Alhamisi, 27 Oktoba 2016

HII NDIO SIRINYA MKOPO




Nichukue fursa hii adhimu, kwa kukupogeza sana wewe kwa kuendelea kusoma makala mbalimbali kupitia mtandao huu, kwani ni imani yangu kubwa sana, kama kweli yale ambayo unayojifunza kupitia mtandao huu na kuyaweka katika matendo basi maisha yako yatakuwa yamebadilika sana kwa kiwango kikubwa sana. Hivyo nikusihi ya kwamba uendelee kujifunza kwa kusoma kila mara kwa mara kupitia mtandao huu wa dira ya mafanikio, pia usisite kumshirikisha mwingine.

Basi nadhani nisizungumze sana  niende moja kwa moja katika somo ambalo nmelikusudia, najua fika wapo baadhi ya watu kwao mikopo ni rafiki , wapo pia baadhi ya watu ambao mikopo kwao imekuwa ni adui mkubwa sana,  hii ni kutokana na matokeo ya mikopo hiyo.

Pia mikopo hiyo ipo ya aina mbalimbali kwa mfano;
(a) mikopo midogo midogo- hii ni mikopo ambayo hutolewa kwa jamii, kwa ajili ya kuendeleza biashara ndogo ndogo. Lengo la mkopo huu husaidia  kuongeza mtaji katika biashara ndogo ndogo ili kuwa biashara kubwa.

(b) Mikopo ya wafanyakazi- hii ni aina ya mikopo ambayo hulipwa wafanyakazi kwa ajili kuendesha maisha yao kiujumla. Na mara nyingi mishahara hili marejesho yake hukatwa kutoka mahali fulani kwenye mshahara wa mkopaji.

(c) Mikopo ya biashara- hii ni aina ya mikopo ambayo mara nyingi humsaidia mtu hasa katika suala la kuongeza mitaji katika biashara kubwa na kuifanya biashara hiyo kukua zaidi.

Hizo ni baadhi za aina ya mikopo ambayo hutolewa kwa wanajamii lakini zipo aina nyingi za mikopo. Lakini katika makala haya naomba nijikite zaidi katika siri ambazo zimejificha katika mikopo ya kibiashara maana huku ndiko ambako watu wengi hasa wafanyabiashara wengi waichukue mikopo hiyo, na watu wachache ndio ambao wana urafiki na mikopo hiyo ya kibiashara. Je nini kinachosababisha hali hiyo?

Zifuatazo ndiyo siri ya mkopo iliyojificha.

1. Usichukue mkopo kama biashara yako haifanyi vizuri.
Watu wengi hususani hawa wanaoichukia mikopo ya kibiashara, wengi wao huchukua mikopo hasa pale ambapo biashara inapokwenda vibaya, lakini kufanya hivi ni kosa kwa sababu wateja wengi huwa wamepotea hivyo ukichukua mkopo itakuwa ni kazi bure kwani wateja watakuwa wachache hivyo suala la marejesho kwako litakuwa ni suala gumu sana, ila ili kuufurahia mkopo wa kibiashara hakikisha unachukua mkopo wakati biashara inakwenda vizuri, kwani kufanya hivi wateja watakuwa wengi pia itakuwa ni rahisi kwako kurejesha marejesho ya mkopo huo.

2. Chukua mkopo kwa lengo ulilokusudia.
Mara zote watu wengi huuchukia mkopo wa kibiashara kwa sababu malengo ya kuchukua mkopo huo hufanya kazi ambazo huzikustaili, kwa mfano utakuta mtu amechukua mkopo kwa kuendeshea biashara lakini cha ajabu pale mtu huyo apewapo mkopo huo utashangaa anafanyia kitu kingine kama vile ulipaji karo, kodi ya nyumba n.k. lakini kufanya hivi ukumbuke ya kwamba ni kupoteza maono sahihi ya kibiashara na mwisho wa siku kupelekea biashara kufa.

Ni vyema ukayazingatia hayo kabla ya kuamua kuchukua mkopo wowote ule. Kufanya hivo kutakusaidia sana kukuza biashara yako.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni