Jumapili, 29 Mei 2016

SIRI YA MAFANIKIO

Mafanikio ni matokeo mazuri ya jambo ambalo unalifanya,mafanikio yanaweza kuwa ya kimwili au kiroho.

Ukweli ni kuwa siri ya mafanikio anayo yule aliyefanikiwa,hakuna aliye na mafanikio makubwa bila ya kupitia siri ambazo nitazielezea.Shauku ya moyo wa mwanadamu ni kufanikiwa katika kila jambo alifanyalo,nilipokutana na mwandishi wa vitabu bwana  Errick Shigongo alinieleza baadhi ya siri za mafanikio ambazo mpaka leo naishi nazo,nalala nazo na ninatekeleza kila kukicha.

Ninakushauri na wewe msomaji wangu tenga siku moja mtembelee mtu yeyote ambaye anajihusisha na kipaji chako,fani yako,utaalamu wako huyo ndio atakuwa mfano wa kuigwa katika maisha yako,ikiwezekana muombe awe mlezi wa maisha/uchumi wako.

Hii itakupa hamasa wewe katika harakati za kufikia malengo yako kwa sababu utakuwa na mlezi ambaye tayari ameshafanikiwa katika maisha yake.Unapokutana nae usiogope kumuuliza swali lolote lile kuhusu mafanikio ila zingatia usiingilie maisha yake binafsi.

Zifuatazo ni siri za mafanikio ambazo ukizifuata hakika utatoka hapo ulipo na kusogea karibu na mti wa mafanikio.

1.   JIAMINI MWENYEWE

Hii ni siri kubwa ambayo watu wengi hawana,wengi wamekuwa waoga kuanzisha kitu fulani ambacho unakiamini kuwa kitaweza kukuletea matokeo chanya katika maisha yako.Usifikirie wala usijali maneno ya watu ambayo yanakukatisha tamaa,fanya bila kujali watu watazungumza nini juu yako.

Jaribu kujilinganisha na mtu wako wa kuigwa na jenga picha katika akili yako jinsi ambavyo unavyotaka kuwa.Mfano unataka kufungua kampuni kubwa,tengeneza picha ya kampuni hiyo katika akili yako kwanza,jaribu kujiona kuwa wewe ndio mkurugenzi wa kampuni hiyo,siku zote mafanikio huanzia kwenye ndoto.

2.        JIFUNZE KILA SIKU.

Wahenga walisema "Elimu haina mwisho",msemo huu unaenda sambamba na siri ya mafanikio kwani ni lazima uwe mtu wa kujifunza kila siku kupitia vitabu,magazeti na mitandao ya kijamii.Hakuna aliyeweza kufanikiwa pasipo kujifunza kwa kusoma,kuhudhuria semina za ujasiliamali au kubadilisha mawazo/uzoefu wa jambo fulani.

3.       FANYA PASIPO KAWAIDA

Watu wamezoea kufanya mambo kawaida,hasa kuiga kutoka kwa mtu fulani,kampuni fulani,shirika fulani.
Jaribu kuwa mbunifu katika biashara yako au kazi yako,mafanikio makubwa huletwa na ubunifu.Usijali maneno ya watu juu ya kile unachotaka kukifanya songa mbele huku ukitazama malengo yako uliyojiwekea.

4          USIOGOPE KUSHINDWA

Ukiamua kufanya jambo ambalo liko katika malengo yako ujue ya kuwa kushindwa kuko mbele yako,unaweza ukakutana na vikwazo vingi ambavyo vitakukatisha tamaa usiogope,hata kama ukianguka simama pukuta mavumbi na kusonga mbele kumbuka ya kuwa huwezi kuwa mshindi siku zote.Kumbuka bila ya maumivu hakuna mafanikio.

Ukiogopa kushindwa ujue ya kuwa huwezi kujisimamia/kujiendesha mwenyewe, ujue ya kuwa unajiendesha mwenyewe kwa sababu unaamini katika ndoto zako na unaamini kuwa upo sahihi kwa kila unalolifanya na unaamini mafanikio yatakuja.*USIWE NA WASIWASI WA KUSHINDWA*

5.        USISIKILIZE KWA WALIOSHINDWA

Ni mara ngapi umesikia  huwezi kufanya hili,huwezi kufanya vile kwa sababu haijawahi kufanywa?Ni mara ngapi umesikia huwezi kufanya hili kwa sababu mimi nilishindwa/mtu flani alishindwa?Binafsi napenda kuambiwa hivyo ili niwe wa kwanza kufanya na kuwaaminisha watu kuwa  kitu hicho kinawezekana kufanywa.

Mfano nilipokiwa chuoni,marafiki zangu walinibeza na kuniambia kuwa siwezi kuandika kitabu na kukisambaza Tanzania nzima kwa sababu ya ukosefu wa fedha,niliamua kutafuta pesa kwa udi na uvumba,nikawa mwandishi wa kujitolea katika gazeti flani,baada ya miezi 9 nilipata pesa ya kuchapisha kitabu cha kwanza kopi 4,000 na kusambaza Tanzania nzima.

6.       FANYA KAZI KWA BIDII

Watu wengi hukosa ufanisi wa kazi zao kwa kushindwa kufanya kazi kwa bidii,amka asubuhi na mapema ikiwezekana saa 11 alfajili  hii itakusaidia wewe kupanga siku yako vizuri,anza na mambo ambayo wewe umejiwekea kuyafanya kila siku Mfano.

Mimi kila siku asubuhi naandika kurasa mbili za hadithi kisha naendelea na shughuli zingine,hii inanisaidia kuendeleza kipaji changu na kuweza kufikiri zaidi.

Hata wewe nakushauri kama unaweza jitahidi kila siku asubuhi tunga na uandike ujumbe mfupi wa maneno wa kutiana moyo tuma kwenye group la whatsap au mtumie rafiki yako hii itaksaidia sana.

7.         SAIDIA WATU

Kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali ni kitu kizuri katika maisha ya kila siku,msaada hukuwezesha wewe kufungua milango yako ya mafanikio,sio lazima kusaidia kwa kutoa pesa unaweza kusaidia watu kwa kuwashauri vizuri,kuandika makala nzuri kama hii au kuwatamkia maneno mazuri ya kuwatia moyo na kuwa bariki "UMEBARIKIWA MKONO UTOAO KULIKO UPOKEAO".Usikose kutembelea blog hii kila siku utapata mambo mapya na mazuri yenye kukujenga kisaikolojia na kiuchumi.Ni mimi Bundala Izengo kocha mzoefu.0656669989


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni