Jumanne, 12 Julai 2016

KAGAME AFUATA NYAYO ZA MAGUFULI, AMFUTA KAZI WAZIRI WA AFYA



Kagame amfuta kazi waziri wa afya

Rais wa Rwanda Paul Kagame amemtimua waziri wake wa afya Dr Agnes Binagwaho aliyeongoza wizara hiyo kwa kipindi cha miaka 5.

Dr Binagwaho alikuwa miongoni mwa mawaziri vigogo katika serikali ya Rwanda lakini wadadisi wanasema kutimuliwa kwake huenda kumetokana na utendaji kazi usioridhisha na matatizo yanayoikumba wizara hiyo kwa sasa.

Tangazo lililotiwa saini na waziri mkuu Anastase Murekezi limebainisha kuwa rais wa jamhuri katika mamlaka yake amemfuta kazi waziri huyo bila kutoa maelezo zaidi.

Lakini wadadisi wanasema huenda matatizo yaliyokuwa ndani ya wizara hiyo ndicho chanzo cha waziri huyo kutimuliwa.

Wakati wa mkutano wa kitaifa mwezi Desemba mwaka uliopita,waziri huyo alikosolewa vikali na washiriki waliobainisha tatizo kubwa la ugonjwa wa malaria.

 Dr Binagwaho alikuwa miongoni mwa mawaziri vigogo katika serikali ya Rwanda

Takwimu zilizopo kutoka wizara ya afya zilibainisha kuwa watu zaidi ya milioni 2.5 waliathirika na ugonjwa huo mwaka jana.

Hata hivyo katika kipindi cha miezi sita pekee ya mwaka huu wanahesabiwa wagonjwa milioni 1.,4 idadi ambayo ni kubwa sana ikilinganishwa na miaka 5 iliyopita ambapo Rwanda ilikuwa miongoni mwa mataifa yaliyokuwa katika nafasi nzuri ya kuangamiza ugonjwa huo.

Tatizo lililobainishwa na wakosoaji ni uzembe uliofanywa na wizara ya afya iliyoagiza vyandarua visivyotimiza viwango vya ubora na kugharimu wizara hiyo dolla milioni 15 za Marekani.

Katika ripoti ya mkaguzi mkuu wa mali ya umma,wizara ya afya ilibainisha pengo la milioni 10 dollar za Marekani zilizotoweka.

Kadhalika swala la utendajikazi mbovu wa hospitali za serikali linalotokana na madaktari bingwa wanaozikimbia hospitali hizo.

wizara ya afya iliagiza vyandarua visivyotimiza viwango vya ubora na kugharimu wizara hiyo dolla milioni 15 za Marekani.

Mwezi uliopita waziri huyo alikiri kuwepo idadi kubwa ya madaktari wanaohamia katika hospitali binafsi wakikimbia mishahara midogo serikalini.

Kuna wanaoona kwamba maamzi yanayochukuliwa kuhusu hayaridhishi kukabiliana na matatizo hayo.

Kuhusu swala la malaria wizara ilikuwa na mkakati wa kutumia washauri wa afya ya uzazi katika kusaidia kutibu ugonjwa huo.

Aidha wizara ilikuwa na pendekezo kwamba waongezewe mshahara na kuruhusiwa kufanya kazi sehemu mbili.
Lakini mswada kuhusu hilo bado unajadiliwa bungeni.


KUTOKA IKULU: MAGUFULI AWAFUNDA WAKURUGENZI WAPYA



Rais JPM amewahutubia Wakurugenzi wa Wilaya,Miji na Majiji Ikulu Dsm
Moja ya jambo analosema limemsikitisha ni mitandao ya jamii kumuandika Luhende kama Msomi mwenye cheti cha hotel Management wakati ana Masters na alikuwa mkaguzi wa elimu wa kanda.

Rais anasema amepitia kwenye mtandao mmoja wa kijamii akaona comment za watu juu ya Luhende akabaki kucheka tu,amemsimamisha Luhende na kuwataka waandishi wa habari wampige picha na waende Sinza kumpiga picha Luhende Meneja wa Hotel na kuzisambaza mitanadaoni

Rais pia anasema anawafahamu Wakurugenzi wake wote,anasikia malalamiko kwenye mitandao ya kijamii,amewaambia wajishangilie wao na si kusikitika kwa kutokushangiliwa na mitandao ya kijamii,anasema hao wasioshangilia kwenye mitandao ni maadui zake,..."Watachonga sana lakini wataka kimya"

Rais anasema zamani nafasi za ukurugenzi zilikuwa "deal",na pale TAMISEMI kulikuwa na mtandao wa kuhongwa ili kuwapatia watu ukurugenzi,aliishagiza Waziri awaondoe wapo watatu pale utumishi ambao kazi yao ilikuwa kuhongwa na kugawa vyeo vya Ukurugenzi.

Rais anasema Wakurugenzi wote aliwapitia jina kwa jina na ndio maana hasafiri ili kufanya mambo yeye mwenyewe na wakati mwingine hulala hata saa nane ili kujiridhisha mambo.

Rais amepiga marufuku Wakurugenzi kutoa "tender" kwa Madiwani na Wanasiasa wafanyabiashara ambao hutumia nafasi zao kushinda zabuni,wapinge kodi ndogondogo kwa wananchi kama za kina mama wauza mchicha,ambao halmashauri zinadai kodi wakati hata mbolea wala mbegu hawakuwasaidia.Watumie madaraka ya kisheria kuwaondoa "watumishi" Miungu watu kwenye vijiji,kata,tarafa na wilaya.

Rais anasema hawezi kuchagua mtu ambaye hawezi kutekeleza sera ya chama cha Mapinduzi wala aamini katika Chama cha Mapinduzi sababu wananchi walichaguwa Chama cha Mapinduzi kutokana na uzuri wa ilani yake.Kwenye mitandao ya Kijamii anasikia kuwa watu wanalalamika anachaguaa watu wasio na "experience",anasema yeye hataki mambo ya ma-experience experience tu,hawezi kuchagua mtu mwenye experience wakati ni mwizi.Kuna watu walijipanga na kutuma "vimemo" ili watu wao wachaguliwe kwenye nafasi hizo,akawafutilia mbali wote waliotumwa na waliotuma.

Rais anasema hawezi kuchagua "",anajuwa kuna watu hawapendi neno  ila yeye hawezi kufanya kazi na **.Waandishi wapige picha cheti cha Luhende ili watu waongo wa mitandaoni washindwe na walegee.(Vi...la...za)

Rais anasema alistuka sana pale majina ya Wakurugenzi yalivyotoka hadharani na kuanza kuona ukosoaji mkubwa mitandaoni,kiasi akaanza kujiuliza nimekosea nini kuteuwa,akaanza kuwa na wasiwasi lakini baadae akajuwa ni maneno tu ya mitandaoni.

Mwisho Rais amewaasa Wakurugenzi wasikilize maneno ya watu na ya mitandaoni,waende kufanya kazi hata kama hawana uzoefu na kama ni uzoefu wataupata huko huko.Ndio maana katika Wakurugenzi waliokuwepo wamerudi 60+.Hakutaka kurudisha Wakurugenzi wezi na mafisadi eti kisa ni uzoefu.

Rais Magufuli: Haiwezekani tunahamasisha wafanyabiashara watumie EFD, lakini sisi serikali tusitumie.

Rais Magufuli: Ikiwezekana, Wakurugenzi waende na EFD kwenye halmashauri zao wakaanze kuzitumia kukusanya mapato.

Rais Magufuli: Wananchi wa chini wanateswa na kunyanyaswa na vikodi vya ajabu ajabu, nawaomba mkatatue kero zao.

Rais Magufuli: Kwa jinsi ninavyoona sura zenu hapa kweli naamini mnaenda kufanya kazi,kwani sura zinaonesha ninyi ndio wenyewe.

Rais Magufuli: Kuna watu wanalalamika fedha zimepotea, hazitapatikana bila kufanya kazi.

Rais Magufuli: Walisema nimemteua mtu anafanya kazi hotelini, waandishi wa habari naomba mpige picha cheti chake.


MGONJWA AFARIKI BAADA YA KUKOSA SHILINGI 2,000 YA CHETI



Patamambo imepata taarifa kuwa huko Tandale Hospitali Dar es salaam  mgonjwa aliyetoka nje ya hospitali na kukaa nje ya hospitali na akalala nje usiku kucha, mashuhuda wanasema hospitali walipopewa taarifa hawakujali.

Mashuhuda wanadai kuwa alishindwa kuhudumiwa kwa sababu alikuwa hana shilingi 2000 ya kadi na mpaka anakata roho alikuwa nje ya hosptali hiyo,tukio hili la kusikitisha limetokea baada ya mgonjwa huyo kuzidiwa na umauti kumkuta.

Mmoja wa mashuhuda amesema kuwa……….>>>’kaja toka jana kaingia ndani baada ya kuingia ndani kwa kuwa alikuwa hajiwezi alivyotoka akafikia akakaa hapa, basi alipofikia akalala mpaka leo asubuhi, tukawa waoga, tukaenda kituo cha polisi tukatoa taarifa, akaja polisi akamwangalia nae akaondoka, mwenyekiti akarudi tena nae akaondoka, mpaka inafikika saa 6;30 akawa anang’ata ulimi anakufa’



POLISI WACHUNGUZA MTANDAO WA KUJIUNGA NA VIKUNDI VYA KIGAIDI




JESHI la Polisi nchini, limesema linafanya uchunguzi kubaini baadhi ya vijana wanaojiunga na vikundi vya kigaidi, vikiwamo IS na Al-Shabaab ili wawachukulie hatua za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa  Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman, alisema wimbi la vijana hao kujiunga na makundi hayo yanayopigwa vita duniani kote, linatokana na ushawishi wa baadhi ya watu.

“Tuna taarifa za kuwapo baadhi ya vijana wa Kitanzania wanaojiunga na vikundi vya ugaidi… suala hili ni la kiintelijensia zaidi, hatuwezi kulizungumzia kiundani, tunaendelea kulifanyia kazi, tutakapofikia sehemu nzuri tutawaambia,” alisema Athuman.

Alisema wakati suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi, jeshi hilo liliendesha operesheni maalumu ya siku mbili, ambayo ilishirikisha nchi 26 za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Alizitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Lesotho, Malawi, Madagascar, Mauritius, Msumbuji, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia, Zimbabwe, Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Shelisheli, Sudan Kusini na Somalia.

Alisema operesheni hiyo iliyojulikana kama ‘Operesheni Usalama III’ ilishirikisha nchi zaidi ya 26 na ilisaidia kukaguliwa kwa magari 1,632 ambayo kati ya hayo, 10 yalikuwa ya wizi huku matano yalibainika yameingiliwa ‘chases’.

Alisema operesheni hiyo pia ilisaidia kukamatwa  pikipiki 12 za wizi, huku 18 zikiendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kutokuwa na vibali halali.

Athuman alisema operesheni hiyo ilisaidia pia kukamatwa aina mbalimbali ya dawa za kulevya, zikiwamo heroine gramu 83, bangi kilogramu 398.6, mirungi kilogramu 30, bunduki aina ya shotgun moja, gobole 11, risasi 104, mkuki mmoja na vipande 15 aina ya exprojel v6, cotex na detonator.

Alisema walikamata wahamiaji haramu 43  maeneo mbalimbali nchini, kati yao 18 ni raia wa DRC, ambao walikamatwa mikoa ya Rukwa na Kagera, wakati 22 wanatoka Burundi waliokamatwa mikoa ya Shinyanga, Tabora na Kagera na raia wawili wa Rwanda walikamatwa Kagera na mmoja wa Kenya alikamatwa Tabora.

“Katika operesheni hii tulifanya ukaguzi katika kampuni mbalimbali zinazofanya biashara ya madini ambapo tatu zilionekana kukosa uhalali wa kupewa leseni ya kuendelea kufanya biashara ya madini,

“Kampuni hizi ni Delicore Metal Company Ltd, Madandwa Gold Mining Export Import (T) Ltd na Alex Mining Co. Ltd, na tatizo lao linaendelea kushughulikiwa na Wizara ya Nishati na Madini. Pia yalikamatwa madini aina ya Acquqmiline Smoky Quartz kilogramu 20.

Alisema pia walikamata gamba moja la kasa mkoani Ruvuma, mbao 410 zilizokuwa zikisafirishwa bila kibali mikoa ya Pwani, Iringa na Morogoro, nyama ya pundamilia kilo 45 na bidhaa bandia.


Jumapili, 10 Julai 2016

SUGU ALIPONZWA NA DOLE LA KATI


Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’ akiwaonesha wabunge wa CCM dole la kati Bungeni Dodoma hivi karibuni, kitendo ambacho kilitafsiliwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa ni tusi, hivyo kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao kumi vya Bunge.

Jumamosi, 9 Julai 2016

WADAKWA WAKIWA NA JENEZA LILILOJAA SILAA ZA KIVITA

walionekana kwa mbali na gari lao wakidai wanasafirisha marehemu kumbe ni majambazi katika msafara wao akiwemo mchungaji na wanandugu wakizuga wanalia sana utazania msiba kweli.
lakini JESH siyo wajinga wa kukubar et mpite mpakani bila kukaguliwa
mshituko mkubwa kumbe marehemu ni risasi mabomu ya kurusha kwa mkono SMG SR
kweli jamaa msiba wao umewageukia!

HAUHITAJI PESA KUPATA PESA

Kila ninapojaribu kushirikisha Rafiki zangu Juu ya dhamira yangu ya kufanya mambo makubwa maishani kama vile kuwa kati ya mabilionea wakubwa 10 nchini Tanzania, huwa ninapata Jibu la "Huwezi", kwamba Hayo ninayotaka kuyafanya yanataka mtaji mkubwa sana.
Hata hivyo, nimeapa kutokata tamaa, kwasababu wanasema "mtu akikwambia Huwezi kufanya Hili" Maana yake.

anakwambia yeye hawezi. Ukiuliza ni Kwanini wanasema "Haiwezekani" kufanya mambo makubwa, Jibu lao huwa ni moja tu nalo ni "mambo mazuri yanataka mtaji" .

Suala la kukosa mtaji limetolewa na watu wengi kama sababu moja Kubwa ya wao kushindwa kujikomboa kutoka kwenye janga kubwa la umaskini na hasa umaskini wa kipato. Kutokana na hali hii, watu wengine wemefikia hapo hata ya kuacha kufikiria Kitu Chochote kinachohusu mafanikio.
Wanasema kila wakiwaza kufanya Kitu chochote cha maendeleo au uwekezaji wanagundua Kuwa hawana hata senti moja ya pesa.

Kwahiyo, mtaji kwao umekuwa ni kizuizi cha wao kufikia maisha mazuri. Hali hii ya kujiona hatuna mtaji ni jambo la hisia zaidi kuliko uhalisia (Ukweli) wenyewe.
Tangu tukiwa wadogo tumeaminishwa uongo Kuwa "Huwezi kufanya Kitu cha maendeleo Mpaka upate pesa Kwanza" . Lakini, Baadae imekuja kugundulika Kuwa suala la kuhitajika pesa na upate pesa ni uongo mtupu.

Tumia akili yako vizuri, itakupa pesa.
Najua utajiuliza maswali mengi bila kupata jibu kamili juu ya usemi huu, na hii ni kutokana na kwamba ukweli, kwa miaka mingi umeweza kusikia na kuambiwa na watu wako wa Karibu Kuwa "unahitaji Kuwa na pesa ili kupata pesa".

Kwa vyovyote vile kama umekuwa ukiambiwa maneno haya mara kwa mara, ni wazi kwamba umekuwa muumini mzuri wa maneno haya. Ni vyema leo ukaanza kuhoji juu yako ya imani hii ambayo umekuwa nayo kwa miaka mingi na inawezekana imechangia hata kukukwamisha kufikia mafanikio makubwa ambayo ni haki Yako ya msingi.

Jaribu leo kuipa akili yako changamoto ya kufikiri nje ya ya mazoea siku zote. Na ukiendelea kuipa akili yako changamoto ya kufikiri upya, ninapenda nikushirikishe walau sababu chache za kwanini ni hatari endapo utaendelea kuamini uongo huu wa kwamba unahitaji kuwa na pesa ili kupata pesa.
Imani ya kwamba ni lazima kuwa na pesa kwanza ili kupata pesa ina athari lukuki na ni mojawapo ya kikwazo kikubwa cha sisi kushindwa kufanikiwa, kwanini ni kwa sababu Inaiba matumaini yako yote.

Kwanini matumaini ni muhimu? Kwa sababu kama huna pesa na ukachagua kuamini uongo huu kuliko kuamini kwamba una nguvu. Unajihisi kunaswa kwenye mbio za sakafuni ambazo uishia ukingoni. Matokeo yake unajihisi na kujisikia Kuwa unahitaji pesa, ili kujinasua kwenye mtego wa umaskini.

Kwahiyo, unapoona huna pesa Kwanza unaamua kuendelea na umaskini wako bila kuchukua hatua yoyote kwasababu wewe unaamini umaskini wako utaondoka tu Siku ukipata pesa - kibaya zaidi ni kwamba siku Hiyo haijulikani itafika! lini inakufanya kuwa mchungu.
Kama unaamini kuwa inahitajika pesa kwanza ili kutengeneza pesa, na huna pesa, basi inawezeka kabisa ukajisikia na kujiona mnyonge mbele ya watu wengine na hatimaye kujiona mwenye mkosi au bahati Mbaya kuliko watu wengine.

Kwahiyo badala ya kuwa na hamasa unapoona mafanikio ya wenzako, wewe unaanza kuwachukia walichonacho. Nadhani mtakubaliana na mimi kuwa hapa Tanzania hali hii ya kuwachukia matajiri bila Sababu inazidi kuota mizizi kadiri siku zinavyozidi Kwenda mbele.
Na badala ya kuongeza kujiamini hadi kufikia mafanikio, unaanza kuona mafanikio ya wengine kama tishio la wewe kupata uhuru wa kipato (fedha). Inakupa kisingizio:

Mojawapo ya jambo la hatari Kubwa kuliko zote ni kutumia uongo huu kama kisingizio au sababu ya wewe kushindwa kuboresha na kuongeza elimu yako juu ya uwekezaji, ujasiriamali na fedha. Badala ya kusonga Mbele na kuchukua kila fursa au mwanya wa kujifunza Juu ya fursa mbalimbali zilizopo, unaamua kuacha kuendelea.

Saa utakayokubali kwamba "haiitajiki pesa kupata pesa" , ndipo mara moja utaanza kujipa Nguvu, matumaini na la muhimu Zaidi, utaacha kutoa visingizio kama sababu ya wewe kushindwa kuchukua fursa fulani fulani zinazojitokeza kila Siku.
Hii ddiyo tofauti ya watu ambao wamefanikiwa na wale ambao hawajafanikiwa. Ewe mtanzania mwenzangu, malalamiko juu ya kukosa mtaji hayatakaa yaishe, kwani hakuna watu maalumu ambao wapo kwaajili ya kukugawia mtaji.

Kupata mafanikio makubwa kunahitaji ndoto ya maisha mazuri, muda, mipango au mikakati. Kikubwa zaidi, tunatakiwa kuchambua na kujua tunahitaji nini ili kuishi maisha ya ndoto yetu.
Ukishafahamu nini hasa mahitaji yako, rahisi kujipanga na kutenda kidogo, huku ukichukua hapo hatua moja baada ya nyingine. Endapo utaweza kuwa na ndoto na baadae ukatenda sawa na ukubwa wa ndoto hiyo, basi ujue kuwa siku moja utaweza kufika kwenye mafanikio makubwa uliyokuwa ukitamani kuyapata.