Dar es Salaam. Wanafunzi walioandamana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakishinikiza malipo yao ya fedha za kujikimu juzi, huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu.
Wanafunzi hao huenda wakaadhibiwa kwa kosa la kukiuka sheria ndogo ya chuo kwa kuandaa mkusanyiko bila kibali cha menejimenti.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Florens Luoga.
Alisema mamlaka za nidhamu chuoni hapo zinaendelea na uchunguzi kubaini nani aliyehusika katika tukio hilo.
Alhamisi, 2 Juni 2016
SINA AMANI NIMEKUWA KAMA NIMEUWA - WEMA SEPETU
Msanii wa filamu na mjasiriamali Wema Sepetu amefunguka ya moyoni kutokana na namna mashabiki wake wa Instgram wanavyomchukulia na kumpa maneno ambayo muda mwingine yanamuumiza na kumkosesha amani na kumfanya ajione ni kama mkosaji mkubwa.
Wema Sepetu ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ha hayo yamekuja baada ya watu kuanza kusema maneno mbalimbali kwa kile alichofanya Wema Sepetu kupost picha ambayo ni promo ya kazi mpya ya msanii kutoka WCB.
Baada ya kupost picha hiyo baadhi ya watu walianza kusema kuwa bidada huyo anatafuta kiki, wengine wakisema kuwa Wema Sepetu kwa Diamond Platnum apindui.
"Kitu ambacho nakiona kutoka Instagram, Watu wanapenda sana fujo fujo, Purukushani, mara huyu na huyu hawaongei, flani kamchukulia flani bwana, yule kafumaniwa. Hicho ndiyo mnachokiona kina kick.
Ila mwisho wa siku ukija kuangalia , ni kweli maana dunia ya leo umbea unauza. Ila jamani ifike muda tukue mimi binafsi kuna vitu vinanichosha actually vimenichosha ifike muda kila mtu aangalie maisha yake na afanye kile kinachomridhisha nafsi yake. kwangu naangalia wat God has to say bout wat im doin... Imekuwa too much tokea nilivyopost uzalendo ikaonekana all sorts of Crazy, But u know wat, I dont care" aliandika Wema Sepetu
"Sasa basi, nitapost ninachotaka nyinyi endeleeni kujudge na kuleta conclusion zenu mnazojua... Iwe nataka attention, iwe natafuta kick, iwe nitokeje, iwe najipendekeza, iwe vyovyote It all comes down to me.
Kuna msemo unasemaga tenda Wema uende zako... Dats how I roll. Na nimekuwa nikifanya hivyo siku zote. Sitegemei na wala sitaki mtu ninae msupport au kumuunga mkono na yeye afanye the same na wala sina haja na kupostiwa.
Niwe sipindui au napindua It doesnt make A difference. Kwanza haya mambo ya kupinduana yameanzaga lini Mungu wangu. Ila instagram mna majungu sana. Mimi siwezi jamani mniachage basi sometimes, sina amani imekuwa kama nimeua" aliongeza Wema Sepetu

Jumatano, 1 Juni 2016
MWANAMKE ALIYEKATAA KUOLEWA ACHOMWA MOTO HADI KUFA
Mwanamke mmoja wa Pakistan aliyechomwa kwa kukataa wito wa ndoa amefariki kutokana na majeraha yake.
Maria Sadaqat ,mwalimu wa shule aliye na umri mdogo alishambulia nyumbani kwake na kundi moja la wanaume siku ya jumapili na kufariki katika hospitali mjini Islamabad siku ya Jumatano.
Familia yake imesema kuwa alikataa kuolewa na mtoto wa mmiliki wa shule ambayo amekuwa akifunza.
Wanakampeni wanasema kuwa visa vya mashambulio dhidi ya wanawake wanaokataa kuolewa ni vingi nchini Pakistan.
Waziri mkuu wa Punjab Shahbaz Sharif alianzisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo.
Babake Maria amesema kuwa mmiliki wa shule hiyo ni mojawapo ya watu waliomshambulia mwanaye.
Polisi wameambia BBC kwamba wanaume hao walimpiga kabla ya kumwagia mafuta ya petroli na kumchoma karibu na eneo la kitalii la Muree,karibu na mji mkuu.

Jumapili, 29 Mei 2016
SIRI YA MAFANIKIO
Mafanikio ni matokeo mazuri ya jambo ambalo unalifanya,mafanikio yanaweza kuwa ya kimwili au kiroho.
Ukweli ni kuwa siri ya mafanikio anayo yule aliyefanikiwa,hakuna aliye na mafanikio makubwa bila ya kupitia siri ambazo nitazielezea.Shauku ya moyo wa mwanadamu ni kufanikiwa katika kila jambo alifanyalo,nilipokutana na mwandishi wa vitabu bwana Errick Shigongo alinieleza baadhi ya siri za mafanikio ambazo mpaka leo naishi nazo,nalala nazo na ninatekeleza kila kukicha.
Ninakushauri na wewe msomaji wangu tenga siku moja mtembelee mtu yeyote ambaye anajihusisha na kipaji chako,fani yako,utaalamu wako huyo ndio atakuwa mfano wa kuigwa katika maisha yako,ikiwezekana muombe awe mlezi wa maisha/uchumi wako.
Hii itakupa hamasa wewe katika harakati za kufikia malengo yako kwa sababu utakuwa na mlezi ambaye tayari ameshafanikiwa katika maisha yake.Unapokutana nae usiogope kumuuliza swali lolote lile kuhusu mafanikio ila zingatia usiingilie maisha yake binafsi.
Zifuatazo ni siri za mafanikio ambazo ukizifuata hakika utatoka hapo ulipo na kusogea karibu na mti wa mafanikio.
1. JIAMINI MWENYEWE
Hii ni siri kubwa ambayo watu wengi hawana,wengi wamekuwa waoga kuanzisha kitu fulani ambacho unakiamini kuwa kitaweza kukuletea matokeo chanya katika maisha yako.Usifikirie wala usijali maneno ya watu ambayo yanakukatisha tamaa,fanya bila kujali watu watazungumza nini juu yako.
Jaribu kujilinganisha na mtu wako wa kuigwa na jenga picha katika akili yako jinsi ambavyo unavyotaka kuwa.Mfano unataka kufungua kampuni kubwa,tengeneza picha ya kampuni hiyo katika akili yako kwanza,jaribu kujiona kuwa wewe ndio mkurugenzi wa kampuni hiyo,siku zote mafanikio huanzia kwenye ndoto.
2. JIFUNZE KILA SIKU.
Wahenga walisema "Elimu haina mwisho",msemo huu unaenda sambamba na siri ya mafanikio kwani ni lazima uwe mtu wa kujifunza kila siku kupitia vitabu,magazeti na mitandao ya kijamii.Hakuna aliyeweza kufanikiwa pasipo kujifunza kwa kusoma,kuhudhuria semina za ujasiliamali au kubadilisha mawazo/uzoefu wa jambo fulani.
3. FANYA PASIPO KAWAIDA
Watu wamezoea kufanya mambo kawaida,hasa kuiga kutoka kwa mtu fulani,kampuni fulani,shirika fulani.
Jaribu kuwa mbunifu katika biashara yako au kazi yako,mafanikio makubwa huletwa na ubunifu.Usijali maneno ya watu juu ya kile unachotaka kukifanya songa mbele huku ukitazama malengo yako uliyojiwekea.
4 USIOGOPE KUSHINDWA
Ukiamua kufanya jambo ambalo liko katika malengo yako ujue ya kuwa kushindwa kuko mbele yako,unaweza ukakutana na vikwazo vingi ambavyo vitakukatisha tamaa usiogope,hata kama ukianguka simama pukuta mavumbi na kusonga mbele kumbuka ya kuwa huwezi kuwa mshindi siku zote.Kumbuka bila ya maumivu hakuna mafanikio.
Ukiogopa kushindwa ujue ya kuwa huwezi kujisimamia/kujiendesha mwenyewe, ujue ya kuwa unajiendesha mwenyewe kwa sababu unaamini katika ndoto zako na unaamini kuwa upo sahihi kwa kila unalolifanya na unaamini mafanikio yatakuja.*USIWE NA WASIWASI WA KUSHINDWA*
5. USISIKILIZE KWA WALIOSHINDWA
Ni mara ngapi umesikia huwezi kufanya hili,huwezi kufanya vile kwa sababu haijawahi kufanywa?Ni mara ngapi umesikia huwezi kufanya hili kwa sababu mimi nilishindwa/mtu flani alishindwa?Binafsi napenda kuambiwa hivyo ili niwe wa kwanza kufanya na kuwaaminisha watu kuwa kitu hicho kinawezekana kufanywa.
Mfano nilipokiwa chuoni,marafiki zangu walinibeza na kuniambia kuwa siwezi kuandika kitabu na kukisambaza Tanzania nzima kwa sababu ya ukosefu wa fedha,niliamua kutafuta pesa kwa udi na uvumba,nikawa mwandishi wa kujitolea katika gazeti flani,baada ya miezi 9 nilipata pesa ya kuchapisha kitabu cha kwanza kopi 4,000 na kusambaza Tanzania nzima.
6. FANYA KAZI KWA BIDII
Watu wengi hukosa ufanisi wa kazi zao kwa kushindwa kufanya kazi kwa bidii,amka asubuhi na mapema ikiwezekana saa 11 alfajili hii itakusaidia wewe kupanga siku yako vizuri,anza na mambo ambayo wewe umejiwekea kuyafanya kila siku Mfano.
Mimi kila siku asubuhi naandika kurasa mbili za hadithi kisha naendelea na shughuli zingine,hii inanisaidia kuendeleza kipaji changu na kuweza kufikiri zaidi.
Hata wewe nakushauri kama unaweza jitahidi kila siku asubuhi tunga na uandike ujumbe mfupi wa maneno wa kutiana moyo tuma kwenye group la whatsap au mtumie rafiki yako hii itaksaidia sana.
7. SAIDIA WATU
Kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali ni kitu kizuri katika maisha ya kila siku,msaada hukuwezesha wewe kufungua milango yako ya mafanikio,sio lazima kusaidia kwa kutoa pesa unaweza kusaidia watu kwa kuwashauri vizuri,kuandika makala nzuri kama hii au kuwatamkia maneno mazuri ya kuwatia moyo na kuwa bariki "UMEBARIKIWA MKONO UTOAO KULIKO UPOKEAO".Usikose kutembelea blog hii kila siku utapata mambo mapya na mazuri yenye kukujenga kisaikolojia na kiuchumi.Ni mimi Bundala Izengo kocha mzoefu.0656669989

Jumatano, 25 Mei 2016
Je wajua Kwa nini Tunakosa Uvumilivu?
Uvumilivu ni hali ya kustahimili machungu.(Maana hii kutokana na kamusi ya Kiswahili sanifu)
Lakini tunaweza kusema uvumilivu ni hali ya kuhimili matatizo mbalimbali yanayotukumba katika maisha yetu ya kila siku.
Kuna sababu kedekede ambazo zinaelezwa kuwa ni chanzo cha kukosa uvumilivu.Katika makala haya nimekuandalia baadhi ya sababu hizo.Kukosa uvumilivu inaweza kusababisha kukosa maadili kazini kwa kuiba,rushwa na ufisadi.Mwandishi wa makala haya ameorodhesha baadhi ya sababu ambazo zinaelezea sababu ya kukosa Uvumilivu.
(1)Mfumo tuliolelewa.
Malezi tuliyolelewa pindi tukiwa watoto wadogo hayakutufunza kuvumilia katika shida,njaa na mateso.,Mfano utakuta mzazi yuko tayari kukopa chipsi ya mtoto wake sio kwa sababu Ana njaa,La hasha bali kwa kuwa amelilia kwa tamaa ya kumuona Fulani anakula ama anataka kuwadolishia wenzake.
Maisha haya yamekuwa yakijenga mazoea mabaya kwa watoto wetu,pia yanaweza kusababisha watoto wetu kujifunza wizi pindi unapokosa pesa ya kununulia hitaji lake ambalo sio la lazima.(sina maana watoto wasinunuliwe chipsi)
(2)Ukosefu wa elimu
Elimu ni mafunzo ambayo yatolewayo kwa mwanadamu ama mnyama katika kujifunza kitu.Wanadamu tumekuwa tukipata elimu kila kukicha na waswahili wanasema elimu haina….(mwisho)
Wengi wetu tumekalili kuwa elimu inatolewa darasani tu,hali ambayo watu wamekuwa wagumu kupokea mapokea mapya kwa tabia ya kujifunza.Elimu hutolewa popote pale chini ya mti nyumbani kwako,kanisana hata misikitini na kazini kwako.
Takwimu zinaonyesha kuwa watanzania wengi ni wavivu wa kusoma vitabu,hali ambayo inawasababisha kukosa elimu kwa njia ya vitabu ambapo ni elimu yenye mafunzo mengi zaidi.
Kukosa elimu kunaweza kumsababisha mtu kuwa na uwezo mdogo wa kupambanua mambo,wengi wetu tumekuwa tukifikilia kufanya maamuzi yasiyofaa kwa sababu ya kukosa elimu ya jambo fulani.
(3)Kutaka mafanikio ya haraka.
Wanadamu tumeumbwa na shauku ya kutaka mafanikio kwa haraka,wengi wetu tumekuwa tukijaribu kupitia njia za panya(mkato) ili kuharakisha kufanikiwa kwa kupata kazi,mchumba,mtaji na mambo mengine yafananayo na hayo.
Tumesahau kuwa ‘haraka haraka haina baraka’tumekuwa tukijaribu kuharakisha kutengeneza maisha mazuri kwa kutoa rushwa ya pesa ama ngono bila kujari kuwa unafanya kosa la jinai na ni hatari kwa afya yako.
Haraka ya mambo wengi huja kujutia,nimeshuhudia rafiki zangu wawili walioajiriwa katika wizara fulani wakifukuzwa kazi kwa sababu ya taaluma zao zilikuwa kinyume na ajira walizokuwanazo.
Mfano.Taaluma yako ni uandishi wa habari,unafanya kazi ya uhasibu kwa sababu mkuu wa kitengo fulani ni ndugu yako.Hesabu na kuandika habari wapi na wapi.
Hata katika mahusiano wengi wamekuwa wakitaka kufanya tendo la ndoa kabla ya kupata baraka kutoka kwa wachungaji,mashehe,wazazi na matokeo yake wanapeana miba na kukimbiana huku wakisema“Ningejua nisingefanya hili”mara nyingi msemo huu huja yalishatokea hivyo ni bora ubadilike sasa,uwe na uvumilivu utafanikiwa katika jambo lako (mvumilivu hula mbivu) ni mimi kocha wako Bundala Izengo kesho tutaangalia madhara yatokanayo na kukosa uvumilivu.
Msomaji wa blog hii makala hii ya leo na kesho nakujenga kisaikolojia ili tuingie kwenye makala ambayo nimekusudia kukuletea katika mfululizo wa makala zangu najua ukinifuatilia vizuri utakuwa mfanya biashara mkubwa,mfanya kazi bora.Nakutakieni SIKU NJEMA MUNGU AWE NANYI KATIKA KAZI ZAKO.

Jumanne, 24 Mei 2016
WILLIAN WA CHELSEA ANENA
Kiungo wa Chelsea Willian amesema mashabiki wa klabu hiyo wanahitaji matokeo mazuri zaidi baada ya timu hiyo kumaliza nafasi ya 10 Ligi Kuu Uingereza.
FALSAFA YA HAPA KAZI TU NI CHACHU YA MAENDELEO
Ikiwa ni miezi kadhaa tangu Falsafa ya HAPA KAZI TU kusikika katika masikio ya watanzania,watu wengi wamehamasika na kujituma katika kufanya kazi.Ni ukweli usiopingika kuwa bila ya kufanya kazi kwa bidii hakuna maendeleo,msemo huu unaenda sambamba na maandiko matakatifu yasemayo ASIYEFANYA KAZI NA ASILE.
Ujio wa falsafa hii umekuwa ukileta chachu kwa wafanyakazi waajiliwa na waliojiajili kufanya kazi kwa bidiii,nguvu zaidi na umakini mkubwa.Katika miaka ya 1990-2015 watanzania wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea hali ambayo iliwafanya kujisahau na kuhisi kuwa huo ndio mtindo wa maishi unaofanyika hapa duniani.
Katika nchi zilizoendelea serikali,makampuni na taasisi mbalimbali zinafanya kazi usiku na mchana na sababu ambayo inaleta matokeo chanya katika uchumi wao.Utafiti wa bwana Wang Qi mhitimu wa chuo kikuu nchini china alitafiti jinsi ambavyo china inavyofanya kazi kwa muda wa masaa 2,200 kwa mwaka akilinganisha na wananchi wa nchi za United Kingdom (UK) wanaofanya kazi kwamuda wa masaa 1,677 Ripoti hii imechwapwa katika gazeti la kila siku la The Gurdian nchini marekeni.
Hapa nchini Tanzania mtanzania mmoja amekuwa akifanya kazi kwa muda wamasaa 8 kwa siku ambayo ni sawa na masaa 176 kwa mwezi,kila mfanyakazi kwa mwaka huchukua likizo ya mwezi mmoja,na ukihesabu sherehe za tanzania mfanyakazi mmoja anapumzika mwezi mmoja kwa mwaka hivyo wafanyakazi wa Tz hupumzika miezi miwili kwa mwaka bila kuhesabu J.Mosi na J.Pili.Hivyo basi kila Mfanyakazi mmoja anafanya kazi kwa muda wa masaa 1760 kwa mwaka.
Katika falsafa hii inaongeza hali ya utendaji wa wafanyakazi na kuwakumbusha wafanyakazi wazembe kuwa wanahitajika kufanya kazi kwa bidii na kuacha mazoea ambayo walikuwa nayo ili kuleta tija na kusukuma gurudumu la maendeleo kwa kasi zaidi.
Sisi kama vijana wa Tanzania tunatakiwa kuwa chachu ya maendeleo ya taifa letu,familia zetu na ndugu kwani kazi ndio msingi wa maendeleo ya taifa lolote duniani.Tembelea blog hii kila siku utapata vitu vipya.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)