Jumatano, 25 Mei 2016

Je wajua Kwa nini Tunakosa Uvumilivu?

  Uvumilivu ni hali ya kustahimili machungu.(Maana hii kutokana na kamusi ya Kiswahili sanifu)
Lakini tunaweza kusema uvumilivu ni hali ya kuhimili matatizo mbalimbali yanayotukumba katika maisha yetu ya kila siku.

Kuna sababu kedekede ambazo zinaelezwa kuwa ni chanzo cha kukosa uvumilivu.Katika makala haya nimekuandalia baadhi ya sababu hizo.Kukosa uvumilivu inaweza kusababisha kukosa maadili kazini kwa kuiba,rushwa na ufisadi.Mwandishi wa makala haya ameorodhesha baadhi ya sababu ambazo zinaelezea sababu ya kukosa Uvumilivu.
(1)Mfumo tuliolelewa.

Malezi tuliyolelewa pindi tukiwa watoto wadogo hayakutufunza kuvumilia katika shida,njaa na mateso.,Mfano utakuta mzazi yuko tayari kukopa chipsi ya mtoto wake sio kwa sababu Ana njaa,La hasha bali kwa kuwa amelilia kwa tamaa ya kumuona Fulani anakula ama anataka kuwadolishia wenzake.

Maisha haya yamekuwa yakijenga mazoea mabaya kwa  watoto wetu,pia yanaweza kusababisha watoto wetu kujifunza wizi pindi unapokosa pesa ya kununulia hitaji lake ambalo sio la lazima.(sina maana watoto wasinunuliwe chipsi)

(2)Ukosefu wa elimu

Elimu ni mafunzo ambayo yatolewayo kwa mwanadamu ama mnyama katika kujifunza kitu.Wanadamu tumekuwa tukipata elimu kila kukicha  na waswahili wanasema elimu haina….(mwisho)

Wengi wetu tumekalili kuwa elimu inatolewa darasani tu,hali ambayo watu wamekuwa wagumu kupokea mapokea mapya kwa tabia  ya kujifunza.Elimu hutolewa popote pale chini ya mti nyumbani kwako,kanisana hata misikitini na kazini kwako.

Takwimu zinaonyesha kuwa watanzania wengi ni wavivu wa kusoma vitabu,hali ambayo inawasababisha kukosa elimu kwa njia ya vitabu ambapo ni elimu yenye mafunzo mengi zaidi.

Kukosa elimu kunaweza kumsababisha mtu kuwa na uwezo mdogo wa kupambanua mambo,wengi wetu tumekuwa tukifikilia kufanya maamuzi yasiyofaa kwa sababu ya kukosa elimu ya jambo fulani.

(3)Kutaka mafanikio ya haraka.

Wanadamu tumeumbwa na shauku ya kutaka mafanikio kwa haraka,wengi wetu tumekuwa tukijaribu kupitia njia za panya(mkato) ili kuharakisha kufanikiwa kwa kupata kazi,mchumba,mtaji na mambo mengine yafananayo na hayo.

Tumesahau kuwa ‘haraka haraka haina baraka’tumekuwa tukijaribu kuharakisha kutengeneza maisha mazuri kwa kutoa rushwa ya pesa ama ngono bila kujari kuwa unafanya kosa la jinai na ni hatari kwa afya yako.

Haraka ya mambo wengi huja kujutia,nimeshuhudia rafiki zangu wawili walioajiriwa katika wizara fulani wakifukuzwa kazi kwa sababu ya taaluma zao zilikuwa kinyume na ajira walizokuwanazo.

Mfano.Taaluma yako ni uandishi wa habari,unafanya kazi ya uhasibu kwa sababu mkuu wa kitengo fulani ni ndugu yako.Hesabu na kuandika habari wapi na wapi.

Hata katika mahusiano wengi wamekuwa wakitaka kufanya tendo la ndoa kabla ya kupata baraka kutoka kwa wachungaji,mashehe,wazazi na matokeo yake wanapeana miba na kukimbiana huku wakisema“Ningejua nisingefanya hili”mara nyingi msemo huu huja yalishatokea hivyo ni bora ubadilike sasa,uwe na uvumilivu utafanikiwa katika jambo lako (mvumilivu hula mbivu) ni mimi kocha wako Bundala Izengo kesho tutaangalia madhara yatokanayo na kukosa uvumilivu.

Msomaji wa blog hii makala hii ya leo na kesho nakujenga kisaikolojia ili tuingie kwenye makala ambayo nimekusudia kukuletea katika mfululizo wa makala zangu najua ukinifuatilia vizuri utakuwa mfanya biashara mkubwa,mfanya kazi bora.Nakutakieni SIKU NJEMA MUNGU AWE NANYI KATIKA KAZI ZAKO.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni