Jumamosi, 24 Septemba 2016

NJIA ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA MAFANIKIO




Kila mmoja anahitaji mafanikio makubwa kwa kile anachokifanya siku zote, japo tatizo huwa ni namna ya kukabiliana na changamoto zinazomsonga ili asifike malengo.

Kuna wakati mwingine tunajikuta tunakata tamaa baada ya kuona baadhi ya changamoto zinatokea na kuzuia mafanikio ambayo tumejipangia. Changamoto hizi zimekuwa zikijitokeza katika biashara, elimu, kazini hata mara nyingine kufiwa na mtu ambaye ulikuwa una mtegemea kwa namna moja ama nyingine pamoja na changamoto nyingine nyingi.

Wakati mwingine changamoto zikitokea, wengi hukata tamaa na muda mwingine kujiona hufai kuendelea kuishi. Wapo wanaofikia hatua ya kukufuru kwa kutoa kauli kama vile Mungu anapendelea, dunia haina usawa na maneno mengine mengi yanayofanana na hayo.

Lakini wasichokielewa watu ni kwamba changamoto ni njia ya kufikia mafanikio tunayoyahitaji. Pia changamoto huja ili kupima imani na uwezo wako kama kweli unaweza kupambana vitani.

Zifuatazo ni baadhi ya njia ya jinsi ya kukabiliana na changamoto katika maisha ya kila Siku;

Kwanza, zikubali changamoto; Kama nilivyoeleza hapo awali, changamoto ni lazima zitokee katika safari yako ya mafanikio, hivyo hakikisha na kisha utafute mbinu zakuweza kupambana nazo.

Unaweza kuanzisha biashara, lakini katikati ya safari ukakimbiwa na wateja, jambo la msingi ni kufanya uchunguzi ni nini kimesababisha hali hiyo, ili uweze kuchukua hatua badala ya kulalamika na kuwanyoshea vidole wengine kwa kuona wao ndio chanzo.

Epuka kukimbilia kwenye imani za kishirikina au mitazamo potofu kama vile chuma ulete, nguvu za giza na mengineyo mengi kwani kufanya kinyume chake kwa kuamini imani hizo si kutatua tatizo bali ni kuliongeza tatizo.

Pili, tafuta washauri. Nafahamu ya kwamba baadhi yetu tuna watu wa karibu ambao huwa tunawaeleza shida zetu. Mfano wazazi, ndugu, marafiki na wengineo.

Pia unaweza kuwatumia viongozi wa dini kwa jambo linao kutatiza, kwani ni watu ambao wana nguvu sana katika jamii hususani suala zima la masuala ya ushauri hasa katika mambo yanayotutiza katika kufikia malengo yetu. Pia unaweza kujifunza kupitia mafunzo mbalimbali kama vile semina kwani kufanya hivyo utaweza kupata majibu ya changamoto zinazokukabili.

Vile vile katika utatuzi wa changamoto, watu wengi huwa tunakosea sana. Huwa tunaanza kuangalia matokeo ya jambo, badala ya kuangalia vyanzo ya matokeo hayo.

Nitaomba kukupa ufafanunuzi wa nukta hii kwa kuangalia mfano mdogo wa ugonjwa wa mlipuko maarafu kama kipindupindu ambao umekuwa ukizuka sana maeneo kadha wa kadha ikiwepo na jiji la Dar-es-salaam, ambapo kila kipindi cha muda fulani huzuka na kuwaathiri watu wengi.

Tatizo kubwa la ugonjwa huu ni kuwa siku zote tunatibu  matokeo, yaani unapotikea viongozi serikalini wanajihimu kuandaa mazingira ya kuwapatia wagonjwa tiba.

Kufanya hivo ni kushughulika na matokeo ya tatizo na kuacha chanzo cha tatizo ambacho kwa mujibu wa wataalamu wa afya ni wananchi kuendelea kuishi kwenye mazingira machafu yanayotoa mwanya watu kula vinyesi kitendo kinachosababisha with kuugua ugonjwa huo.

Tukifuata kanuni hii ya kuangalia chanzo kisha tuangalie matokeo, kuna uwezekano mkubwa wa kushinda changamoto zinazotukabili katika shughuli zetu za kila siku iwe kwenye biashara, kazini, masomoni na maeneo mengine.

Pia naomba usemi huu kila mara "usizibe ufa uktani kabla ya kujua chanzo cha ufa huo"


FACEBOOK IMEPITISHA KIMA CHA WALIOTIZAMA VIDEO ZAKE




Facebook ilipuuza video fupi zilizotazamwa

Facebook imepitisha idadi ya watu waliotazama video katika mtandao huo katika miaka miwili iliyopita kampuni hiyo imekiri.

Mteja mmoja anayetangaza biashara katika mtandao huo amesema kwa wakatimwingine, takwimu hizo zilipitishwa kwa hadi 80%.

Facebook's analytics ni kigezo wanachotumia wafanyabiashara wanaotangaza biashara zao kubaini ni kiasi gani video zao zinatizamwa kwenye Facebook.

Mtandao huo wa kijamii unasema makosa hayo yamerekebishwa na hayajabadili kiwango wanacholipa wafanyabiashara kutangaziwa biashara zao.

'Mwenendo usiokubalika'

Katika taarifa yake, Facebook imesema: "Tumegundua hivi karibuni makosa katika namna tunavyohesabu idadi ya watu wanaoangalia video.

"makosa haya yamerekebishwa, haikuathiri malipo na tumewaarifu washirika wetu," imeongeza.
Kifaa hicho cha kuhesabu kimebadilishwa jina kwa sasa na kimepewa jina "average watch time" na Facebook imeanza kukitumia kukusanya takwimu za watu wanaotizama video mwishoni mwa mwezi agosti.

Jarida la Wall Street limeinukuu kampuni ya Publicis iliosema kuwa Facebook kutoa takwimu za makosa "haikubaliki".

Publicis imesema inaonyesha haja ya kuwa na kampuni ya tatu kuangalia upya takwimu zinazokusanywa na Facebook.

Mtandao huo wa kijamii umewahi kushutumiwa tena katika siku za nyuma kwa kuhesabu video inatazamwa baada ya sekundi tatu tu

FACEBOOK IMEPITISHA KIMA CHA WALIOTIZAMA VIDEO ZAKE




Facebook ilipuuza video fupi zilizotazamwa

Facebook imepitisha idadi ya watu waliotazama video katika mtandao huo katika miaka miwili iliyopita kampuni hiyo imekiri.

Mteja mmoja anayetangaza biashara katika mtandao huo amesema kwa wakatimwingine, takwimu hizo zilipitishwa kwa hadi 80%.

Facebook's analytics ni kigezo wanachotumia wafanyabiashara wanaotangaza biashara zao kubaini ni kiasi gani video zao zinatizamwa kwenye Facebook.

Mtandao huo wa kijamii unasema makosa hayo yamerekebishwa na hayajabadili kiwango wanacholipa wafanyabiashara kutangaziwa biashara zao.

'Mwenendo usiokubalika'

Katika taarifa yake, Facebook imesema: "Tumegundua hivi karibuni makosa katika namna tunavyohesabu idadi ya watu wanaoangalia video.

"makosa haya yamerekebishwa, haikuathiri malipo na tumewaarifu washirika wetu," imeongeza.
Kifaa hicho cha kuhesabu kimebadilishwa jina kwa sasa na kimepewa jina "average watch time" na Facebook imeanza kukitumia kukusanya takwimu za watu wanaotizama video mwishoni mwa mwezi agosti.

Jarida la Wall Street limeinukuu kampuni ya Publicis iliosema kuwa Facebook kutoa takwimu za makosa "haikubaliki".

Publicis imesema inaonyesha haja ya kuwa na kampuni ya tatu kuangalia upya takwimu zinazokusanywa na Facebook.

Mtandao huo wa kijamii umewahi kushutumiwa tena katika siku za nyuma kwa kuhesabu video inatazamwa baada ya sekundi tatu tu

Ijumaa, 23 Septemba 2016

ZIJUE MBINU 5 ZA KUONGEZA KIPATO




Suala la kuongeza kipato ni la msingi sana na lina umuhimu mkubwa kwa kila mmoja. Si watu wengi sana duniani wana kipato cha kutosha kutimiza ndoto zao maishani,wakati mwingine hata kukidhi mahitaji ya msingi kama chakula, malazi, mavazi ,afya na elimu binafsi na za watoto wao.

Kama ilivyo kwangu binafsi naamini pia kuna umuhimu mkubwa wa kuangalia namna nyingine tofauti na kile unachokifanya sasa hivi ambacho kitasaidia kuongeza kipato juu ya kile unachopata sasa.

Mbinu 5 Za Kuongeza Kipato Kwa Asilimia 100 Au Zaidi Ya Kipato Chako Cha Sasa
Zifuatazo ni mbinu 5 ambazo zinaweza kumsaidi kila mmoja anayetaka kuongeza kipato chake

1. Anzisha Biashara Yenye Mahitaji Kwa Jamii
Zig Ziglar ,Mwandishi wa vitabu na mwanamasoko maarufu duniani anasema “ukiwasaidia watu wengi kupata wanachotaka nawe pia utapata unachotaka”. Kwa maana nyingine ni kwamba ukitaka kufanikiwa kiuchumi basi tafuta nini watu wanataka na tengeneza bidhaa au toa huduma kujaza mahitaji hayo ya watu.

Kwahiyo unaweza kuongeza kipato chako kwa kuanzisha biashara inayotoa suluhisho la matatizo ya watu au huduma inayohitajika na watu.

Kama watu wanahitaji kupunguza uzito kutokana na hatari za kiafya hivyo wangependa kupata suluhisho ya tatizo lao,hivyo unaweza ukaanzisha huduma ya mazoezi kwa kuanzisha nyumba ya mazoezi pamoja na kuweka walimu wa kuwasidia wateja wako.  Wateja wanaweza kujisajili na kulipa ada ya mwaka ya uanachama ili kuhudhuria mazoezi au wakalipa kila wanapohudhuria.

Au unaweza ukaanzisha duka la vyakula vyenye kujenga afya njema kama mbogamboga na unga wa nafaka zisizokobolewa,mafuta yasiyo na rehemu nyingi kama alizeti na ufuta na vyakula vingine visivyo na madhara kwa afya za watu.


2. Ingia Katika Biashara Ya Mtandao
Biashara za mtandao ni biashara ambazo makampuni yanatumia watumiaji kama wasambazaji wa bidhaa zao kwa njia ya mmoja kumjulisha mwingine kwa njia ya mdomo. Na kampuni huwalipa watumiaji hao wasambazaji kwa kazi hiyo.

Biashara hizi zimeshamiri sama barani Amerika na Ulaya na kwa sasa hivi zimeingia mabara mengine ikiwemo Afrika.  Mfumo huu wa biashara unampa mtumiaji na msambazaji faida mara mbili, kwanza faida ya kutumia bidhaa yenyewe na ya pili ni malipo yatokanayo na kuwajulisha wengine kuhusu biashara na kujiunga na matumizi yao ya bidhaa ya kampuni husika.

Watu wengi wana matazamo hasi na aina hii ya biashara, ni wazi kwakuwa watu hawana elimu ya kutosha kuhusu mfumo huu ni kitu cha kawaida kuwa nahofu -inaitwa “hofu ya usichokijua”. Kitu cha msingi ni kupata elimu kwanza ya namna mfumo huu ilivyo. Ukitaka kujua zaidi tuandikie barua pepe au tupigie simu.

Ili kuongeza kipato amua kujifunza bishara ya mtandao na kama ilivyo katika kujifunza chochote njia rahisi ya kufanikiwa ni kufanya kwa vitendo. Chagua kampuni yenye bidhaa nzuri itakayokufaa na itakayofaa wengine pia na ujiunge. Pia angalia kampuni yenye mfumo mzuri wa malipo.

Mwanafalsafa wa biashara na tajiri mkubwa duniani siku za nyuma John D. Rockefeller  alisema “Ni bora kupata 1% toka kwa watu 100 kuliko kupata 100% toka kwa mtu mmoja”. Biashara ya mtandao inasimama katika falsafa hii. Unahitaji kuwa na timu ya watu kadhaa ( 10 kwa mfano) ambao nao wataongea na wengine  na mapato yako na yao yatategemea kazi ya ujumla wao. Unatumia nguvu kidogo kupata kipato kikubwa.

Katika mfumo wa kawaida wa kufanya kazi kama biashara ya kuuza nguo mfano au vifaa vya ujenzi, juhudi ni ya mtu mmoja, ili uongeze mapato unatakiwa kuanya kazi muda mwingi zaidi.



3. Ongeza Mtandao Wa Watu Na Mahusiano
Unaweza kuongeza kipato chako kwa kujenga mtandao na watu mbalimbali na kisha kuwajulisha biashara unazofanya. Wataalamu wa masoko wanasema watu hawanunui bidhaa au huduma yako unayotoa bali wananua mahusiano. Kwa maana kwamba watu ili wanunue bidhaa yako au huduma ni lazima wawe na mhusiano mazuri na wewe kwanza. Mahusiano haya yanaweza kuwa yamejengwa kwa muda mrefu au katika dakika chache mtu alipoingia dukani kwako.

Vitu 3 vinavyomfanya mtu anunue bidhaa yoyote:
Imetambulika kuwa ili mtu anunue kitu vifuatavyo ni vitu muhimu

Utaalamu:  Aamini kuwa wewe mtoa huduma ni mtaalamu katika eneo hilo
Urafiki: Mahusiano yenu ni mazuri yani umejenga urafiki mfano kwa huduma kwa mteja unyoionesha na lugha nzuri unayotumia kwa mteja, watu wanannnua toka kwa watu wanaowapenda
Uaminifu au Imani: Mtu anayenunua ni lazima aamini kuwa mtu anayempa huduma ana uwezo na ni mkweli.
Mambo haya matatu ni muhimu sana kusaidia kufanikiwa katika utoaji wa huduma na mapato ya biashara unayotoa.



4. Tangaza Biashara Zako Katika Mtandao
Matangazo ya biashara ni muhimu sana ili kuwafikishia habari watu wengi. Kuna aina nyingi za kuweza kutangaza biashara kama redio,TV na magazeti lakini hapa tutaangalia aina mpya na yenye nguvu kubwa  ya matumizi ya mtandao wa intaneti. Imefahamika kuwa takribani watu bilioni 3 (Kulingana na taarifa toka mtandao wa internetworldstats.com Nov 2015) wapo katika intaneti kwa maana ya kuwa watu hawa wanatumia mtandao wa intenet aidha kwa mawasiliano,burudani au biashara. Katika hawa wengi wapo katika mamitandao ya kijamii kama facebook Bilioni 1 , Twitter Milioni 400 na Instagram Milioni 100.

Kama unataka kuwafikia watu wengi zaidi duniani basi mtandao wa intaneti ni sehemu ya kufikiria kwanza.

Baadhi ya matangazo katika intaneti yanalipiwa. Na mengine ni bure. Andaa matanzano ya video na weka katika mitandao ya facebook,youtube na picha  katika mitandao ya picha kama intragram an pinterest.

Tovuti na blogu ni kitu kingine ambacho ni muhimu sana nadiriki kusema cha lazima katika karne hii ya habari.

Bill Gate (Tajiri namba moja Duniani kwa muda mrefu) aliwahi kusema “Kama biashara yako haitakuwa katika intaneti basi biashara yako itakufa” akiwa na maana kuwa ni muhimu sana kwa biashara yoyote kujitangaza na kuwo katika mtandao wa intaneti katika karne hii ya digitali. Watu wataendelea kuwa digitali zaidi na huduma nyingi zitakuwa katika mtandao.

Inatabiliwa kuwa katika karne ijayo hata hela zitakuwa katika mfumo ywa kadi na eletroniki tu. Unaweza kuona haya yameshaanzakutokea. Kadi za plastiki zinatumika kununua huduma mbilimbali na huduma za kieletroniki kama “mobile money” na “web wallet” ambapo huhitaji hata kuwa na kadi wala pesa taslimu kufanya miamala.

Hivyo ili kuoneza kipato tangaza huduma unazitoa kupitia mtandao na jenga biashara yako katika mtandao



5. Ongeza Elimu Na Utaalamu Katika Kazi
Unaweza kuongeza kipato zaidi kwa kuboresha kili unachofanya sasa. Mfano kama wewe umeajiriwa basi unaweza kupata malipo zaidi kwa kukuza ujuzi wako na kupandishwa cheo na kulipwa mshara mkubwa zaidi.

Jenga uwezo wa kuweza kufanya vizuri zaidi na kuzalisha zaidi ili kuweza kupata malipo maradufu.
Anza kozi katika muda wa jioni au kozi ya mbali. Lakini uanaweza kwenda chuoni na kusoma kwa masaa yote kama unaweza kupata ruhusa hiyo kazini kwako.

Kama umejiajiri na unafanya bishara binafsi ni muhimu kujifunza kitu kipya na kupata taaluma zaidi ambayo itakusaidia kuboresha biashara yako na kuongeza mapato.

Mwisho
Natumaini makala hii itakusaidia katika maamuzi yako kuhusu kuongeza kipato kwa asilimia 100 ya kile unachopata sasa na kuboresha maisha tako na familia yako.


Tafuta matatizo ambayo watu wanayo na yanahitaji ufumbuzi,buni na jenga suluhisho litakalowasaidia watu na matatizo yao na utafanikiwa kuongeza kipato chako wakati ukiwasaidia watu katima matatizo yao.

Jumapili, 11 Septemba 2016

HIZI NDIO MBINU ZA KUMNASA MTEJA KWENYE BIASHARA YAKO




Kazi kubwa sana unayohitaji kufanya baada ya kumpata mteja ni kuhakikisha anaendelea kuwa wako, yaani anaendelea kufanya biashara na wewe.

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kuwafikisha wateja kwenye biashara zao, lakini wateja wanapofika na kupata huduma huondoka na wengi kutokurudi tena.

Ni rahisi sana kumuuzia mteja ambaye ulishamuuzia awali, kuliko kumuuzia mteja mpya. Hivyo kama ukiweza kuiendesha biashara yako vizuri, wateja ambao wananunua kwako watakuwa wateja wako wa kudumu.

NAPENDA BIASHARA
Zifuatazo ni mbinu kumi unazotakiwa kuanza kuzitumia leo kwenye biashara yako ili kuhakikisha wateja wako wanaendelea kufanya biashara na wewe.

1. Tekeleza ulichoahidi.
Kama umemtangazia mteja kwamba akija kwenye biashara yako atapata kitu fulani, basi hakikisha anapata kitu hiko. Hakuna kitu ambacho watu hawapendi kama kudanganywa. Mteja anapoona kwamba amedanganywa hatorudi tena kwenye biashara yako na utakuwa umemkosa milele. Hakikisha unatimiza ulichomwahidi mteja wako.

2. Ahidi kikubwa na pitiliza(overpromise and overdeliver)
Najua hapa unaweza usielewe kwa sababu ulichozoea ni kuahidi kidogo na kupitiliza(underpromise and overdeliver). Hii ilikuwa unafanya kazi zamani, ila kwa sasa, haifanyi kazi tena. Kwa sababu kama wewe unaahidi kidogo, wenzako wanaahidi kikubwa na wanafanyia kazi. Hivyo kitu pekee cha kuhakikisha unawabakisha wateja ni kuwaahidi makubwa na kuyapitiliza hayo. Kama umejitoa kweli kwenye biashara yako, hili halitakushinda.

3. Imarisha mawasiliano yako na wateja wako.
Ni muhimu sana uwe na mawasiliano na wateja wako. Bila ya kujali ni biashara gani unafanya, kuna na mfumo w akupata namba za simu, au barua pepe za wateja wako. Mata kwa mara watumie ujumbe ukiwatakia heri na wakati mwingine kuwajulisha bidhaa au huduma mpya zilizopo kwenye biashara yako.

4. Fanyia kazi malalamiko ya wateja haraka.
Wateja wanapokuwa na malalamiko, yafanyie kazi haraka sana. Usisubiri mpaka yawe makubwa kiasi cha kuwafanya watafute mahali pengine wanakoweza kufanya biashara bila ya matatizo wanayopata kwako.

5. Toa huduma bora ambazo mteja hawezi kupata popote.
Huduma kwa wateja, mteja amepokelewaje, ameelezwaje kuhusiana na bidhaa au huduma anayohitaji, maswali yake yamejibiwaje, hivi ni vitu vinavyoonekana vidogo sana ila vina maana kubwa sana kwa wateja wa biashara yako. hakikisha wateja wako wanapata huduma ambazo zitawafanya wajisikie ufahari.

6. Wakumbuke wateja waliopotea.
Kama biashara yako imekuwepo kwa muda, kuna wateja waliokuwepo awali ila kwa sasa hawapo tena. Kuna wateja ulikuwa unafanya nao biashara zamani, ila kwa sasa huwaoni tena kwenye biashara yako. ni vyema kuwatafuta na kujua kwa sasa biashara wanafanya na nani na ni kitu gani limewafanya hawaji tena kwako.

7. Muuzie mteja baada ya kumuuzia.
Mara nyingi mteja atakuja kwako akitaka kitu fulani, lakini pia anaweza kuwa anataka vingine zaidi ya alichofuata hapo. Ni jukumu lako kujua mahitaji haya yote ya mteja wako na kuyafanyia kazi. Usiishie kumuuzia mteja kitu kimoja pekee, hakikisha kila anachohitaji ambacho kipo kwenye biashara yako, unampatia. Ataendelea kuja kwako kwa sababu anajua mahitaji yake yote anayapata kwako.

8. Pima thamani ya mteja ya muda mrefu.
Kuna wateja ambao wananunua mara moja na kuondoka na kuna wateja ambao wataendelea kununua kwako kwa muda mrefu. Wateja wanaonunua mara moja na kuondoka unaweza kupata faida kubwa, lakini ndio imeishia hapo. Wateja ambao wananunua muda mrefu unaweza kupata faida ndogo, ila utaendelea kuipata kwa muda mrefu. Jua wateja wale wa muda mrefu na endelea kuwapatia thamani nzuri.

9. Tumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii kuwa karibu na wateja wako.
Mtandao umerahisisha sana mfanyabiashara kuwa karibu na wateja. Hakikisha biashara yako ipo kwenye mtandao kwa kuwa na tovuti, kuwa na blogu na kuwa na kurasa kwenye mitandao ya kijamii. Utatumia mitandao hii kutoa taarifa muhimu kuhusiana na biashara yako.

10. Toa zawadi na motisha kwa wateja.
Kuwa na njia ambapo utatoa zawadi mbalimbali kwa wateja wanaorudi tena kwenye biashara yako. inaweza kuwa kuwapatia kuponi za punguzo kadiri wanavyonunua mara nyingi, au kutoa punguzo la bei kama mteja ananunua mara nyingi. Vyovyote vile hakikisha mteja anapata motisha pale anaponunua kwako kwa muda mrefu.

Anza kufanyia kazi mambo hayo kumi ili kuboresha uhusiano wako na wateja wako na uweze kukuza biashara yako.

Ijumaa, 22 Julai 2016

HALMASHAURI KUU CCM YAMPENDEKEZA DR.JOHN POMBE MAGUFULI KUWA MWENYEKITI WA CHAMA TAIFA



Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelipitisha kwa kauli moja jina Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, John Magufuli kuwa mgombea wa uenyekiti wa chama hicho

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelipitisha kwa kauli moja jina Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, John Magufuli kuwa mgombea wa uenyekiti wa chama hicho akimrithi mtangulizi wake Jakaya Mrisho Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma, Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, Christopher Ole Sendeka amesema kuwa baada ya NEC kupitisha jina hilo ni wajibu wa Halmashauri kuu ya Taifa kuwasilisha jina hilo kwenye mkutano mkuu wa CCM utakaofanyika kesho kwenye ukumbi wa mpya wa CCM.

Ole Sendeka amesema kuwa ana imani na wajumbe wote wa mkutano Mkuu maalum wa CCM kuwa watampa kura za kutosha Dk, Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa CCM tangu kuanzishwa kwake.

Awali akifungua kikao cha NEC Mwenyekiti wa CCM Dk, Jakaya Kikwete amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kiko imara na kwamba kama hakikuvunjika mwaka 2015 hakitavunjika tena kutokana na mgawanyiko wa wanachama uliokuwepo katika kupata jina la mgombea urais kupitia chama hicho.

PANYA SASA KUTUMIA UZAZI WA MPANGO



CHUO Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kimepata suluhisho la kupunguza kuzaliana  panya nchini, kwa kuanzisha uzazi wa mpango kwa wanyama hao.

Akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana, Mtaalamu wa Kilimo wa Chuo hicho, Thoneson Mhamphi alisema, utafiti huo ambao upo katika hatua za awali  haujaweza kusambazwa.

Mhamphi alisema dawa hizo za uzazi wa mpango zinazojulikana kama Quinestro na Levonorgester, zimekuwa zikichanganywa kwenye chakula na kuwapatia panya hao, hatua  inayowafanya washindwe kuzaliana.

“Huu utafiti ndiyo tumeanza kuufanyia kazi hivi sasa na   umeonyesha mafanikio kwa sababu  baada ya kuwapa chakula hicho panya hao wameacha kuzaana,” alisema.

Alisema dawa hiyo husababisha panya dume kuwa na nguvu ndogo ya kuzalisha kwa vile kizazi cha jike hujaa maji.

Mtaalamu huyo alisema panya wana  kasi ya kuzaliana ana anaweza kuzaa kila baada ya wiki tatu.

Vilevile, panya ana uwezo wa kupata mimba  tena  saa 24 baada ya kuzaa, alisema mtaalamu huyo.

Alisema   utafiti huo   unaendelea kufanyika katika hatua nyingine   kuona jinsi ya kukabiliana na panya waliopo   mashambani.

“Mlipuko wa panya ni mkubwa  na kama tusipopata njia za kuwadhibiti, hali katika mashamba yetu inaweza kuwa mbaya kabisa,” alisema.