Ijumaa, 27 Januari 2017

HAYA NDIO MAAJABU YA CHUNGWA



Chungwa ni tunda linalostawi ulimwenguni kote , lakini haswa tunda hili lilianza kusini mwa bara la Asia, huku likilimwa sana huko nchini China.


Chungwa lina kiwango cha juu cha vitamin C, huku nyama /ngozi nyeupe iliyozunguka kati ya ngozi ya nje na tunda lililomenywa ni chanzo kizuri cha madini ya ‘calcium.’

Mtaalam wa tiba asili kutoka Mandai Herbalist Clinic, Dk Abdallah Mandai anasema kuwa kwa wale wanaosumbuliwa na mafua wanaweza kuongeza maji ya moto katika juisi ya chungwa kisha mhusika anywe.

Mtaalam huyo, anaeleza kuwa majani ya mchungwa yakipondwa na kisha kuchanganywa na maji ya moto pamoja na asali kidogo, kwa ujumla mchanganyiko huo hutumika kama dawa ya kikohozi.

Aidha, Dk Mandai anafafanua kuwa endapo maua makavu yakisagwa nakuchanganywa katika maji ya moto ni dawa ya shinikizo la mishipa ya fahamu. Huku maganda yake yakisuguliwa usoni huwa ni dawa ya chunusi.

Pamoja na hayo, Dk Mandai anabainisha kuwa kwa ujumla juisi ya machungwa husaidia ugonjwa wa pumu, matatizo ya kifua, kusafisha damu, kupooza, kuungua, matatizo ya meno pamoja na beriberi.



 .
Mbali na magonjwa hayo, pia husaidia matatizo ya kizazi, mishipa ya damu, magonjwa ya ngozi, matatizo ya mirija ya uzazi, husaidia usagaji wa chakula mwulini pamoja na kutuliza kichefuchefu kwa wajawazito.

Hizo ndizo baadhi ya dondoo muhumu za faida za machungwa kwa afya 
TEMBELEA BLOG HII  KILA SIKU UPATE MAMBO MENGI YANAYOHUSU AFYA NA UREMBO

Maoni 1 :