Jumapili, 22 Mei 2016

                                  JINSI YA KUPATA WAZO ZURI LA BIASHARA


Kumekuwa na maswali mengi ambayo nimekuwa nikiulizwa na marafiki zangu juu ya kupata wazo zuri la biashara.Kutokana na takwimu za shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP kuna biashara 4,000  ambazo hubuniwa kila siku,kati ya biashara hizo ni biashara 1740 ambazo huleta matokeo chanya,biashara 2260 huleta matokeo hasi kwa sababu ya kukosa ubunifu au kuwa na wazo baya la biashara.Kabla ya kuendelea tuangalie maana ya maneno yafuatayo.
WAZO LA BIASHARA:Hili ni jambo linalofikiriwa na mtu ili aweze kununua,kuuza au kuchuuza bidhaa fulani kwa nia ya kupata faida.

                          HATUA MUHIMU NNE ZA KUTENGENEZA WAZO LA BIASHARA

1. UJUZI/UZOEFU WOWOTE                            

Chukua karamu na karatasi orodhesha changamoto zinazoikumba jamii uliyonayo jaribu kuhusisha na ujuzi au uzoefu ulionao.Mfano mtaani kwako kuna tatizo la wizi wa kupora au wa kuvunja milango,anzisha kikundi cha ulinzi shirikishi chenye watu wasiopungua 15,nenda serikal za mtaa waeleze nia na madhumuni ya kuanzisha kikundi,wasilisha wazo lako kituo kikuu cha polisi kilichopo karibu yako ili usajili kikundi kile kitambulike kisheria,wekeni sheria ndogondogo ambazo zitawabana watuhumiwa mtakao wakamata walipe faini na faini zile zitaingia kwenye kikundi,wasilisha mswada wa sheria kwenye kamati ya ulinzi ya serikali ya mtaa/kijiji ili itengenezwe sheria ndogondogo  ambapo kila kaya watachangia Tsh. 1000 kila mwezi kwa ajili ya ulinzi shirikishi,hapo utakuwa umejitengenezea ajira na umetengeneza ajira kwa wengine.

2. KIPAJI CHAKO NI KIPI?

Nikiwa katika mazungumzo na vijana hapa mtaani nilishangazwa na kijana mmoja ambae alisema kuwa hajui kipaji chake.Suala hili lilinizibua fikra zangu na kuona kuwa kuna haja ya kufanya utafiti mdogo kwa kuwahoji vijana kumi.Kati ya vijana hao vijana 2 tu ndio walikuwa wanajua vizuri vipaji vyao na jinsi ya kuvitumia ili kuwapatia kipato,vijana 5 hawajui kabisa  vipaji vyao na vijana 3 walikuwa wanajua vipaji vyao lakini hawajui jinsi ya kuvitumia ili kuwapatia kipato. Hii ilikuwa ni changamoto kwangu,kuwaelimisha kujua vipaji vyao na jinsi ambavyo wanaweza kubadili vipaji vyao kuwa bidhaa na kuwazalishia pesa. Msomaji wa makala haya unaweza kubadili kipaji/ujuzi wako kuwa bidhaa na kukupatia pesa kama hujui tuwasiliane kwa email izengobundala@gmail.com  au whatsap 0656669989

3. HUDHURIA MAONYESHO YA BIASHARA

Kila tarehe 8/08/kila mwaka huwa ni siku ya wakulima kitaifa maarufu kama nanenane,watu binafsi,makampuni mbalimbali,wajasiliamali wadogo na wakubwa hukusanyika pamoja na kuonyesha maonyesho ya bidhaa zao. Pia kila tarehe 07/07(sabasaba) huwa ni siku ya wafanya biashara ambapo wafanyabiashara wakubwa na wadogo hukusanyika pamoja wakionyesha biashara mbalimbali nyingine kutoka mataifa ya ughaibuni na nyingine kutoka mataifa jirani. Nia na madhumuni ya maonyesho hayo ni kukutanisha wanunuzi,wauzaji na watengenezaji bidhaa kuonyesha jinsi ambavyo bidhaa flani inatengenezwa kwa ubora fulani.Ninakushauri wewe unayesoma makala hii kuhudhuria maonyesho hayo ili uweze kujifunza mengi.

4. MALALAMIKO.

Kumekuwa na malalamiko mengi kwenyemaofisi mengi hasa ya serikali,watu wamekuwa waoga kufuatilia haki zao kwa sababu hawazijui sheria na kwa sababu watu wengi wamenyimwa elimu ya uraia na kujitambua. Unaweza ukatumia fulsa hii kufuatilia haki za watu hawa ambapo utaingia nao mkataba wa kukulipa kiasi fulani cha pesa pindi utakapofanikisha.Mfano huko vijijini kuna migogoro mingi ya mipaka ya mashamba,wewe uliye na elimu tena una shahada ya sheria unabaki mjini kusubili ajira mwaka wa tano sasa nakushauri tumia elimu yako kuwasaidia watu hawa.Unaweza kwenda vijijini ukafungua kampuni ya uwakili ambapo utatoa huduma hiyo ambayo itakupatia kipato kikubwa na chenji inarudi.Asanteni sana nawatakia safari njema ya mafanikio.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni