGO NA WEWE UTAMTAMBUA KWA HAYA
Nimekuwekea hapa zisome Tabia za mwanaume mwenye malengo na wewe.
1. Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli.
2. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu.
3. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume!
4. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu!
5. Hakulazimishi kufanya mapenzi. Anakupenda sana kiasi kwamba hawezi kukulazimisha jambo ambalo hauko na hiari nalo. Yupo karibu na wewe wakati wote na sio tu anapokutaka kimapenzi, huyu ni bonge la bwana.
6. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda!
7. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati kutoka moyoni mwake ya kukufanya uwe mkewe.
Hizi ni moja ya dalili kwamba mwanaume wako anakupenda na anataka atengeneze future pamoja na wewe. Usikate tamaa juu ya mwanaume wa aina hii.
Hao wenye sixpack sijui eight pack, wabeba vyuma, wavaa milegezo, wanyonya midomo na mahandsome wavaa hereni, waume za watu, masupa staa, watoto wa vigogo, hawatakusaidia lolote, utabaki ukiumizwa tu moyo wako.
Kabla hujajipendekeza kwa wanaume wa aina hiyo, jiulize wanawake wanzako wangapi wameshajipendekeza kwa sababu ya hzo pesa zake, hivyo na wewe unajiongeza kwenye foleni!
Mvumilie mwanaume wako, anazo ndoto njema, mapenzi ya kweli ni vigumu sana kuyapata. Ila pesa na mali ni rahisi sana kuzipata kama utajibidiisha.
Usipende mitelemko, mitelemko mingine ni njia ziletazo mauti! - Ukishikwa shikamana, ukipendwa, pendeka!
"Don't date a rich man, date a GOOD MAN, Good man will spend his life trying to keep u happy, no rich man can buy that!"
TANESCO YAIDAI SERIKALI MABILIONI
Na SARAH MOSES, DODOMA
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limeiambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kwamba linaidai Serikali zaidi ya Sh bilioni 125 kutokana na huduma za umeme linazotoa katika taasisi za umma pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).
Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba, wakati akijibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo waliotaka kujua juu ya ripoti ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inayoishia Juni 2015 kuhusu hesabu za shirika hilo.
Akiendelea kufafanua kuhusu hoja hiyo ya madeni, Mramba alisema tayari shirika hilo limeanza kufanya mikutano kadhaa na ZECO kwa ajili ya kuweka mikakati itakayofanikisha deni hilo la tangu mwaka 2013, kulipwa.
“Katika mikutano ile, tulibaini kuwa ZECO inashindwa kulipa kwa sababu inatoza gharama ndogo kwa watumiaji wa umeme Zanzibar tofauti na gharama za ununuaji umeme kutoka Tanesco,”alisema Mramba.
Kuhusu mikakati iliyoanza kuchukuliwa na shirika hilo ili kukabiliana na hali hiyo, Mramba alisema kwa sasa wameanza kuondoa mita zote za kawaida na kuweka mita za LUKU.
“Katika hilo, hadi sasa tumefanikiwa kuondoa mita za kawaida kwa takribani asilimia 99 kwa wateja wa kawaida ikiwa ni pamoja na kufungia taasisi kubwa za Serikali kama vile polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Magereza.
“Hili la Luku, tunatarajia hadi Aprili mwakani, tutakuwa tumelikamilisha kwa taasisi zote za Serikali,” alisema Mramba.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Naghejwa Kaboyoka, aliiagiza Serikali ihakikishe inalipa madeni hayo ndani ya miezi sita.
“Ni wakati sasa shirika hilo liachwe lijiendeshe lenyewe kibiashara kwani kwa hali ya sasa ilivyo, haileti maana mwananchi wa kawaida abanwe ili alipie bili yake ya umeme, wakati taasisi kubwa za Serikali zikiachwa na mlundikano wa madeni wa bili hizo za umeme,”alisema Kaboyoka.
Source: Mtanzania
Alhamisi, 27 Oktoba 2016
TAJIRIKA:NA UFUGAJI WA KUKU
Hebu anza na kuku Watano (5) tu Majike wenye Rika/Umri mmoja (au wanaokaribiana).
Watunze vizuri kwa kuwapatia chakula kilicho na mchanganyiko kamili wa viini lishe
vinavyotakiwa katika mwili wa kuku,
yaani;
wanga, protini, calcium, chumvichumvi, madini joto nk (kama nilivyoeleza hapa chini). Wawekee na Jogoo mmoja mzuri wa kienyeji/ kizungu/chotara (kama nilivyoeleza hapa chini juu ya uchaguzi wa majogoo).
Wanapoanza kutaga watayarishie mahali pazuri/Kiota kizuri cha kutagia na kuatamia kwa kuwajengea viota ndani ya banda.
Hakikisha mahali hapo hapavuji wala hapapati unyevunyevu wala joto kali sana. Hakikisha mahali hapo pana usalama wa kutosha (mahali wanyama hatari kama vicheche, pakashume, nyoka nk hawawezi kufika).
Kuku wakiendelea kutaga na sasa ukaona wanakaribia kuatamia,Anza kuchagua aina ya mayai unayotaka kuku wako walalie. Hii inamaanisha kuwa; ukichagua mayai makubwamakubwa hayo yanakuwa na vifaranga majogoo na mayai madogomadogo mara nyingi huwa ni ya vifaranga majike.
Acha kuwawekea mayai ya mviringo kama mpira!
Hakikisha kuku wote wanasubiriana ili walalie/ waatamie kwa pamoja.
Weka mayai 12 hadi 15 kwa kila kiota cha kuku 1 kulingana na umbo la kuku wako.
Kuku anaweza kutaga hadi mayai 30 kwa kila msimu wa kutaga unapofika. Unaweza kutumia mayai machache kati ya 30 kwa kumuatamishia kuku wako huku mayai mengine yakisubiri awamu ya pili ya kuatamiwa.Kwa mfano ukiwawekea kuku wako hao watano, Kuku 5 x Mayai 12 =Mayai 60.
Kwa kawaida kuku huatamia/hulalia mayai kwa siku 19 hadi 21/24 tu hadi anapototoa vifaranga. Hakikisha unawawekea kuku walioatamia chakula chenye viini lishe vya kutosha na maji mengi karibu na viota vyao ili wakitoka kwenye viota vyao wale chakula mara moja na kunywa maji kisha warudi haraka kwenye mayai yao. Hii itasaidia kuangua mayai yote 12/15 bila kuharibu yai hata moja.
Au hata yakiharikbika basi hayataharibika mengi kama ukiacha kuwawekea chakula waende kufukuzana na panzi na vyakula majalalani huko nje na kuchelewa kurudi kwenye mayai yao.
Wakati ukisubiria siku hizo 21/24 anza kujenga kibanda kidogo ndani ya banda kubwa ulilojenga awali au jikoni au andaa boksi kubwa na gumu kwaajili ya kutunzia vifaranga watakaoanguliwa ndani ya siku 21/24 zijazo.
Baada ya kuku hao 5 kuangua vifaranga wako 60 hapo ndipo kazi kubwa ya kulea vifaranga inapoanza. Elewa kuwa ili upate mafanikio haraka hakikisha kuwa kazi ya kulea vifaranga inakuwa yako na siyo ya kuku! Kwanza, Unatakiwa kuondoa na kuchoma moto/kufukia mabaki yote ya mayai na kuboresha usafi wa banda lote ili kuepusha magonjwa kama vile kuharisha, viroboto, papasi nk.
Hapo unaweza kuwatoa vifaranga wako wote 60 mmojammoja kadri wanavyoanguliwa hadi kufikia kifaranga wa mwisho, yaani Yule wa 60 na kuwaweka katika kibanda kidogo/boksi ulichokijenga na kuwawekea mayai mengine mama zao (yale 15/18 kati ya 30 uliyoyabakiza) ili waatamie tena kwa siku 21 hadi 24 zingine.
Unapotoa kifaranga kutoka kwa kuku aliyeatamia humfanya kuku Yule ashindwe kutoka kwenye mayai maana hana mtoto wa kulea.
Akimaliza kuangua mayai yote na ukamuwekea mengine ni rahisi kwake kuendelea kuatamia maana atasubiri kupata vifaranga na ndipo atajikuta amelalia kwa siku 21 zingine bila wasiwasi.
Kwa kufanya hivyo utakuwa tayari umejipatia vifaranga/kuku zaidi ya 100 ndani ya wiki 7 tu! Sasa Unatakiwa kuwajali sana kuku hawa wanaolalia kwa mara ya pili kwa kuwapa chakula cha kutosha, maji, majani ya makongwe, mchicha, mchunga nk ili wapate vitamini na madini mengine muhimu kwa afya zao.
Fanya hivyo hata watakapokuwa wametotoa na ukawanyang’anya vifaranga. Hii itawasaidia ili wasinyonyoke sana manyoya maana kuku wengi hunyonyoka manyoya wanapoatamia. Kwa kufanya hivi, kuku wako watakaa kwa wiki 2 hadi 3 bila vifaranga na kisha wataanza kutaga tena na kuatamia kama mwanzo.
NAMNA YA KULEA VIFARANGA.
Katika ulezi wa vifaranga kama kuku utawanyang’anya vifaranga vyao utatakiwa kuwajengea banda dogo (ndani ya banda kubwa/uzio) ili uwawekee chanzo cha joto kama taa/jiko la mkaa (kama ni sehemu/ majira ya baridi).
Kama utatumia jiko la mkaa unatakiwa kuacha kwanza hadi mkaa mweusi uwake wote ndipo uweke bandani maana mkaa ukitoa moshi unaweza kuathiri vifaranga vyako.
Angalia namna ya kuweka jiko lako la mkaa juu kidogo ili vifaranga wasiungue. Hakikisha taa yako haitoi moshi sana na haivujishi mafuta. Pia uwe na akiba ya mafuta ya taa ya kutosha.
Usiweke mafuta mengi kwenye taa maana inaweza kulipuka ikakuletea hasara. Vifaranga wasizidi 50 kwa boksi 1. Hakikisha umewasha taa/jiko lako ndani ya boksi saa tatu au zaidi kabla ya kuwaweka vifaranga ili chumba/boksi lipate joto kabla ya vifaranga kuwasili.
Njia hizi zinahitaji uangalifu wa hali ya juu sana kwani kuhatarisha/kuua vifaranga ni kuhatarisha maendeleo yako. Kama utaamua kutumia umeme pia ni vizuri zaidi maana inapunguza hatari zaidi.
Kwa hiyoa njia zote tatu unaweza kutumia jedwali lifuatalo ili kuweza kumeneji joto la kibanda cha vifaranga;
UMRI WA KUKU/VIFARANGA JOTO NDANI YA BOX/KIBANDA CHA KULELEA VIFARANGA JOTO NDANI YA CHUMBA/BANDA
Wiki 1 33-35oc 30-32oc
Wiki 2 30-33oc 27-29oc
Wiki 3 27-31c 24-26oc
Wiki 4 24-29oc 21-23oc
Wiki 5 26-27oc 22-23oc
Baada ya wiki ya 4/5 pasua box/watoe kwenye banda la kulelea ili walelewe kwa joto la kawaida la banda/chumba.
Kwa kawaida joto hupimwa kwa kipimajoto (thermometer), lakini kama huna kipimo hiki, njia rahisi ni kuwaangalia kulingana na tabia zifuatazo;
Kama vifaranga wamejikusanya sehemu moja basi joto ni kidogo bandani mwao, au kama wanaenda mbali na chanzo cha joto huku wanatanua mabawa yao na wakihema harakaharaka basi joto ni kali/ limezidi kiwango.
Pale watakapo tawanyika vizuri ndani ya boksi/kibanda cha kulelea huku wanakula na kunywa maji vizuri basi joto ni la wasta na ndilo linalofaa. Kama unatumia njia ya Boksi, basi unatikiwa kulipanua kulingana na ukuaji na mahitaji ya vifaranga vyako.
Vifaranga wako wape chakula cha vifaranga cha kutosha, maji safi na salama, majani mabichi ambayo hufungwa kwa kuning’inizwa kwa kamba,na CHANJO za minyoo nk ili wapate vitamin, madini na protini itakiwayo na kuzuia tabia ya kudonoana ili wakue vizuri.
Hakikisha kuwa chumba chao ni kisafi na hakina unyevunyevu wakati wote. Unyevunyevu husababisha ugonjwa wa baridi na hufanya vifaranga wajikunyate na kutetemeka na wanaweza kufa ghafla! Inashauriwa kuwa siyo salama kufuga aina nyingine ya ndege kama vile njiwa, bata, bata
mzinga nk kwa kuwachanganya na kuku maana kila aina ya ndege wanamagonjwa yao.
Hivyo kuwachanganya kutakufanya ushindwe namna ya kuwatibu wanapopatwa na ugonjwa.
Pia chawa wa njiwa huleta ugonjwa wa Ndui hasa kuku wanapoangua vifaranga wao.
Hapa ugonjwa unaweza kufyeka vifaranga wako wote 60/100 kama utafuata ushauri wangu!
Baada ya wiki 2 hadi 3 baada ya kuwanyang’anya vifaranga kuku wako wataanza tena kutaga mayai. Wakiatamia wote 5 Kama utaimarisha huduma kwao na kwa vifaranga/kuku wale 100 tayari utakuwa una kuku 105 au zaidi.
Kuku wale 5 wa mwanzo wakiatamia tena kwa siku 21 hadi 48 (kama utafuata mfumo ule wa mwanzo wa kuaatamishia mara 2) utajipatia vifaranga wengine 100 tena na hivyo kuwa na kuku zaidi ya 200 ndani ya miezi 5/6 tu!
Ukiwahudumia vifaranga wale wa mwanzo 100 vizuri kwa miezi 3 na nusu nao wataanza kutaga kama mama zao. kwahiyo, Chukulia walalie majike 5 wa mwanzo na majike 50 waliopatikana baada ya uzao wa kwanza kwa miezi ile 3 ya mwanzo utakuwa na mitetea 55.
Wote wakiatamia na watoe vifaranga 10 kila mmoja kwa siku zilezile 21 hadi 46, tayari utakuwa na vifaranga 550!
Sasa jumlisha na wale 150 waliobakia kati ya kuku 200 na wote wakakua vizuri utapata kuku na vifaranga zaidi ya 700! Jumlisha na 550 watakaototolewa na mama zao wale 5 wa kwanza na wale 50 wa uzao wa 1 na 2 kwa mara ya 2 si tayari utakuwa na kuku zaidi ya 1,200 ndani ya miezi 6 hadi 8 tu? Hivyo utajikuta unao kuku zaidi ya 1,000!
Kati ya kuku 1,000 ukisema utoe kuku 800 wa kuuza na ukiwauza kwa bei ya Tsh. 4,000 kwa kila kuku 1 tayari utakuwa na Jumla ya Tsh. 320,000/= ambazo unaweza kufanya mtaji wa mambo mengine au kuboresha mradi wako zaidi. Unafikiri hapo hujaanza kufikia lengo la kuku 1 akuletee shilingi Milioni 1?
Ukiendelea hivi inamaana kuku 1 atakuzalishia zaidi ya hapo.
BANDA LA KUKU.
Unatakiwa kuwa na banda bora la kufugia kuku ambalo litaweza kutunza kuku ili wasiweze kupatwa na madhara mbalimbali kama vile; kuliwa/kujeruhiwa na wanyama wakali, kuchukuliwa na wezi nk.
Lakini banda bora pia litawasaidia kuku kuhimili mabadiliko mbalimbali ya hali ya hewa yanayoweza kujitokeza.
Sehemu ambayo inafaa kwa ujenzi wa banda bora ni ile ambayo inaweza kufikika kwa urahisi, iwe na mwanga wa kutosha, isiwe na upepo mkali na isiyoruhusu maji kusimama au kuingia ndani.
Banda ni vema likawa la ukuta/mbao/ mabanzi.matete/mianzi imara ili lishikilie paa vizuri lisianguke. Kuta hizi zaweza kujengwa kwa matofali ya saruji/matope/kuchomwa/ mabanzi/mbao nk.
Katika kuezeka waweza kutumia mabati/vigae/nyasi. Banda ni vema likawa kubwa kulingana na kiasi cha kuku na umri walionao.
Kitu cha kuzingatia ni kwamba banda liwe na hewa ya kutosha. Kuku wanaofugwa ndani ni vema
wakatengenezewa uzio mpana (angalau Mita 8x10) ili wapate mahali wanapoweza kuota jua,
kupumzikia/kupunga hewa na kufanya mazoezi (wawekee kamba/bembea/ngazi ndani ya banda).
Hakikisha kuwa banda ni imara na hawatoki nje ya banda na kwenda mbali ili uweze kuwawekea chakula cha kutosha na maji na hata wale wanaotaga/kuatamia wapate chakula na kurudi haraka.
Banda likiwa kubwa na bora litapunguza magonjwa kwani litakuwa na hewa ya kutosh ambayo itasaidia kupunguza joto na unyevunyevu usio wa lazima bandani mwako. Hii itasaidia uingizaji oksijeni ya kutosha na kupunguza hewa chafu zenye madhara kwa kuku.
Pia litasaidia namna ya kufanya usafi kwa urahisi na kupunguza vumbi ambalo linaweza kusababisha kikohozi kwa kuku wako. Ni vema banda lisipungue Mita 3 kwenda juu. Mambo muhimu ndani ya Banda.
1. Sakafu nzuri (iliyotengenezwa kwa saruji/ udongo ili isituamishe maji. Isiwe na nyufa ili iweze kusafishwa kwa urahisi.
2. Hakikisha kuwa banda linakuwa na Viota (vitagio) vizuri kwaajili ya kutagia. Viota viwe na urefu wa Sentimita 30 na upana sentimita 30 na kina sentimita 35. Sehemuya mbele izibwe kwa sentimita 10 tu chini. Sehemu zote hizo zizibwe kwa ubao. Kama kuku wako ni wakubwa unaweza kuongeza upana, urefu na kina kiasi cha kutosha mfano, Upana na Urefu 35cm, kina 55cm nk.
Hakikisha kiota/kitagio kinakuwa na giza kiasi maana kuku hupenda kutaga mahala pa giza kidogo/palipojificha. Giza litasaidia kuku asiweze kula mayai au asiweze kudonoana na kuku wengine. Kiota pia kinatakiwa kiwe mahali ambapo ni rahisi kwa kuku kuingia na kutoka, pia iwe ni rahisi kusafisa.
Ndani ya kiota kuwekwe majani makavu/ maranda ya mbao laini na kinyunyize dawa ya unga ya kuzuia viroboto/utitiri kabla ya kuweka nyasi.
AIDHA, ni vizuri sana kuwawekea kuku wanaoatamia mayai wakati wa usiku maana ukimuwekea wakati wa mchana anaweza kuyaacha.
Kuku anayetarajiwa kuatamia ni vema akachunguzwa kama anao utitiri/viroboto/ chawa kwenye manyoya yake. Wadudu hawa humkosesha raha kuku anayeatamia na wengi huacha mayai na kukimbia/wasitulie kwenye viota vyao.
Hali inapelekea kuanguliwa kwa vifaranga wachache. Unaweza kumuona mtaalam wa mifugo kwa ushauri zaidi.
1. Banda liwe na vichanja maana kuku hupenda kulala juu ya vichanja maana nao ni ndege.
2. Vyombo safi na vizuri kwaajili ya chakula na maji.
3. Walazie majani makavu/maranda ya mbao/ makapi ya mazao sakafuni kwa banda zima.
HII NDIO SIRINYA MKOPO
Nichukue fursa hii adhimu, kwa kukupogeza sana wewe kwa kuendelea kusoma makala mbalimbali kupitia mtandao huu, kwani ni imani yangu kubwa sana, kama kweli yale ambayo unayojifunza kupitia mtandao huu na kuyaweka katika matendo basi maisha yako yatakuwa yamebadilika sana kwa kiwango kikubwa sana. Hivyo nikusihi ya kwamba uendelee kujifunza kwa kusoma kila mara kwa mara kupitia mtandao huu wa dira ya mafanikio, pia usisite kumshirikisha mwingine.
Basi nadhani nisizungumze sana niende moja kwa moja katika somo ambalo nmelikusudia, najua fika wapo baadhi ya watu kwao mikopo ni rafiki , wapo pia baadhi ya watu ambao mikopo kwao imekuwa ni adui mkubwa sana, hii ni kutokana na matokeo ya mikopo hiyo.
Pia mikopo hiyo ipo ya aina mbalimbali kwa mfano;
(a) mikopo midogo midogo- hii ni mikopo ambayo hutolewa kwa jamii, kwa ajili ya kuendeleza biashara ndogo ndogo. Lengo la mkopo huu husaidia kuongeza mtaji katika biashara ndogo ndogo ili kuwa biashara kubwa.
(b) Mikopo ya wafanyakazi- hii ni aina ya mikopo ambayo hulipwa wafanyakazi kwa ajili kuendesha maisha yao kiujumla. Na mara nyingi mishahara hili marejesho yake hukatwa kutoka mahali fulani kwenye mshahara wa mkopaji.
(c) Mikopo ya biashara- hii ni aina ya mikopo ambayo mara nyingi humsaidia mtu hasa katika suala la kuongeza mitaji katika biashara kubwa na kuifanya biashara hiyo kukua zaidi.
Hizo ni baadhi za aina ya mikopo ambayo hutolewa kwa wanajamii lakini zipo aina nyingi za mikopo. Lakini katika makala haya naomba nijikite zaidi katika siri ambazo zimejificha katika mikopo ya kibiashara maana huku ndiko ambako watu wengi hasa wafanyabiashara wengi waichukue mikopo hiyo, na watu wachache ndio ambao wana urafiki na mikopo hiyo ya kibiashara. Je nini kinachosababisha hali hiyo?
Zifuatazo ndiyo siri ya mkopo iliyojificha.
1. Usichukue mkopo kama biashara yako haifanyi vizuri.
Watu wengi hususani hawa wanaoichukia mikopo ya kibiashara, wengi wao huchukua mikopo hasa pale ambapo biashara inapokwenda vibaya, lakini kufanya hivi ni kosa kwa sababu wateja wengi huwa wamepotea hivyo ukichukua mkopo itakuwa ni kazi bure kwani wateja watakuwa wachache hivyo suala la marejesho kwako litakuwa ni suala gumu sana, ila ili kuufurahia mkopo wa kibiashara hakikisha unachukua mkopo wakati biashara inakwenda vizuri, kwani kufanya hivi wateja watakuwa wengi pia itakuwa ni rahisi kwako kurejesha marejesho ya mkopo huo.
2. Chukua mkopo kwa lengo ulilokusudia.
Mara zote watu wengi huuchukia mkopo wa kibiashara kwa sababu malengo ya kuchukua mkopo huo hufanya kazi ambazo huzikustaili, kwa mfano utakuta mtu amechukua mkopo kwa kuendeshea biashara lakini cha ajabu pale mtu huyo apewapo mkopo huo utashangaa anafanyia kitu kingine kama vile ulipaji karo, kodi ya nyumba n.k. lakini kufanya hivi ukumbuke ya kwamba ni kupoteza maono sahihi ya kibiashara na mwisho wa siku kupelekea biashara kufa.
Ni vyema ukayazingatia hayo kabla ya kuamua kuchukua mkopo wowote ule. Kufanya hivo kutakusaidia sana kukuza biashara yako.
Jumanne, 27 Septemba 2016
JIFUNZE JINSI YA KUTONGOZA MWANAMKE
Kujifundisha jinsi ya kumuapproach mwanamke kwa mara ya kwanza si jambo gumu la kufanya kama utafuata kanuni na masharti na kuyahifadhi baadhi ya michongo kwa moyo. Michongo ni maneno ya kwanza ambayo mtu hutumia kuanzisha maongezi na mwanamke.
Maneno haya ndio mara nyingi hutumiwa na wanaume mara yao ya kwanza wanapomshobokea mwanamke. Ukiitumia vizuri michongo itakupa wewe nafasi ya kumvutia mwanamke kwa uharaka zaidi.
Ingawa wanaume wengi hutegemea zaidi bahati ama kukosa, hauwezi kamwe kufaulu kumridhisha mwanamke iwapo hujui kuipanga michongo yako vizuri pindi unapokutana na mwanamke unayemzimia kwa mara ya kwanza.
Ok. Kukusaidia kujipanga vyema, tumeweza kuiorodhesha baadhi ya michongo iliyowazi na iliyofunge na jinsi ya kuitumia.
Aina ya michongo -wazi na funge
Unaweza kumuapproach mwanamke bila wasiwasi kwa kutumia michongo aina mbili -wazi na funge. Michongo ile mizuri zaidi inakuwezesha wewe kuonekana kujiamiani, mcheshi na kuonekana mtu anayevutia zaidi kuwaliko wengine walioko karibu nawe.
Ijapokuwa michongo iliyowazi inahitaji mtu mwenye kujiamini kwa kiasi cha juu, michongo funge inaweza kutumika na yeyote yule bora tu ufuate masharti ya kuitumia.
Michongo iliyofunge
Aina hii ya michongo ni rahisi kuitumia kwa mwanamke na si rahisi kwake kuelewa kama unatumia maneno kama hayo ukiwa na ajenda fulani. Michongo hii ni kuanzia matukio, kumsifu ama kuangazia mazingira. Kila aina ya michongo hii ina manufaa yake na pia upungufu wake kiasi fulani kulingana na mazingira ambapo yanatumika. [soma: Hatua za kufanya kama mwanamke anakataa kujibu texts zako]
1. Matukio
Aina hii ya michongo ni rahisi kuikumbuka na ukiitumia kwa mwanamke atakupa atenshen yake automatic. Michongo hii hutumika ili kutaka atenshen ya mwanamke kwa kujaribu kumuuliza maswali ambayo yanalingana na mazingira aliyeko.
Baadhi ya aina ya michongo iliyofunge ni kama:
"Unaweza kujua wakati gani gari lingine la abiria linaweza kufika hapa?"
"Je unajua sehemu nzuri ambayo mtu anaweza kujiinjoy katika huu mji?"
"Nlikuwa nataka kuvuta sigara lakini kibiriti changu sikioni, naweza kuomba chako?"
"Nilikuwa sijamaliza kuandika maswali ya mwalimu kwa ubao, unaweza kunisaidia kitabu chako?"
2. Kumsifu
Aina hii ya michongo inakaribiana na ile ya wazi lakini kwa mpango flani inazuia kumfanya mwanamke kuelewa ajenda yako kwa uharaka. Michongo hii inafaa zaidi wakati ambapo inatumika katika vilabu, sehemu za kujivinjari ama sehemu yeyote ile ambayo unaona inaweza kutumika.
Kabla hujamsifu, ni lazima uhakikishe ni kwanini unamsifu manake mara nyingi unapomsifu mwanamke kuhusu jambo fulani atataka kujua kwa nini unammiminia sifa kama hizo.
Baadhi ya michongo ya kumsifu ni kama vile;
"Dress uliyoivaa imekupendeza, yaani imekufanya kuonekana mfano wa malaika"
"Una pozi lengine ajab, lazima wewe ni dansa flani"
"Nimependezwa na mtindo wako wa nguo na umbo lako, umetoklezea"
Ujanja wa kutumia aina hii ya michongo ni kuhakikisha unacheza na tabia na umbo lake, hakikisha kuwa unajaribu kumchunguza ili kupata mambo ambayo anayapenda kumhusu yeye. Usisahau ya kuwa utafiti umebainisha kuwa wanawake hupenda sana kusikia wakisifiwa.
3. Kuangazia mazingira
Kulingana na mazingira, unahitaji kuifahamu sanaa ya kuingia katika akili ya mwanamke na kufahamu kile ambacho anafikiria. Ukifahamu kile ambacho anafikiria, itakuwa ni jambo jema zaidi.
Kwa mfano, kama mwanamke anajaribu kusoma lakini kila dakika anasumbuliwa na jambo fulani, unaweza kumuuliza: "Si inaonekana ni vigumu zaidi kusoma wakati ambapo jua ni kali zaidi huko nje?"
Kama umekutana na kundi la wanawake na ungetaka kuanza kuongea nao, unaweza kuwaapproach halafu useme "Nyinyi wanawake mnaonekana mnaenjoy sana na wenye nishati, kwani kitu gani kinachoendelea ambacho nakikosa?"
Pia kama kuna mwanamke unayemzimia na hujawahi kuongea na yeye unaweza kumwambia "happy birthday"
Michongo iliyowazi
Kama wewe una confidence na unajiamini kuwa unaweza, basi njia yako ya kutumia ni michongo iliyowazi. Kumbuka kuwa kama wakati wowote utaonyesha unyonge katika sauti yako juwa ya kwamba michongo yako itaanguka hapo hapo na utajiaibisha mwenyewe. [soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke akutamani]
Kutumia michongo iliyowazi itakuwezesha wewe kukupatia matokeo ya haraka kwa sababu ni kuwa wanawake hupenda wanaume ambao wanajiamini kwa mambo wanayoongea na kufanya. Kama mwanamke ataonyesha dalili zozote za kutaka kuongea nawe kwa njia ya miondoko ya mwili, basi unafaa kutumia michongo iliyowazi.
Baadhi ya michongo iliyowazi ni kama vile:
"Unaoneka mrembo, unaweza kuniruhusu nitake kukujua zaidi?"
"Nilikuwa nimekuona kutoka upande ule mwingine wa nyumba na nikaamua kuja kukusalimia, bila hivyo ningeishi kujutia kukosa kumjua mwanamke mrembo zaidi maishani mwangu"
Mwisho ni kuwa hakikisha kuwa baada ya kutumia hii michongo kupata atenshen ya mwanamke, hakikisha unaendeleza maongezi yenu. Jaribu kupata kulijua jina lake halafu ujibidiishe kulitumia kila wakati, lazima atapenda.
Usisahau kutumia sanaa za kutongoza kwa kujua vitu ambavyo mnagawa interest pamoja, jinsi ya kumfurahisha na kadhalika. Hii utamfanya apendezwe na wewe na mudan usiomrefunatakuzoea.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)