Alhamisi, 14 Julai 2016

LULU ATENGENEZA FILAMU YA KIMATAIFA



Baada ya kimya cha muda mrefu, mshindi wa tuzo za Africa Magic, Elizabeth ‘Lulu’ Michael, anakuja na filamu yake mpya iitwayo ‘Ni Noma.’

Filamu hiyo inaingia sokoni Ijumaa hii kwa mfumo wa dijitali ambapo watu watainunua na kuingalia kwenye smartphone zao kupitia app ya Proin Box.

Lulu ameiambia Bongo5 kuwa filamu hiyo imekuja na mapinduzi makubwa kwa kila kitu kuanzia teknolojia na uigizaji. Amedai kuwa yeye na kampuni yake ya Proin, walitaka kuja na kitu tofauti na vilivyozoeleka kwenye filamu za Tanzania.

“Ilitubidi kwa kiasi fulani tutulie, tusome mazingira, tasnia yetu inamiss nini sasa hivi, mashabiki wetu wanahitaji nini sasa hivi,” anasema Lulu.
“Tumejitahidi kufanya production ya tofauti ambayo ina quality nzuri, it needs time, sio kama zamani kwa siku mnaweza mkashoot scene sita, saba, lakini saa zingine production kwa siku tulikuwa tunaweza kushoot scene mbili tu lakini mnahakikisha mnatoka na kitu kizuri,” ameongeza.

Amedai kuwa hata sauti zingine pia ilibidi waziingize upya studio ili kuwa na kitu bora kama ambavyo hufanyika kwenye filamu za Hollywood.

Lulu amesema watu wataweza kununua filamu hiyo kwenye app ya Proin Box kwa shilingi 2,500 tu kwa kupitia huduma za malipo ya simu kama M-Pesa, Airtel Money na zingine huku wale waliopo nje wakiweza kununua kwa credit cards.

Amesema baada ya kuizindua kwa mfumo wa dijitali, filamu hiyo itaanza kuoneshwa kwenye majumba ya sinema na kisha baadaye kuuzwa kwenye DVD. Hata hivyo ameeleza kuwa kwenye DVD hizo kutakuwa na vitu vya ziada kama vile behind the scenes, interview na vitu vingine.

Jumatano, 13 Julai 2016

MZIMU WAAJABU WAITESA MBEYA



WANANCHI wa Kijiji cha Mwela Kata ya Kandete wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya wako hatarini kukumbwa na baa la njaa baada ya kuibuka kile kinachodaiwa ‘mzimu wa ajabu’ ambao umekuwa ukianua unga unapokuwa umeanikwa juani na kupotea hewani katika mazingira ya kutatanisha.

Hali hiyo imejitokeza siku chache baada ya ‘mzimu’ huo kuzuka katika kijiji hicho ikielezwa kuwa unga na mazao mengine yaliyokuwa yameanikwa juani yalipotea hewani.

Kutokana na tukio hilo, imewalazimu wananchi wa Kijiji cha Mwela kutisha mkutano wa halmashauri ya kijiji kujadili na kutafuta suluhu ya hali hiyo.

Akizungumza na mwandishi kuhusu tukio hilo, mkazi mmoja wa kijiji hicho, Hamfrey Mwakitwange, alisema kuibuka kwa mzimu huo kumezua hofu kwa wakazi wa Mwela na maeneo ya jirani.

Alisema mwaka huu kuna hatari ya kutokea ukame na baa la njaa baada ya kuibuka mzimu huo wa ajabu.

“Kwa tukio la kuwapo mzimu huu wa ajabu tumejawa na hofu kubwa na kuna dalili ya kukumbwa na baa la njaa mwaka huu.

“Mzimu umekuwa ukichukua chakula hasa unga na mazao yanayoanikwa juani…tunabaki tunajiuliza, na sasa kimeitishwa kikao cha halmashauri ya kijiji ingawa mtazamo umegawanyika… sasa kuna wengine wanataka hata tuhushishe waganga,” alisema Mwakitwange.

Mjumbe wa Nyumba 10 wa CCM, Matrida Mwaisumbwa, alisema kitendo cha kuibuka mzimu huo ambao umekuwa ukichukua chakula, umeleta sintofahamu kijijini hapo.

Alisema hata wanapokuwa wanapika chakula kama ugali au ndizi, kimekuwa hakina radha na inadaiwa chakula hicho pia kinakuwa kimetembelewa na mzimu huo wa ajabu.

Alisema uongozi umeandaa mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba kukusanya michango kuwasaidia wananchi ambao wamekwisha kuathirika na mzimu huo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwale, Ferki Mwandenga, alisema licha ya kuwapo taarifa za mzimu huo wa ajabu anashindwa kuieleza kwa kina hali hiyo.

“Siwezi kulisema hili jambo maana linachanganya kidogo, sijui ni tukio la kichawi? Ingawa pamoja na hali hiyo, tambua kuwa Serikali haiamini uchawi,” alisema Mwandega.

MAJAMBAZI YAWATOROKA POLISI MBEYA WENGINE WAWILI WAUWAWA





watu wanne waliokuwa na pikipiki wanaodiwa kuwa majambazi waliokuwa wamepanga kupora fedha kutoka taasisi moja ya fedha na maduka ya biashara huko Tukuyu Rungwe Mbeya, hili ni tukio la pili la ujambazi kutokea ndani ya miezi miwili mkoani Mbeya
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya amesema watu wawili waliuwa na polisi katika mapambano hayo na polisi na wawili wametoroka, waliouawa walikutwa na silaha mbili bastola na gobore
Kamanda huyo amesema wote ambao hawajasajili silaha zao mpaka sasa watakuwa na makosa kwa kuwa ndio zinazotumika kufanya uhalifu

ANAYEDAIWA KUHAMISHA SHILINGI MILIONI SABA KWA DAKIKA AFIKISHWA MAHAKAMANI


Mfanyabiashara Mohamed Mustapha (anayeongea na simu) na wenzake, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana kukabiliana na tuhuma za kuibia Serikali kodi ya Sh milioni 7 kwa kila dakika kwa kipindi kirefu.
 **
Hatimaye mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa amekuwa akiibia Serikali takriban Sh7 milioni kwa dakika, amepandishwa kizimbani na wenzake wanne na kusomewa mashtaka 199, wote kwa pamoja.

Mfanyabiashara huyo, Mohamed Mustafa Yusufali na wenzake Alloyscious Gonzaga Mandago, Isaac Wilfred Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif Kabla, walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

 Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka za Serikali, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh15 bilioni.

Katika ya mashtaka hayo, Yusufali maarufu kwa majina ya Mohamedali, Choma au Jamalii anakabiliwa na mashtaka 198 yeye peke yake huku wenzake wakikabiliwa shtaka moja la utakatishaji fedha.

Kutokana na wingi wa mashtaka hayo, waendesha mashtaka wawili; Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai walilazimika kubadilishana ili kuwapa muda wa kupumua.

Kutokana na kukabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na shtaka la kutakatisha fedha, washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu na kulingana na mashtaka yanayowakabili, hayana dhamana.

Baada ya kumaliza kuwasomewa mashtaka hayo, upande wa mashtaka uliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Hivyo, Hakimu Mkazi, Huruma Shahidi anayesikiliza kesi hiyo aliamuru washtakiwa wapelekwe mahabusu hadi Julai 25, kesi hiyo itakapotajwa tena.

Kabla ya kupandishwa kizimbani, Yusufali alitajwa na Rais Magufuli kuwa ana mashine inayotoa risiti za kielektroniki (EFD) nje ya mfumo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuzisambaza kwa wafanyabiashara wengine, hivyo kujiingizia Sh7 milioni kwa dakika.

Rais Magufuli alieleza kuwa mtandao wake unawashirikisha watumishi wa TRA na Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brela), hivyo kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya shilingi.

 Katika mashtaka hayo, Yusufali anakabiliwa na mashtaka 181 ya kughushi, mashtaka 15 ya kuwasilisha nyaraka za uongo, udanganyifu katika kulipa kodi moja, shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh15,645,944,361, huku shtaka moja tu la utakatishaji fedha ndilo likimhusisha na wenzake.

Waendesha mashtaka hao walidai kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa akighushi nyaraka za kampuni mbalimbali, kuonyesha kuwa zimesajiliwa na zinaendesha  shughuli zake nchini kihalali wakati akijua siyo kweli.

Pia, walidai kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa akiwasilisha nyaraka za uongo TRA.

Kuhusu shtaka la kutakatisha fedha, upande wa mashtaka ulidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja kati ya Machi 2011 na Januari 2016, walitakatisha Sh1,895,88500 kwa kujifanya kuwa ni malipo ya  mikopo waliyoipokea kwa watu mbalimbali.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa kati ya Januari 2008 na Januari 2016, mfanyabiashara huyo alifanya udanganyifu katika kuwasilisha kwa Kamishna Mkuu wa TRA taarifa ya uongo ya marejesho ya mapato, hivyo kuikosesha Serikali mapato ya kodi ya VAT zaidi ya Sh15.6 bilioni.

Jumanne, 12 Julai 2016

LINAH : AAHIDI PENZI LAKIFICHO KWA MWENZI WAKE



Msanii Linah Sanga ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya 'Imani' amefunguka na kusema kuwa kwa mambo ambayo tayari yamemkuta kwenye mahusiano hayupo tayari tena kumuweka wazi mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii.

Linah Sanga akiongea kwenye kipindi cha Enews amesema kwamba kwa sasa yeye hayupo tayari kumuweka wazi mpenzi wake kama ilivyokuwa awali kwani jambo hilo kwanza linapelekea watu kuanza kufuatilia maisha yake ya mahusiano na si kazi zake za muziki.

Mbali na hilo Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa wapo watu kwenye mahusiano wanaingia ili kutaka kuonja penzi la mtu na kuona huyo mtu yupoje kwenye mapenzi ila hawana mipango endelevu wala hawaangalii mipango ya baadaye.
Msanii Linah Sanga ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya 'Imani' amefunguka na kusema kuwa kwa mambo ambayo tayari yamemkuta kwenye mahusiano hayupo tayari tena kumuweka wazi mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii.


AKIWA SAFARINI: MUSEVEN APOKEA SIMU KWA STAILI YA KIPEKEE



Rais Mseveni aliamua kusimamisha msafara wake na kushuka ili aweze kupokea simu.Hali hiyo ikafanya wasaidizi wake wampe na kiti kabisa ili asikilize simu yake kwa raha na amani bila bughuza.Simu hiyo inaonekana ilikuwa muhimu sana kiasi Rais hakutaka mazungumzo yake kusikilizwa na wasaidizi wake wala walinzi wake.Baada ya kumaliza mazungumzo yake aliongea na wananchi.


MSANIFU WA SOKO LA KARIAKOO AFARIKI DUNIA



HII NDIO HISTORIA YA SOKO LA KARIAKOO

Katika mwaka 1914, Serikali ya kikoloni ya Ujerumani ya Tanganyika iliamuru jengo la kwanza katika ardhi kwenye Soko la Kariakoo. Jengo lilijengwa kwa ajili ya kufanya sherehe ya maadhimisho ya kutawazwa kwa Mfalme Kaiser Wilheim, lakini Vita vya Kwanza vya Dunia vilianza kabla ya tukio kuweza kutokea.

Wakati wa vita, Dar es Salaam na Tanganyika zilianguka chini ya utawala wa Uingereza. Jeshi la Uingereza lilitumia jengo kama kambi la kitengo cha jeshi la askari, timu ya mabawabu wa kiafrika ambao waliunga mkono jeshi la Uingereza kwenye vita. Timu ya wachukuzi Watanzania waliotegemezwa kwa askari wa Uingereza katika mapigano.

Baada ya vita mwaka 1919, serikali ya kikoloni ya Uingereza ilibadilisha sehemu hiyo na kuwa soko. Soko likaitwa "Kariakoo", ambayo ni tafsiri ya Kiswahili ya neno "Jeshi la askari", kwa heshima ya watu waliopigana katika vita. Kadri Dar es Salaam ilivyozidi kukua kama jiji, mazao kadhaa wa kadha yalipitia soko hilo kwa wingi, mnamo miaka ya 1960, baada ya uhuru wa Tanzania, serikali ndogo ya Nyerere iliamuru simenti na magenge imara yajengwe kwa ajili ya wauzaji.

Mwaka 1970, serikali ya taifa iliagiza Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam wafanye mipango ya ujenzi wa soko la kisasa litakalodumu kwa miaka hamsini mpaka sabini. Uongozi wa kitaifa uliiagiza Halmashauri ya Jiji kushirikisha sehemu muhimu ya soko la mazao lililopo katika Jiji Accra nchini Ghana na Lusaka nchini Zambia.



Msanifu majengo Mtanzania Beda J. Amuli alichora ramani ya jengo jipya na ujenzi ulianza Machi 1971, iliyoongozwa na kampuni ya Kitanzania Mwananchi Engineering and Contracting Co. Soko lilikamilika Novemba mwaka 1975 kwa gharama ya shilingi milioni 22 pesa ya Kitanzania.

Sehemu ya soko ina majengo mawili, jengo kuu lenye ghorofa tatu yenye magenge na maofisi, na jengo dogo la pili. Vyote kwa pamoja vikijumuisha eneo la mita za mraba zaidi ya 17,000. Desemba 8, 1975 Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere alifungua soko jipya la kihistoria kwa hafla.

Kabla ya ujenzi kuisha, Oktoba 1974 Bunge ilianzisha Shirika la Soko la Kariakoo (SMK) na kuihusisha na kazi za uendeshaji wa soko. SMK ilipaswa kujilipia uendeshaji wake kwa kupangisha magenge kwa wauzaji na kuwatoza asilimia ya faida ya mauzo. Shirika lilipewa fedha na fungu la jumla la shilling za kitanzania milioni 25, ambayo ilimilikiwa na serikali kwa asilimia mia.

Mkataba wa soko ulithibitisha kua SMK itaongozwa na Meneja Mkuu na bodi ya wakurugenzi ambao wote watateuliwa na rais mwenyewe. Meneja mkuu na bodi nzima walipaswa kuchagua maafisa watakaoongoza soko pamoja nao.

Kabla ya ujenzi kumalizika, katika mwezi kumi mwaka 1974, Bunge lilithibitisha Shirika la Soko la Kariakoo (SMK), shirika la serikali litakaloendesha soko. SMK liliombwa kujilipia shughuli zake kwa kupangisha maduka kwa wachuuzi na kuchukua asilimia ya faida ya mauzo.

Kwa kuanza, Shirika liligharamiwa na Hisa zilizofikia milion 25 za Kitanzania kwa jumla, zilizomilikiwa na serikali kwa 100%.

Toka mwaka 1975, Shirika la Soko la Kariakoo linaendelea kuendesha soko chini ya uongozi wa Serikali ya Tanzania. Soko linaendelea kuwa mahali pakuu pa kuuza mazao Tanzania.