ILIPOISHIA :-
Hakuna aliyekuwa akijua hata mmoja hali hizo kwani nyumbani walichukulia kama alikuwa mtu ambaye alipenda urembo na anayependa kuwasaidia watu wa hali ya chini hasa misikitni na makanisani.
ENDELEA
Watu wengi walimjua kuwa ni kijana mwenye roho nzuri aliyekuwa na kila aina ya huruma,mwenye kupenda watu na aliyekuwa akisaidia kwa hali na mali tena bila kinyongo chochote.
Baba alikuwa ni mtu mpole aliyekuwa mcheshi na aliyependa kulinda heshima yake kwa kuwapa watu salamu za upendo na amani.Alikuwa anakubalika kila alipokanyaga ama aliposimama kuzungumza, watu walimkubali na kumuona kuwa ni mtu mwenye hekima na busara, ni kijana ambaye a jasiri mwenye tama na pesa na aliweza kufanya lolote lile kwa ajiri ya kupata pesa.Ili kuthibitisha hayo msomaji tililika na ukurasa huu usifikiri nakupiga kabobo.
Siku moja tukiwa sebureni tunaangalia kituo kimoja cha Televisheni, mtangazaji wa zamu alitangaza tukio la vifo vya maalbino wawili huko mkoani Shinyanga hali ambayo watu wote tulikuwa kimya tukisikiliza habari hiyo iliyotikisa mtima wa kila mtanzania mpenda amani,lakini ilisikika sauti ya baba ikisema
“Aaa hivi unafikiri ningekuwa mimi ni mlemavu wa ngozi(albino)ningejikata mkono ili wanipe changu niendeleze maisha.”
Sauti hii iligonga kingo zaubongo wangu na kujikuta nikimtizama baba kwa jicho la kufikilia mengi juu yake,nilipiga picha ya kifikra na kugundua kuwa, Kama anashindwa kujihurumia mwenyewe je atamhurumia vipi mtu mwingine.
Ngoja nikupe angalizo kidogo msomaji….watu kama hawa hawaoni hatari kutoa kafara mama,baba,mtoto hata mkewe.Angalia usije ukaachana na mmeo kwa sababu ya kalamu yangu.
Kwa kuwa nilikuwa ni mchunguzi sana wa mambo mbalimbali ambayo baba alikuwa akiyafanya niliweza kugundua mengi juu ya siri ambayo alikuwanayo.
Nyumbani kulikuwa na nyumba tatu ambapo kulikuwa na nyumba moja kwa ajiri ya familia,nyumba hii ilikuwa na vyumba saba na sebule mbili,sebule ya kwanza ilikuwa ni sebure ambayo tuliitumia sisi (watoto).
Sebure ya pili ilikuwa ni sebure ambayo wageni wa kawaida walipumzika kama ndugu jamaa na marafiki,pembeni ya sebure hii kulikuwa na chumba cha kujisomea ambacho kilikuwa kimesheheni vitabu na kompyuta.
Pembezoni mwa chumba hiki kulikuwa na chumba kimoja kikubwa ambacho kikuwa kimesheheni kila aina ya starehe kama,bwawa la kuogelea,baa yenye kila kinywaji,video ya kuchezea gemu, sehemu zote zilijaa viyoyozi hali ambayo joto la Dar es salaamu lilikuwa ni hadithi kwetu.
Nyumba ya pili ilikuwa ni nyumba ambayo baba na mama walikuwa wakilala,nyumba hii ilikuwa ni ya vioo,haikujengwa kwa tofali wala simenti,ilikuwa na umbo la bikali Hakika ilipendeza kwa kila aliyeitizama.
Nyumba nyingine ilikuwa ni nyumba ya chini ambayo baba alikuwa amezuia mtu yeyote kuingia katika nyumba hii na baathi ya vyumba vilikuwa vimefungwa na funguo alikuwanayo mwenyewe.Katika lifti ya nyumba hii kulikuwa na alama ya nyoka na alama ya fuvu la kichwa.Namba za siri za kuingia katika lifti hii zilikuwa ni 666.
Namba hii 666 ni namba ya mpinga kristo ambayo ni namba inayotumiwa na freemasoni kuteka dunia kabla ya yesu kurudi mara ya pili.Haya nafikiri umenielewa manake ulishafikiri kuwa ni namba ya simu.
Ndani ya chumba hicho kulikuwa na alama mbalimbali ambazo wakati huo sikuzijua maana yake,si mimi tu hata mama,kaka wadogo zangu hawakuzijua.Tulizitizama alama hizo na kuziona kama mapambo mazuri yaliyonakshi kuta.
Pembeni ya chumba ambacho kilikuwa hakifunguliwi kulikuwa na viti viwili,na katikati ya viti hivyo kuliachanishwa na meza ambayo ilikuwa na alama zilizofanana na za ukutani zilizokuwa zimepangwa kwa ustadi mkubwa na kuifanya meza hiyo kupendeza vilivyo.
Katika chumba hiki kulikuwa na hewa nzuri kwan kulikuwa na mitambo maalumu ya kuingiza na kutoa hewa,chumba hiki kilikuwa kinatumika kwa wageni maalumu ambao baba alikuwa akiwapokea kutoka ndani na nje ya nchi.
Ndani ya chumba hiki kulikuwa na kifaa maalumu cha kusafisha nyumba,Chombo hiki kilifungwa na mafundi kutoka ujerumani.
Ngoja nikupe dondoo fupi kuhusu nyumba hii,ujenzi wa nyumba hii ilijengwa na mafundi kutoka Marekani,Afrika ya kusini na Nigeria.Mafundi hawa walijenga kwa awamu lakini cha kushangaza kila walipotaka kumalizia kujenga mmoja wao alifariki dunia kwa kupigwa na kitu kichwani ama kubanwa ama homa ya ghafla.Hiyo ndio historia fupi ya nyumba hii.
MDOGO WANGU KUTOLEWA KAFARA
Ilikuwa ni siku ya tatu ya juma ya mwezi wa 04 mwaka 2014 kabla ya sikukuu ya pasaka kufika,baba alitukalisha kikao cha familia ambapo tulizungumzia kuhusu kwenda kutalii katika moja ya mbuga za wanyama nchini Tanzania.
Ma zungumzo yetu yalikuwa na kila aina ya mabishano kwani baadhi yetu hawakutaka kwenda katika mbuga ambayo baba alikuwa akiitaja.Hali hii ilisababisha kuzua mtafaruko katika kikao hicho na kusababisha baba kutumia fimbo ya ukuu wa familia kulazimisha kukubali matakwa yake.
Hakuna aliyeweza kuzungumza tena baada ya baba kutoa tamko hilo ambapo aliamua kwenda kutembelea mbuga za wanyama za Serengeti.Tulipewa sikyu mbili za kujiandaa kwa kununua mavazi maalumu ya kuvaa mbugani na vyakula vya kusindika.
Mimi na wadogo zangu tulichukua gari letu na kwenda super market kufanya shoping hiyo,nyumbani kulikuwa na gari la baba,mama na magari mawili kwa ajiri ya watoto.
Baada ya kumaliza kufanya maandalizi hayo tulijiandaa kwa safari huku tukiwa na shangwe ya kwenda kuwaona sImba,Twiga na wanyamapori wengine.
Siku iliyofuata baba alipeleka gari lake kwa ajiri ya kufanyiwa matengenezo madogo madogo kwa kuliweka sawa na safari.Baba alirudi nyumbani,siku hiyo ilikuwa ni siku ya kipekee kwani baada ya kurudi nyumbani alifanya vitu viofuatavyo.
Aliingia katika nyumba ile ya chini na alikaa zaidi ya masaa mawili,sikuweza kujua kwa haraka alikuwa akifanya nini lakini ilinilazimu niingie ndani ya chumba hicho ili kukamilisha utafiti wangu.
Niliingia katika chumba cha liftio na kubofya 666 kisha lifti hiyo ilishuka chini na kunifikisha chini,nuilishuka na kuanza kupIga hatua kwa kunyata nikielekea katika chumba ambacho kilikuwa kinafungwa muda wote lakini wakati huo kilikuwa kimefunguliwa.
Hali ya nyumba ilikuwa kimya hali ya kwamba hata kama ukitoa pumzi ilisikika,nilisogea taratibu katika chumba hicho,mlango wa chumba hicho ulikuwa umeegesha huku ukiacha mpenyo mdogo ambao nilipitisha jicho langu na kutizama.
Nilimuona baba akiwa amevalia suti yake nyeusi ambayo ilikuwa iking’ara kama nyota ya mashariki,mkono wa kushoto alikuwa ameshikilia kitabu ambacho kilikuwa kimezungushiwa madini mbalimbali yaliyo na alama mbalimbali za mafuvu,vidole,nyoka na alama iliyofanana na umbo pweza.
Akiwa amekaza uso alikuwa akizungumza maneno ambayo sikuweza kuyang’amua mara moja lakini nilisikia neno la mwisho akimtaja mdogo wangu wa mwisho Chimo,kengere ya hatari ililia katika kichwa changu nilishindwa kuelewa mara moja kuhusu alichokuwa akikifanya.
Niliendelea kumtizama baba aliyekuwa akizungumza kwa hisia kali huku akiwa amefumba macho yake,ghafla nywele zangu zilisisimka na ubongo wangu ukapata taarifa kuwa kulikuwa kuna kitu kibaya kiliingia ndani.
Nilipiga moyo konde na kusema kuwa
“Nitaangalia mwanzo mpaka mwisho wa tukio hili”
Niliendelea kutizama tena kwa makini lakini nilishtuka nilipoona rangi ya taa hafifu zilizokuwa zikimulika ndani zikififia na kuwaka mwanga mkali ambao ulikuwa ukiwaka mfano wa radi,hali ambayo ilinifanya niumie macho na kushindwa kuona vizuri.
Nilitoa uso wangu katika kipenyo kile na kutizama kwingine…Haaa…!!!nilishangaa kuona nyumba yoye ilikuwa ikiwaka mwanga ambao nuilishindwa kuelewA ulikuwa ukitoka katika chanzo gain.
Nilianza kuutafuta mlango wa kutokea ambapo,nilishika lifti na kuingia kisha ilinitoa nje,ilikuwa imetimu saa sita usiku.Baada ya kutoka,nilielekea ndani na kuwakuta mama na wadogo zangu wawili wakijiuliza kuhusu kutoweka kwangu usiku huo.
Mama aliamini kuwa nilitoka na baba lakini wadogo zangu walikataa na kusema kuwa waliniona nikitoka peke yanu,nilishangaa sana kusikia kuwa hata mama hakujua baba alikoelekkea.
Nini kitaendelea endelea kufuatilia hadithi hii ya kusisimua.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni