Jumamosi, 24 Septemba 2016

NJIA ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA MAFANIKIO




Kila mmoja anahitaji mafanikio makubwa kwa kile anachokifanya siku zote, japo tatizo huwa ni namna ya kukabiliana na changamoto zinazomsonga ili asifike malengo.

Kuna wakati mwingine tunajikuta tunakata tamaa baada ya kuona baadhi ya changamoto zinatokea na kuzuia mafanikio ambayo tumejipangia. Changamoto hizi zimekuwa zikijitokeza katika biashara, elimu, kazini hata mara nyingine kufiwa na mtu ambaye ulikuwa una mtegemea kwa namna moja ama nyingine pamoja na changamoto nyingine nyingi.

Wakati mwingine changamoto zikitokea, wengi hukata tamaa na muda mwingine kujiona hufai kuendelea kuishi. Wapo wanaofikia hatua ya kukufuru kwa kutoa kauli kama vile Mungu anapendelea, dunia haina usawa na maneno mengine mengi yanayofanana na hayo.

Lakini wasichokielewa watu ni kwamba changamoto ni njia ya kufikia mafanikio tunayoyahitaji. Pia changamoto huja ili kupima imani na uwezo wako kama kweli unaweza kupambana vitani.

Zifuatazo ni baadhi ya njia ya jinsi ya kukabiliana na changamoto katika maisha ya kila Siku;

Kwanza, zikubali changamoto; Kama nilivyoeleza hapo awali, changamoto ni lazima zitokee katika safari yako ya mafanikio, hivyo hakikisha na kisha utafute mbinu zakuweza kupambana nazo.

Unaweza kuanzisha biashara, lakini katikati ya safari ukakimbiwa na wateja, jambo la msingi ni kufanya uchunguzi ni nini kimesababisha hali hiyo, ili uweze kuchukua hatua badala ya kulalamika na kuwanyoshea vidole wengine kwa kuona wao ndio chanzo.

Epuka kukimbilia kwenye imani za kishirikina au mitazamo potofu kama vile chuma ulete, nguvu za giza na mengineyo mengi kwani kufanya kinyume chake kwa kuamini imani hizo si kutatua tatizo bali ni kuliongeza tatizo.

Pili, tafuta washauri. Nafahamu ya kwamba baadhi yetu tuna watu wa karibu ambao huwa tunawaeleza shida zetu. Mfano wazazi, ndugu, marafiki na wengineo.

Pia unaweza kuwatumia viongozi wa dini kwa jambo linao kutatiza, kwani ni watu ambao wana nguvu sana katika jamii hususani suala zima la masuala ya ushauri hasa katika mambo yanayotutiza katika kufikia malengo yetu. Pia unaweza kujifunza kupitia mafunzo mbalimbali kama vile semina kwani kufanya hivyo utaweza kupata majibu ya changamoto zinazokukabili.

Vile vile katika utatuzi wa changamoto, watu wengi huwa tunakosea sana. Huwa tunaanza kuangalia matokeo ya jambo, badala ya kuangalia vyanzo ya matokeo hayo.

Nitaomba kukupa ufafanunuzi wa nukta hii kwa kuangalia mfano mdogo wa ugonjwa wa mlipuko maarafu kama kipindupindu ambao umekuwa ukizuka sana maeneo kadha wa kadha ikiwepo na jiji la Dar-es-salaam, ambapo kila kipindi cha muda fulani huzuka na kuwaathiri watu wengi.

Tatizo kubwa la ugonjwa huu ni kuwa siku zote tunatibu  matokeo, yaani unapotikea viongozi serikalini wanajihimu kuandaa mazingira ya kuwapatia wagonjwa tiba.

Kufanya hivo ni kushughulika na matokeo ya tatizo na kuacha chanzo cha tatizo ambacho kwa mujibu wa wataalamu wa afya ni wananchi kuendelea kuishi kwenye mazingira machafu yanayotoa mwanya watu kula vinyesi kitendo kinachosababisha with kuugua ugonjwa huo.

Tukifuata kanuni hii ya kuangalia chanzo kisha tuangalie matokeo, kuna uwezekano mkubwa wa kushinda changamoto zinazotukabili katika shughuli zetu za kila siku iwe kwenye biashara, kazini, masomoni na maeneo mengine.

Pia naomba usemi huu kila mara "usizibe ufa uktani kabla ya kujua chanzo cha ufa huo"


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni