Jumapili, 22 Mei 2016
JINSI YA KUPATA WAZO ZURI LA BIASHARA
Kumekuwa na maswali mengi ambayo nimekuwa nikiulizwa na marafiki zangu juu ya kupata wazo zuri la biashara.Kutokana na takwimu za shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP kuna biashara 4,000 ambazo hubuniwa kila siku,kati ya biashara hizo ni biashara 1740 ambazo huleta matokeo chanya,biashara 2260 huleta matokeo hasi kwa sababu ya kukosa ubunifu au kuwa na wazo baya la biashara.Kabla ya kuendelea tuangalie maana ya maneno yafuatayo.
WAZO LA BIASHARA:Hili ni jambo linalofikiriwa na mtu ili aweze kununua,kuuza au kuchuuza bidhaa fulani kwa nia ya kupata faida.
HATUA MUHIMU NNE ZA KUTENGENEZA WAZO LA BIASHARA
1. UJUZI/UZOEFU WOWOTE
Chukua karamu na karatasi orodhesha changamoto zinazoikumba jamii uliyonayo jaribu kuhusisha na ujuzi au uzoefu ulionao.Mfano mtaani kwako kuna tatizo la wizi wa kupora au wa kuvunja milango,anzisha kikundi cha ulinzi shirikishi chenye watu wasiopungua 15,nenda serikal za mtaa waeleze nia na madhumuni ya kuanzisha kikundi,wasilisha wazo lako kituo kikuu cha polisi kilichopo karibu yako ili usajili kikundi kile kitambulike kisheria,wekeni sheria ndogondogo ambazo zitawabana watuhumiwa mtakao wakamata walipe faini na faini zile zitaingia kwenye kikundi,wasilisha mswada wa sheria kwenye kamati ya ulinzi ya serikali ya mtaa/kijiji ili itengenezwe sheria ndogondogo ambapo kila kaya watachangia Tsh. 1000 kila mwezi kwa ajili ya ulinzi shirikishi,hapo utakuwa umejitengenezea ajira na umetengeneza ajira kwa wengine.
2. KIPAJI CHAKO NI KIPI?
Nikiwa katika mazungumzo na vijana hapa mtaani nilishangazwa na kijana mmoja ambae alisema kuwa hajui kipaji chake.Suala hili lilinizibua fikra zangu na kuona kuwa kuna haja ya kufanya utafiti mdogo kwa kuwahoji vijana kumi.Kati ya vijana hao vijana 2 tu ndio walikuwa wanajua vizuri vipaji vyao na jinsi ya kuvitumia ili kuwapatia kipato,vijana 5 hawajui kabisa vipaji vyao na vijana 3 walikuwa wanajua vipaji vyao lakini hawajui jinsi ya kuvitumia ili kuwapatia kipato. Hii ilikuwa ni changamoto kwangu,kuwaelimisha kujua vipaji vyao na jinsi ambavyo wanaweza kubadili vipaji vyao kuwa bidhaa na kuwazalishia pesa. Msomaji wa makala haya unaweza kubadili kipaji/ujuzi wako kuwa bidhaa na kukupatia pesa kama hujui tuwasiliane kwa email izengobundala@gmail.com au whatsap 0656669989
3. HUDHURIA MAONYESHO YA BIASHARA
Kila tarehe 8/08/kila mwaka huwa ni siku ya wakulima kitaifa maarufu kama nanenane,watu binafsi,makampuni mbalimbali,wajasiliamali wadogo na wakubwa hukusanyika pamoja na kuonyesha maonyesho ya bidhaa zao. Pia kila tarehe 07/07(sabasaba) huwa ni siku ya wafanya biashara ambapo wafanyabiashara wakubwa na wadogo hukusanyika pamoja wakionyesha biashara mbalimbali nyingine kutoka mataifa ya ughaibuni na nyingine kutoka mataifa jirani. Nia na madhumuni ya maonyesho hayo ni kukutanisha wanunuzi,wauzaji na watengenezaji bidhaa kuonyesha jinsi ambavyo bidhaa flani inatengenezwa kwa ubora fulani.Ninakushauri wewe unayesoma makala hii kuhudhuria maonyesho hayo ili uweze kujifunza mengi.
4. MALALAMIKO.
Kumekuwa na malalamiko mengi kwenyemaofisi mengi hasa ya serikali,watu wamekuwa waoga kufuatilia haki zao kwa sababu hawazijui sheria na kwa sababu watu wengi wamenyimwa elimu ya uraia na kujitambua. Unaweza ukatumia fulsa hii kufuatilia haki za watu hawa ambapo utaingia nao mkataba wa kukulipa kiasi fulani cha pesa pindi utakapofanikisha.Mfano huko vijijini kuna migogoro mingi ya mipaka ya mashamba,wewe uliye na elimu tena una shahada ya sheria unabaki mjini kusubili ajira mwaka wa tano sasa nakushauri tumia elimu yako kuwasaidia watu hawa.Unaweza kwenda vijijini ukafungua kampuni ya uwakili ambapo utatoa huduma hiyo ambayo itakupatia kipato kikubwa na chenji inarudi.Asanteni sana nawatakia safari njema ya mafanikio.
Jumamosi, 21 Mei 2016
JE UNAZIJUA NJIA RAHISI ZA KUPATA MTAJI?
Moja ya changamoto ambazo zinawakumba watu wengi ni upatikanaji wa mtaji.Mtaji ni pesa,amana au wazo ambalo linaweza kuleta faida litumiwapo kwa usahihi.Changamoto za mtaji zimekuwa kilio kikubwa kwa watanzania wengi hasa wahitimu wa vyuo na wasiosoma kabisa.
Mahitaji ya mitaji yamekuwa yakiongezeka kadri changamoto ya ajira inavyozidi kuitafuna dunia na wahitimu wengi kukosa ajira za moja kwa moja hali ambayo inadhalilisha usomi wao.Tatizo kubwa lililopo Tanzania ni mfumo mbovu wa elimu uliopo ambao hamfundishi mwanafunzi kujiajili bali unamfundisha mwanafunzi kuajiliwa maofisini nk.
ZIFUATAZO NI NJIA HALALI ZA KUPATA MTAJI
1. ANZA KUWEKA AKIBA.
Hiki ni kipenigele muhimu ambacho watanzania wengi hatukitumii,unaweza kuweka akiba kidogokidogo mpaka kitakapotimia malengo yako(kidogo kidogo hujaza.......).Weka akiba kutoka kwenye pesa unazotumiwa na wazazi wako kwa ajili ya matumizi ya shule/chuo.Kanuni ni rahisi sana unaweza ukaamua kuweka Tsh.1000 kila siku ambapo kwa mwezi ukawa na 30,000/= kwa mwaka 300,000/=
2. UNGANA NA MWENZAKO MWENYE NDOTO KAMA ZAKO.
Hii itakusaidia kubadilishana mawazo jinsi ya kutafuta mtaji na pia huwa ni rahisi sana kwa watu wawili au zaidi kufanikisha ndoto zao.Zingatia kuwa wote mlio katika jambo hilo mnakuwa na lengo moja ambalo ni kufika paleee.Pia ukiungana na wenzako inakuwa ni rahisi kupata mtaji kupitia mikopo ya mabenki,mnaweza kuanzisha sacos kutafuta wadhamini wa wazo lenu n.k
3. JIUNGE NA MAKAMPUNI YA SIMU
Makampuni ya simu yameweza kutoa ajira millioni moja katika mwaka 2014-2015.Ili kuweza kupata ajira hii haihitaji gharama kubwa kwani gharama yako itakuwa ni kununua laini na kuwekewa acces ya usajili ambayo ni bure, kununua simu, pia kununua laini kwa ajili ya kumuuzia mteja.Kazi hii ina faida sana kuliko tunavyofikiria ukimsajili mteja mmoja atakulipa 1,000 palepale,kadri mteja anapoweka vocha na kuitumia ndivyo kamisheni yako inavyozidi kuongezeka.ukisajili wateja 200 kwa mwezi 150 wakaweka vocha ya 500 kila siku,na katika vocha hiyo kuna asilimia 6 unazopewa wewe ambayo ni kama shilingi 60 ambapo 60x150=9000,huyu mtu anaingiza commision ya Tsh. 9,000 kwa siku zidisha mara mwezi 9,000x30= 270,000 na laini hizo utalipwa kiasi hicho kwa muda wa miezi 6.Namaanisha kuwa mwezi wa kwanza ukasajili wateja walio hai 150 ukapata 270,000 mwezi wa pili ukasajili idadi hiyo hiyo utakuwa na jumla ya pesa ya Tsh 540,000 kadri utakavyosajili wateja wengi ndivyo kamisheni yako itapanda.(usiwadharau hao wanatengeneza pesa nzuri ajabu)
4. UZA AMANA ZAKO
Ili kupata mtaji unaweza ukauza simu ya gharama uliyonayo,tv au kitanda.Hakikisha pesa hiyo unaipeleka kwenye malengo uliyokusudia pia uwe na usalama wa mtaji wako na uhakika wa soko la bidhaa ambayo utaiuza.
Asanteni sanaa ni mimi kocha wako BUNDALA IZENGO
ASAMOAH ALAMBA SHAVU CHELSEA
Chelsea wametakiwa kutoa kitita cha paundi milioni 25 kumsajili mchezaji wa miamba wa Italia, Kwadwo Asamoah
Alhamisi, 19 Mei 2016
HIZI NDIZO NJIA ZA KUPATA WAFANYAKAZI BORA
Hulka na tabia za watu ni tofauti,waajili na waajiliwa wanatakiwa kuvumiliana kwa mamabo mbalimbali ambayo yanaweza kuleta fikra hasi kati ya mmoja wa.Si rahisi kwa mwanadamu kuishi bila kukosea ama kufanya kazi bila kukosea.Waajili wengi wamekuwa wakilalamika juu ya wafanyakazi wao kushindwa kufuata maelekezo ambayo wanawapa ili kuleta ufanisi katika biashara/kazi zao.Moja ya changamoto ambazo waajili wengi wanakutana nazo ni kushindwa kutambua changamoto za wafanyakazi wao Jasmini ni mmoja wa waajili ambaye amekuwa akikumbana na changamoto nyingi katika biashara yake.Leo nimekuletea njia mabazo zitakuwezesha kupata wafanyakazi bora
1.KUAJILI WAFANYAKAZ WENYE VIGEZO NA UJUZI:
Uendesshaji wa biashara (hasa ambayo inahitaji mtu aliyesomea kiteengo husika)inahitaji umakini mkubwa kumpata fanyakazi anayefaa.Waajili wengi wamekuwa wakiwaajli watu ambao hawajasomea kazi ile ili aweze kumlipa ujira mdogo.Dada jasmini hii itakula kwako kwani ufanisi wa kazi utakuwa mdgo na wateja watakimbia na biashara kufa kabsaaa.
2.TENGENEZA UPYA PROGRAME(MFUMO) WA UENDESHAJI
Hii inahusisha mambo mengi sana,lkini tuzungumzie tu kuwa unahitaji kuwa na mfumo ambao kila mfanyakazi wako ajisikie kama yuko nyumbani (mfumo rafiki) kuwa na tabia ya kutoa pongezi kwa anayefanya vizuri,sherehe za mwisho wa mwaka n.k 3:WEKA UTARATIBU RAFIKI KWA WAFANYAKAZI:
Kuna wafanyakkaz wengine wana magonjwa mbalimbali na mengine ni siri mfano siku za hedhi za mwanamke,magonjwa yatokanayo na giographia wafanyakaz kama hao waahitaji kuwa na uangalizi maalumu unaweza kumnunulia koti,peds n.k.
4.TENGENEZA MFUMO WA KUNUSA UHALIFU:
Jasmini ukisoma kitabu cha THINK BIG kilichoandikwa na Donalrd Tramp amezungumzia jinsi ambavyo amejiwekea mfumo bora wa kunusa matukio ya uhalifu kabla hayajatokea.Mfano unaweza ukawa umewaajili watu katika kampuni yako lakini mmoja kati ya hao anataka kufanya uhalifu wa kuiba,kuacha kazi bila taarifa inakubdi pate taarifa haraka ili uweze kuweka mamb sawa. 5.WAAMBUKIZE WAFANYAKAZI WAKO:
Simaanishi kuwa unawaambukza magonjwa la hasha namaanisha kuwaambukiza endaji wa kazi,ukubali au ukatae utendaji wa wafanyakazi wako unaakisi utendaji wako wa kazi,mfano ukiwa mzembe watakuwa wazembe tu,ukichelewa kufika ofsini watachelewa zaid yako.
JOHN TERRY LULU YA CHELSEA
Chelsea imetangaza kuwa John Terry amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Antonio Conte amefanya uamuzi wa busara kumbakisha John Terry Chelsea baada ya kufikia makubali ya pamoja na bodi kumpa mkataba wa mwaka mmoja.
Jumatatu, 9 Mei 2016
JE UNAIJUA SAKOLOJIA YA MWENZI WAKO?
Watu wengi wamekuwa wakiishi na wapenzi wao kwa muda mfupi na kuachana.Wengine wamekuwa wakibadilisha wapenzi kila kukicha hali ambayo ni hatari kwa afya zao.
Katika tafit zilizofanywa na mwandishi wa makala haya amegundua kuwa, wengi wao wamekuwa wakikosa elimu ya saikolojia ya mapenzi inayohusu kumsoma mpenzi wako jinsi alivyo na kujua njia ya kukabiliana na changamoto za kimapenzi.
Hakuna aliye mkamilifu duniani kila mmoja ana mapungufu yake,hata kama ukiwa na busara sana hali inayopelekea kusikilizwa,kuaminiwa ama kukukubalika katika jamii lakini ujue ya kuwa kuna zimwi la mapungufu ambalo linakutafuna.
Watu wengi wamekuwa wakishangazwa na ndoa ambazo zimekuwa zikifungwa leo baada ya wiki mbili kunakuwa na mizozano na migogoro ndani ya ndoa hali ambayo inapelekea mmoja wao kufungasha vilago.
Mara kwa mara tumekuwa tukisikia sauti za ‘ningejua nisingeolewa’ ama ‘ningejua nisingeoa’hizi ni sauti ambazo huja baada ya wawili kushindwa kujua saikolojia ya mwenzake.
Changamoto za kujua sakolojia ya mpenzi wako imekuwa ikiumiza ndoa na mahusiano ya watu wengi,sababu kubwa ya kushindwa kujua saikolojia ya mwenzi wako ni kwa sababu ya kukosa elimu ya kutosha kuhusu saikolojia ya mapenzi.
Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini watu wengi wamekuwa na mtandao wa mapenzi?Ama ni kwa nini kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara ya kimapenzi?
Ukweli ni kwamba watu wamekuwa wakijiingiza katika mapenzi bila kujiandaa,napozungumzia kujiandaa sina maana ya kupiga zoezi la kama wacheza mpira ama ndondi la hasha.
Nina maana ya kuchukua jukumu a kusoma vitabu,makala ama kuangalia filamu mbalimbali zinazohusu mapenzi vinavyozungumzia mapenzi na jinsi ya kuishi na watu mbalimbali walio na tabia/hulka tofauti.
Kumbuka kuwa watu tumeumbwa na hulka mbalimbali,lakini wengi wetu wamekuwa wakilazimissha kubadili tabia zao kwa kufuata mkumbo wa marafiki ama makundi mbalimbali ya watu
Katika mfululizo wa makala haya,nitakuletea tabia/haiba mbalimbali za wanadamu na jinsi ya kukabiriana nazo mfano:: kuishi na mchumba mpole,muongeaji,mlopokaji,mkali n.k uskose kuitembelea blog hii.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)