Jumatatu, 9 Mei 2016

 JE UNAIJUA SAKOLOJIA YA MWENZI WAKO?

                             

Watu wengi wamekuwa wakiishi na wapenzi wao kwa muda mfupi na kuachana.Wengine wamekuwa wakibadilisha wapenzi kila kukicha hali ambayo ni hatari kwa afya zao.

Katika tafit zilizofanywa na mwandishi wa makala haya amegundua kuwa, wengi wao wamekuwa wakikosa elimu ya saikolojia ya mapenzi inayohusu kumsoma mpenzi wako jinsi alivyo na kujua njia ya kukabiliana na changamoto za kimapenzi.

Hakuna aliye mkamilifu duniani kila mmoja ana mapungufu yake,hata kama ukiwa na busara sana hali inayopelekea kusikilizwa,kuaminiwa ama kukukubalika katika jamii lakini ujue ya kuwa kuna zimwi la mapungufu ambalo linakutafuna.

Watu wengi wamekuwa wakishangazwa na ndoa ambazo zimekuwa zikifungwa leo baada ya wiki mbili kunakuwa na mizozano na migogoro ndani ya ndoa hali ambayo inapelekea mmoja wao kufungasha vilago.

Mara kwa mara tumekuwa tukisikia sauti za ‘ningejua  nisingeolewa’ ama ‘ningejua nisingeoa’hizi ni sauti ambazo huja baada ya wawili kushindwa kujua saikolojia ya mwenzake.
Changamoto za kujua sakolojia ya mpenzi wako imekuwa ikiumiza ndoa na mahusiano  ya watu wengi,sababu kubwa ya kushindwa kujua saikolojia ya mwenzi wako ni kwa sababu ya kukosa elimu ya kutosha kuhusu saikolojia ya mapenzi.

Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini watu wengi wamekuwa na mtandao wa mapenzi?Ama ni kwa nini kumekuwa na  migogoro ya mara kwa mara ya kimapenzi?
Ukweli ni kwamba watu wamekuwa wakijiingiza katika mapenzi bila kujiandaa,napozungumzia kujiandaa sina maana ya kupiga zoezi la kama wacheza mpira ama ndondi la hasha.

Nina maana ya kuchukua jukumu a kusoma vitabu,makala ama kuangalia filamu mbalimbali zinazohusu mapenzi vinavyozungumzia mapenzi na jinsi ya kuishi na watu mbalimbali walio na tabia/hulka tofauti.

Kumbuka kuwa watu tumeumbwa na hulka mbalimbali,lakini wengi wetu wamekuwa wakilazimissha kubadili tabia zao kwa kufuata mkumbo wa marafiki ama makundi mbalimbali ya watu
         Katika mfululizo wa makala haya,nitakuletea tabia/haiba mbalimbali za wanadamu na jinsi ya kukabiriana nazo mfano:: kuishi na mchumba mpole,muongeaji,mlopokaji,mkali n.k uskose kuitembelea blog hii.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni