Alhamisi, 4 Mei 2017
BABA USINITOE KAFARA KWA FREEMASON
Maisha ya nyumbani yalibadilika ghafla,yalikuwa ni maisha mazuri ambayo yalifanana kabisa na maisha ya kuzimu,vizimbao na matanuzi ya hapa na pale yalitawala maisha yetu ambapo kila mwaka tulikuwa tunachagua sehemu ya kwenda kupumzika.
Baba yangu alikuwa ni tajiri wa kutupwa na alikuwa akizidi kupata pesa nyingi ambazo hatukujua zilikuwa zinatoka wapi.Maswali mengi tulijiuliza vichwani mwetu
“Je ni kile kibanda cha kuchomea chipsi ndicho kinachomwingizia baba pesa nyingi kiasi hiki hali ambayo amekuwa ni tajiri wa kutisha kiasi hiki?”
Kwa kuwa nilikuwa ni mdogo sikuwaza wala kuthubutu kuuliza uhalali wa baba kumiliki pesa mali hizo nyingi.Maisha yetu yalikuwa ni ya kula baga,pizza na kutembelea magari ya kifahari.
Baba aliweza kuchinja ng’ombe kila ijumaa ya mwisho wa mwezi lakini akija mgeni asichinjiwe hata kuku.Hakuna aliyekuwa akijua siri nzito aliyokuwanayo baba yangu ambaye aliitwa kwa jina linalopendwa na watu wengi duniani ‘Mapesa’.
Cha kushangaza kila alipotaka kuchinga Ng’ombe alitufukuza nyumbani ama alitupa pesa kwa ajiri ya kwenda kubarizi ufukweni au kuingia katika kumbi za starehe.Alikuwa akibaki yeye peke yake nyumbani hata mama pia alimficha.
Kila ijumaa ya mwisho wa mwezi tulikuta nyama nyingi na ngozi ya ng’ombe ambayo hugawia maskini,makanisani na misikitini huku bila ya kuibakisha hata mnofu mmoja kwa ajiri ya nyumbani.Mara nyingi alipokuwa akichinja ng’ombe alikuwa akiagiza nyama nyingine kutoka buchani kwa ajiri ya matumizi ya nyumbani.
Alikuwa akipokelea mkono wa kushoto unapompatia pesa ama anapotoa pesa ,alikuwa akiutumia mkono wa kushoto katika kubeba begi lenye pesa na kuchukua ama kuvuata droo iliyokuwa na pesa.
Ngoja nikumegulie siri kidogo,mkono wa kushoto ni mkono autumiao shetani katika kutimiza haja zao,Luthifa ambaye ndiye mkuu wa freemasoni anatumia mkono wa kushoto katiaka kuwaapisha ama kupokea kitu..haya endelea kutililika.
Siku ya kuchinja ng’ombe alikuwa anavaa suti nyeusi iliyotengenezwa kwa madini ya ajabu ambayo sijawahi kuyaoni,na kuifanya suti hiyo kung’ra kuliko kitu chochote duniani.Pete aliyokuwa anavaa siku hiyo ilikuwa ni pete ya ajabu ambayo ilikuwa na alama ya fuvu na joka kubwa ambalo lilifanana na samaki aina ya pweza.
Pia alikuwa na cheni ya shingoni ambayo ilikuwa nakila aina ya madini na ailiyokuwa iking’ara katika kiza na iliyokuwa na chata ya vidole viwili.Kila alipokuwa akizungumza na watu alikuwa akishika kimoja kati ya hivyo.
Katika uchunguzi wangu wa kila siku kuhusu baba sikuwahi kumuona amevaa nguo ya ndani(chupi)hata kwa bahati mbaya.Heee….najua utaujiuliza nilikuwa namuona vipi.
Baba alikuwa na umbo kubwa hivyo kutokana na umbo lake ilikuwa ni virahisi kujua kama alikua amevaa kitu ama la.
Hakuna aliyekuwa akijua hata mmoja hali hizo kwani nyumbani walichukulia kama alikuwa mtu ambaye alipenda urembo na anayependa kuwasaidia watu wa hali ya chini hasa misikitni na makanisani.
Watu wengi walikuwa wakimjua kuwa alikuwa ni kijana mwenye roho nzuri aliyekuwa na kila aina ya huruma,mwenye kupenda watu na aliyekuwa akisaidia kwa hali na mali tena bila kinyongo chochote.
Baba alikuwa ni mtu mpole, mcheshi aliyependa kulinda heshima yake kwa kuwapa watu salamu za upendo na amani.Alikubalika kila alipokanyaga ama aliposimama kuzungumza watu walimkubali na kumuona kuwa ni mtu mwenye hekima na busara.
Baba alikuwa ni kijana ambaye alikuwa jasiri mwenye tamaa na pesa na aliweza kufanya lolote lile kwa ajiri ya kupata pesa.Ili kuthibitisha hayo msomaji tililika na ukurasa huu usifikiri nakupiga kabobo.
Siku moja tukiwa sebureni tunaangalia kituo kimoja cha Televisheni mtangazaji wa zamu alitangaza tukio la vifo vya maalbino wawili huko mkoani Shinyanga hali ambayo watu wote tulikuwa kimya tukisikiliza habari hiyo,lakini ilisikika sauti ya baba ikisema
“Aaa hivi unafikiri ningekuwa mimi ni mlemavu wa ngozi(albino)ningejikata mkono ili wanipe changu niendeleze maisha.”
Sauti hii iligonga kingo za kichwa changu na kujikuta nikimtizama baba kwa jicho la kufikilia mengi juu yake na nilipiga picha na kugundua kuwa Kama anashindwa kujihurumia mwenyewe je atamhurumia vipi mtu mwingine.
Ngoja nikupe angalizo kidogo msomaji….watu kama hawa hawaoni hatari kutoa kafara mama,baba,mtoto hata mkewe.Angalia usije ukaachana na mmeo kwa sababu ya kalamu yangu cha kuzingatia fanya uchunguzi wa kutosha.
Kwa kuwa nilikuwa ni mchunguzi sana wa mambo mbalimbali ambayo baba alikuwa akiyafanya niliweza kugundua mengi juu ya siri ambayo alikuwanayo.
Nyumbani kulikuwa na nyumba tatu ambapo kulikuwa na nyumba moja kwa ajiri ya familia,nyumba hii ilikuwa na vyumba saba na sebule mbili,sebule ya kwanza ilikuwa ni sebure ambayo tuliitumia sisi.
Sebure ya pili ilikuwa ni sebure ambayo wageni wa kawaida walipumzika kama ndugu jamaa na marafiki,pembeni ya sebure hii kulikuwa na chumba cha kujisomea ambacho kilikuwa kimesheheni vitabu na kompyuta.
Pembeni ya chumba hiki kulikuwa na chumba kimoja kikubwa ambacho kilikuwa kimesheheni kila aina ya starehe kama,bwawa la kuogelea,baa yenye kila kinywaji,video ya kuchezea gemu, sehemu zote zilijaa viyoyozi hali ambayo joto la Dar es salaamu lilikuwa ni hadithi kwetu.
Nyumba ya pili ilikuwa ni nyumba ambayo baba na mama walikuwa wakilala,nyumba hii ilikuwa ni ya vioo,haikujengwa kwa tofali wala simenti,ilikuwa na umbo la uyoga Hakika ilipendeza kwa kila aliyeitizama. Nini kitaendelea tembelea Blog hii ili kujua yatakayojiri.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni