Jumapili, 29 Mei 2016

SIRI YA MAFANIKIO

Mafanikio ni matokeo mazuri ya jambo ambalo unalifanya,mafanikio yanaweza kuwa ya kimwili au kiroho.

Ukweli ni kuwa siri ya mafanikio anayo yule aliyefanikiwa,hakuna aliye na mafanikio makubwa bila ya kupitia siri ambazo nitazielezea.Shauku ya moyo wa mwanadamu ni kufanikiwa katika kila jambo alifanyalo,nilipokutana na mwandishi wa vitabu bwana  Errick Shigongo alinieleza baadhi ya siri za mafanikio ambazo mpaka leo naishi nazo,nalala nazo na ninatekeleza kila kukicha.

Ninakushauri na wewe msomaji wangu tenga siku moja mtembelee mtu yeyote ambaye anajihusisha na kipaji chako,fani yako,utaalamu wako huyo ndio atakuwa mfano wa kuigwa katika maisha yako,ikiwezekana muombe awe mlezi wa maisha/uchumi wako.

Hii itakupa hamasa wewe katika harakati za kufikia malengo yako kwa sababu utakuwa na mlezi ambaye tayari ameshafanikiwa katika maisha yake.Unapokutana nae usiogope kumuuliza swali lolote lile kuhusu mafanikio ila zingatia usiingilie maisha yake binafsi.

Zifuatazo ni siri za mafanikio ambazo ukizifuata hakika utatoka hapo ulipo na kusogea karibu na mti wa mafanikio.

1.   JIAMINI MWENYEWE

Hii ni siri kubwa ambayo watu wengi hawana,wengi wamekuwa waoga kuanzisha kitu fulani ambacho unakiamini kuwa kitaweza kukuletea matokeo chanya katika maisha yako.Usifikirie wala usijali maneno ya watu ambayo yanakukatisha tamaa,fanya bila kujali watu watazungumza nini juu yako.

Jaribu kujilinganisha na mtu wako wa kuigwa na jenga picha katika akili yako jinsi ambavyo unavyotaka kuwa.Mfano unataka kufungua kampuni kubwa,tengeneza picha ya kampuni hiyo katika akili yako kwanza,jaribu kujiona kuwa wewe ndio mkurugenzi wa kampuni hiyo,siku zote mafanikio huanzia kwenye ndoto.

2.        JIFUNZE KILA SIKU.

Wahenga walisema "Elimu haina mwisho",msemo huu unaenda sambamba na siri ya mafanikio kwani ni lazima uwe mtu wa kujifunza kila siku kupitia vitabu,magazeti na mitandao ya kijamii.Hakuna aliyeweza kufanikiwa pasipo kujifunza kwa kusoma,kuhudhuria semina za ujasiliamali au kubadilisha mawazo/uzoefu wa jambo fulani.

3.       FANYA PASIPO KAWAIDA

Watu wamezoea kufanya mambo kawaida,hasa kuiga kutoka kwa mtu fulani,kampuni fulani,shirika fulani.
Jaribu kuwa mbunifu katika biashara yako au kazi yako,mafanikio makubwa huletwa na ubunifu.Usijali maneno ya watu juu ya kile unachotaka kukifanya songa mbele huku ukitazama malengo yako uliyojiwekea.

4          USIOGOPE KUSHINDWA

Ukiamua kufanya jambo ambalo liko katika malengo yako ujue ya kuwa kushindwa kuko mbele yako,unaweza ukakutana na vikwazo vingi ambavyo vitakukatisha tamaa usiogope,hata kama ukianguka simama pukuta mavumbi na kusonga mbele kumbuka ya kuwa huwezi kuwa mshindi siku zote.Kumbuka bila ya maumivu hakuna mafanikio.

Ukiogopa kushindwa ujue ya kuwa huwezi kujisimamia/kujiendesha mwenyewe, ujue ya kuwa unajiendesha mwenyewe kwa sababu unaamini katika ndoto zako na unaamini kuwa upo sahihi kwa kila unalolifanya na unaamini mafanikio yatakuja.*USIWE NA WASIWASI WA KUSHINDWA*

5.        USISIKILIZE KWA WALIOSHINDWA

Ni mara ngapi umesikia  huwezi kufanya hili,huwezi kufanya vile kwa sababu haijawahi kufanywa?Ni mara ngapi umesikia huwezi kufanya hili kwa sababu mimi nilishindwa/mtu flani alishindwa?Binafsi napenda kuambiwa hivyo ili niwe wa kwanza kufanya na kuwaaminisha watu kuwa  kitu hicho kinawezekana kufanywa.

Mfano nilipokiwa chuoni,marafiki zangu walinibeza na kuniambia kuwa siwezi kuandika kitabu na kukisambaza Tanzania nzima kwa sababu ya ukosefu wa fedha,niliamua kutafuta pesa kwa udi na uvumba,nikawa mwandishi wa kujitolea katika gazeti flani,baada ya miezi 9 nilipata pesa ya kuchapisha kitabu cha kwanza kopi 4,000 na kusambaza Tanzania nzima.

6.       FANYA KAZI KWA BIDII

Watu wengi hukosa ufanisi wa kazi zao kwa kushindwa kufanya kazi kwa bidii,amka asubuhi na mapema ikiwezekana saa 11 alfajili  hii itakusaidia wewe kupanga siku yako vizuri,anza na mambo ambayo wewe umejiwekea kuyafanya kila siku Mfano.

Mimi kila siku asubuhi naandika kurasa mbili za hadithi kisha naendelea na shughuli zingine,hii inanisaidia kuendeleza kipaji changu na kuweza kufikiri zaidi.

Hata wewe nakushauri kama unaweza jitahidi kila siku asubuhi tunga na uandike ujumbe mfupi wa maneno wa kutiana moyo tuma kwenye group la whatsap au mtumie rafiki yako hii itaksaidia sana.

7.         SAIDIA WATU

Kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali ni kitu kizuri katika maisha ya kila siku,msaada hukuwezesha wewe kufungua milango yako ya mafanikio,sio lazima kusaidia kwa kutoa pesa unaweza kusaidia watu kwa kuwashauri vizuri,kuandika makala nzuri kama hii au kuwatamkia maneno mazuri ya kuwatia moyo na kuwa bariki "UMEBARIKIWA MKONO UTOAO KULIKO UPOKEAO".Usikose kutembelea blog hii kila siku utapata mambo mapya na mazuri yenye kukujenga kisaikolojia na kiuchumi.Ni mimi Bundala Izengo kocha mzoefu.0656669989


Jumatano, 25 Mei 2016

Je wajua Kwa nini Tunakosa Uvumilivu?

  Uvumilivu ni hali ya kustahimili machungu.(Maana hii kutokana na kamusi ya Kiswahili sanifu)
Lakini tunaweza kusema uvumilivu ni hali ya kuhimili matatizo mbalimbali yanayotukumba katika maisha yetu ya kila siku.

Kuna sababu kedekede ambazo zinaelezwa kuwa ni chanzo cha kukosa uvumilivu.Katika makala haya nimekuandalia baadhi ya sababu hizo.Kukosa uvumilivu inaweza kusababisha kukosa maadili kazini kwa kuiba,rushwa na ufisadi.Mwandishi wa makala haya ameorodhesha baadhi ya sababu ambazo zinaelezea sababu ya kukosa Uvumilivu.
(1)Mfumo tuliolelewa.

Malezi tuliyolelewa pindi tukiwa watoto wadogo hayakutufunza kuvumilia katika shida,njaa na mateso.,Mfano utakuta mzazi yuko tayari kukopa chipsi ya mtoto wake sio kwa sababu Ana njaa,La hasha bali kwa kuwa amelilia kwa tamaa ya kumuona Fulani anakula ama anataka kuwadolishia wenzake.

Maisha haya yamekuwa yakijenga mazoea mabaya kwa  watoto wetu,pia yanaweza kusababisha watoto wetu kujifunza wizi pindi unapokosa pesa ya kununulia hitaji lake ambalo sio la lazima.(sina maana watoto wasinunuliwe chipsi)

(2)Ukosefu wa elimu

Elimu ni mafunzo ambayo yatolewayo kwa mwanadamu ama mnyama katika kujifunza kitu.Wanadamu tumekuwa tukipata elimu kila kukicha  na waswahili wanasema elimu haina….(mwisho)

Wengi wetu tumekalili kuwa elimu inatolewa darasani tu,hali ambayo watu wamekuwa wagumu kupokea mapokea mapya kwa tabia  ya kujifunza.Elimu hutolewa popote pale chini ya mti nyumbani kwako,kanisana hata misikitini na kazini kwako.

Takwimu zinaonyesha kuwa watanzania wengi ni wavivu wa kusoma vitabu,hali ambayo inawasababisha kukosa elimu kwa njia ya vitabu ambapo ni elimu yenye mafunzo mengi zaidi.

Kukosa elimu kunaweza kumsababisha mtu kuwa na uwezo mdogo wa kupambanua mambo,wengi wetu tumekuwa tukifikilia kufanya maamuzi yasiyofaa kwa sababu ya kukosa elimu ya jambo fulani.

(3)Kutaka mafanikio ya haraka.

Wanadamu tumeumbwa na shauku ya kutaka mafanikio kwa haraka,wengi wetu tumekuwa tukijaribu kupitia njia za panya(mkato) ili kuharakisha kufanikiwa kwa kupata kazi,mchumba,mtaji na mambo mengine yafananayo na hayo.

Tumesahau kuwa ‘haraka haraka haina baraka’tumekuwa tukijaribu kuharakisha kutengeneza maisha mazuri kwa kutoa rushwa ya pesa ama ngono bila kujari kuwa unafanya kosa la jinai na ni hatari kwa afya yako.

Haraka ya mambo wengi huja kujutia,nimeshuhudia rafiki zangu wawili walioajiriwa katika wizara fulani wakifukuzwa kazi kwa sababu ya taaluma zao zilikuwa kinyume na ajira walizokuwanazo.

Mfano.Taaluma yako ni uandishi wa habari,unafanya kazi ya uhasibu kwa sababu mkuu wa kitengo fulani ni ndugu yako.Hesabu na kuandika habari wapi na wapi.

Hata katika mahusiano wengi wamekuwa wakitaka kufanya tendo la ndoa kabla ya kupata baraka kutoka kwa wachungaji,mashehe,wazazi na matokeo yake wanapeana miba na kukimbiana huku wakisema“Ningejua nisingefanya hili”mara nyingi msemo huu huja yalishatokea hivyo ni bora ubadilike sasa,uwe na uvumilivu utafanikiwa katika jambo lako (mvumilivu hula mbivu) ni mimi kocha wako Bundala Izengo kesho tutaangalia madhara yatokanayo na kukosa uvumilivu.

Msomaji wa blog hii makala hii ya leo na kesho nakujenga kisaikolojia ili tuingie kwenye makala ambayo nimekusudia kukuletea katika mfululizo wa makala zangu najua ukinifuatilia vizuri utakuwa mfanya biashara mkubwa,mfanya kazi bora.Nakutakieni SIKU NJEMA MUNGU AWE NANYI KATIKA KAZI ZAKO.


Jumanne, 24 Mei 2016

WILLIAN WA CHELSEA ANENA


Kiungo wa Chelsea Willian amesema mashabiki wa klabu hiyo wanahitaji matokeo mazuri zaidi baada ya timu hiyo kumaliza nafasi ya 10 Ligi Kuu Uingereza.

FALSAFA YA  HAPA KAZI TU NI CHACHU YA MAENDELEO

                                 

Ikiwa ni miezi kadhaa tangu Falsafa ya HAPA KAZI TU kusikika katika masikio  ya watanzania,watu wengi wamehamasika na kujituma katika kufanya kazi.Ni ukweli usiopingika kuwa bila ya kufanya kazi kwa bidii hakuna maendeleo,msemo huu unaenda sambamba na maandiko matakatifu yasemayo ASIYEFANYA KAZI NA ASILE.

Ujio wa falsafa hii umekuwa ukileta chachu kwa wafanyakazi waajiliwa na waliojiajili kufanya kazi kwa bidiii,nguvu zaidi na umakini mkubwa.Katika miaka ya 1990-2015 watanzania wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea hali ambayo iliwafanya kujisahau na kuhisi kuwa huo ndio mtindo wa maishi unaofanyika hapa duniani.

Katika nchi zilizoendelea serikali,makampuni na taasisi mbalimbali zinafanya kazi usiku na mchana na sababu ambayo inaleta matokeo chanya katika uchumi wao.Utafiti wa bwana Wang Qi mhitimu wa chuo kikuu nchini china alitafiti jinsi ambavyo china inavyofanya kazi kwa muda wa masaa 2,200 kwa mwaka akilinganisha na wananchi wa nchi za United Kingdom (UK) wanaofanya kazi kwamuda wa masaa 1,677 Ripoti hii imechwapwa katika gazeti la kila siku la The Gurdian nchini marekeni.

Hapa nchini Tanzania mtanzania mmoja amekuwa akifanya kazi kwa muda wamasaa 8 kwa siku ambayo ni sawa na masaa 176 kwa mwezi,kila mfanyakazi kwa mwaka huchukua likizo ya mwezi mmoja,na ukihesabu sherehe za tanzania mfanyakazi mmoja anapumzika mwezi mmoja kwa mwaka hivyo wafanyakazi wa Tz hupumzika miezi miwili kwa mwaka bila kuhesabu J.Mosi na J.Pili.Hivyo basi kila Mfanyakazi mmoja anafanya kazi kwa muda wa masaa 1760 kwa mwaka.

Katika falsafa hii inaongeza hali ya utendaji wa wafanyakazi  na kuwakumbusha wafanyakazi wazembe kuwa wanahitajika kufanya kazi kwa bidii na kuacha mazoea ambayo walikuwa nayo ili kuleta tija na kusukuma gurudumu la maendeleo kwa kasi zaidi.
Sisi kama vijana wa Tanzania tunatakiwa kuwa chachu ya maendeleo ya taifa letu,familia zetu na ndugu kwani kazi ndio msingi wa maendeleo ya taifa lolote duniani.Tembelea blog hii kila siku utapata vitu vipya.

Jumapili, 22 Mei 2016

                                  JINSI YA KUPATA WAZO ZURI LA BIASHARA


Kumekuwa na maswali mengi ambayo nimekuwa nikiulizwa na marafiki zangu juu ya kupata wazo zuri la biashara.Kutokana na takwimu za shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP kuna biashara 4,000  ambazo hubuniwa kila siku,kati ya biashara hizo ni biashara 1740 ambazo huleta matokeo chanya,biashara 2260 huleta matokeo hasi kwa sababu ya kukosa ubunifu au kuwa na wazo baya la biashara.Kabla ya kuendelea tuangalie maana ya maneno yafuatayo.
WAZO LA BIASHARA:Hili ni jambo linalofikiriwa na mtu ili aweze kununua,kuuza au kuchuuza bidhaa fulani kwa nia ya kupata faida.

                          HATUA MUHIMU NNE ZA KUTENGENEZA WAZO LA BIASHARA

1. UJUZI/UZOEFU WOWOTE                            

Chukua karamu na karatasi orodhesha changamoto zinazoikumba jamii uliyonayo jaribu kuhusisha na ujuzi au uzoefu ulionao.Mfano mtaani kwako kuna tatizo la wizi wa kupora au wa kuvunja milango,anzisha kikundi cha ulinzi shirikishi chenye watu wasiopungua 15,nenda serikal za mtaa waeleze nia na madhumuni ya kuanzisha kikundi,wasilisha wazo lako kituo kikuu cha polisi kilichopo karibu yako ili usajili kikundi kile kitambulike kisheria,wekeni sheria ndogondogo ambazo zitawabana watuhumiwa mtakao wakamata walipe faini na faini zile zitaingia kwenye kikundi,wasilisha mswada wa sheria kwenye kamati ya ulinzi ya serikali ya mtaa/kijiji ili itengenezwe sheria ndogondogo  ambapo kila kaya watachangia Tsh. 1000 kila mwezi kwa ajili ya ulinzi shirikishi,hapo utakuwa umejitengenezea ajira na umetengeneza ajira kwa wengine.

2. KIPAJI CHAKO NI KIPI?

Nikiwa katika mazungumzo na vijana hapa mtaani nilishangazwa na kijana mmoja ambae alisema kuwa hajui kipaji chake.Suala hili lilinizibua fikra zangu na kuona kuwa kuna haja ya kufanya utafiti mdogo kwa kuwahoji vijana kumi.Kati ya vijana hao vijana 2 tu ndio walikuwa wanajua vizuri vipaji vyao na jinsi ya kuvitumia ili kuwapatia kipato,vijana 5 hawajui kabisa  vipaji vyao na vijana 3 walikuwa wanajua vipaji vyao lakini hawajui jinsi ya kuvitumia ili kuwapatia kipato. Hii ilikuwa ni changamoto kwangu,kuwaelimisha kujua vipaji vyao na jinsi ambavyo wanaweza kubadili vipaji vyao kuwa bidhaa na kuwazalishia pesa. Msomaji wa makala haya unaweza kubadili kipaji/ujuzi wako kuwa bidhaa na kukupatia pesa kama hujui tuwasiliane kwa email izengobundala@gmail.com  au whatsap 0656669989

3. HUDHURIA MAONYESHO YA BIASHARA

Kila tarehe 8/08/kila mwaka huwa ni siku ya wakulima kitaifa maarufu kama nanenane,watu binafsi,makampuni mbalimbali,wajasiliamali wadogo na wakubwa hukusanyika pamoja na kuonyesha maonyesho ya bidhaa zao. Pia kila tarehe 07/07(sabasaba) huwa ni siku ya wafanya biashara ambapo wafanyabiashara wakubwa na wadogo hukusanyika pamoja wakionyesha biashara mbalimbali nyingine kutoka mataifa ya ughaibuni na nyingine kutoka mataifa jirani. Nia na madhumuni ya maonyesho hayo ni kukutanisha wanunuzi,wauzaji na watengenezaji bidhaa kuonyesha jinsi ambavyo bidhaa flani inatengenezwa kwa ubora fulani.Ninakushauri wewe unayesoma makala hii kuhudhuria maonyesho hayo ili uweze kujifunza mengi.

4. MALALAMIKO.

Kumekuwa na malalamiko mengi kwenyemaofisi mengi hasa ya serikali,watu wamekuwa waoga kufuatilia haki zao kwa sababu hawazijui sheria na kwa sababu watu wengi wamenyimwa elimu ya uraia na kujitambua. Unaweza ukatumia fulsa hii kufuatilia haki za watu hawa ambapo utaingia nao mkataba wa kukulipa kiasi fulani cha pesa pindi utakapofanikisha.Mfano huko vijijini kuna migogoro mingi ya mipaka ya mashamba,wewe uliye na elimu tena una shahada ya sheria unabaki mjini kusubili ajira mwaka wa tano sasa nakushauri tumia elimu yako kuwasaidia watu hawa.Unaweza kwenda vijijini ukafungua kampuni ya uwakili ambapo utatoa huduma hiyo ambayo itakupatia kipato kikubwa na chenji inarudi.Asanteni sana nawatakia safari njema ya mafanikio.

Jumamosi, 21 Mei 2016

JE UNAZIJUA NJIA RAHISI ZA KUPATA MTAJI?


Moja ya changamoto ambazo zinawakumba watu wengi ni upatikanaji wa mtaji.Mtaji ni pesa,amana au wazo ambalo linaweza kuleta faida litumiwapo kwa usahihi.Changamoto za mtaji zimekuwa kilio kikubwa kwa watanzania wengi hasa wahitimu wa vyuo na wasiosoma kabisa.
Mahitaji ya mitaji yamekuwa yakiongezeka  kadri changamoto ya ajira inavyozidi kuitafuna dunia na wahitimu wengi kukosa ajira za moja kwa moja hali ambayo inadhalilisha usomi wao.Tatizo kubwa lililopo Tanzania ni mfumo mbovu wa elimu uliopo ambao hamfundishi mwanafunzi kujiajili bali unamfundisha mwanafunzi kuajiliwa maofisini nk.
                                                    ZIFUATAZO NI NJIA  HALALI ZA KUPATA MTAJI
1.     ANZA KUWEKA AKIBA.

Hiki ni kipenigele muhimu ambacho watanzania wengi hatukitumii,unaweza kuweka akiba kidogokidogo mpaka kitakapotimia malengo yako(kidogo kidogo hujaza.......).Weka akiba kutoka kwenye pesa unazotumiwa na wazazi wako kwa ajili ya matumizi ya shule/chuo.Kanuni ni rahisi sana unaweza ukaamua kuweka Tsh.1000 kila siku ambapo kwa mwezi ukawa na 30,000/= kwa mwaka 300,000/=

2.      UNGANA NA MWENZAKO MWENYE NDOTO KAMA ZAKO.

Hii itakusaidia kubadilishana mawazo jinsi ya kutafuta mtaji na pia huwa ni rahisi sana kwa watu wawili  au zaidi kufanikisha  ndoto zao.Zingatia kuwa wote mlio katika jambo hilo mnakuwa na lengo moja ambalo ni kufika  paleee.Pia ukiungana na wenzako inakuwa ni rahisi kupata mtaji kupitia mikopo ya mabenki,mnaweza kuanzisha sacos kutafuta wadhamini wa wazo lenu n.k

3.        JIUNGE NA MAKAMPUNI YA SIMU

Makampuni ya simu yameweza kutoa ajira millioni moja katika mwaka 2014-2015.Ili kuweza kupata ajira  hii haihitaji gharama kubwa kwani gharama yako itakuwa ni kununua laini  na kuwekewa acces ya usajili ambayo ni bure, kununua simu, pia kununua laini kwa ajili ya kumuuzia mteja.Kazi hii ina faida sana kuliko tunavyofikiria ukimsajili mteja mmoja atakulipa 1,000 palepale,kadri mteja anapoweka vocha na kuitumia ndivyo kamisheni yako inavyozidi kuongezeka.ukisajili wateja 200 kwa mwezi 150 wakaweka vocha ya 500 kila siku,na katika vocha hiyo kuna asilimia 6 unazopewa wewe ambayo ni kama shilingi 60  ambapo 60x150=9000,huyu mtu anaingiza commision ya Tsh. 9,000 kwa siku zidisha mara mwezi 9,000x30= 270,000 na laini hizo utalipwa kiasi hicho kwa muda wa miezi 6.Namaanisha kuwa mwezi wa kwanza ukasajili wateja walio hai 150 ukapata 270,000 mwezi wa pili ukasajili idadi hiyo hiyo utakuwa na jumla ya pesa ya Tsh 540,000 kadri utakavyosajili wateja wengi ndivyo kamisheni yako itapanda.(usiwadharau hao wanatengeneza pesa nzuri ajabu)

4.        UZA AMANA ZAKO

Ili kupata mtaji unaweza ukauza simu ya gharama uliyonayo,tv au kitanda.Hakikisha pesa hiyo unaipeleka kwenye malengo uliyokusudia pia uwe  na usalama wa mtaji wako na uhakika wa soko la bidhaa ambayo utaiuza.
Asanteni sanaa ni mimi kocha wako BUNDALA IZENGO

ASAMOAH ALAMBA SHAVU CHELSEA

Chelsea wametakiwa kutoa kitita cha paundi milioni 25 kumsajili mchezaji wa miamba wa Italia, Kwadwo Asamoah


Alhamisi, 19 Mei 2016

MCHEZO HUU HAUHITAJI HASIRA


HIZI NDIZO NJIA ZA KUPATA WAFANYAKAZI BORA                                                                     

                                                                               

                  Hulka na tabia za watu ni tofauti,waajili na waajiliwa wanatakiwa kuvumiliana kwa mamabo mbalimbali ambayo  yanaweza kuleta fikra hasi kati ya mmoja wa.Si rahisi kwa mwanadamu kuishi bila kukosea ama kufanya kazi bila kukosea.Waajili wengi wamekuwa wakilalamika juu ya wafanyakazi wao kushindwa kufuata maelekezo ambayo wanawapa ili kuleta ufanisi katika biashara/kazi zao.Moja ya changamoto ambazo waajili wengi wanakutana nazo ni kushindwa kutambua changamoto za wafanyakazi wao Jasmini ni mmoja wa waajili ambaye amekuwa akikumbana na changamoto nyingi katika biashara yake.Leo nimekuletea njia mabazo zitakuwezesha kupata wafanyakazi bora


                                 1.KUAJILI WAFANYAKAZ WENYE VIGEZO NA UJUZI:
Uendesshaji wa biashara (hasa ambayo inahitaji mtu aliyesomea kiteengo husika)inahitaji umakini mkubwa kumpata fanyakazi anayefaa.Waajili wengi wamekuwa wakiwaajli watu ambao hawajasomea kazi ile ili aweze kumlipa ujira mdogo.Dada jasmini hii itakula kwako kwani ufanisi wa kazi utakuwa mdgo na wateja watakimbia na biashara kufa kabsaaa.    

                                  2.TENGENEZA UPYA PROGRAME(MFUMO) WA UENDESHAJI  
   
 Hii inahusisha mambo mengi sana,lkini tuzungumzie tu kuwa unahitaji kuwa na mfumo ambao kila mfanyakazi wako ajisikie kama yuko nyumbani (mfumo rafiki) kuwa na tabia ya kutoa pongezi kwa anayefanya vizuri,sherehe za mwisho wa mwaka n.k                                                                                                                                                                                                                                          3:WEKA UTARATIBU RAFIKI KWA WAFANYAKAZI:                

 Kuna wafanyakkaz wengine wana magonjwa mbalimbali na mengine ni siri mfano siku za  hedhi za mwanamke,magonjwa yatokanayo na giographia wafanyakaz kama hao waahitaji kuwa na uangalizi maalumu unaweza kumnunulia koti,peds n.k.                                                                                                                                                                                          
                                 4.TENGENEZA MFUMO WA KUNUSA UHALIFU:          

 Jasmini ukisoma kitabu cha THINK BIG kilichoandikwa na Donalrd Tramp amezungumzia jinsi ambavyo amejiwekea mfumo bora wa kunusa matukio ya uhalifu kabla hayajatokea.Mfano unaweza ukawa umewaajili watu katika kampuni  yako lakini mmoja kati ya hao anataka kufanya uhalifu wa kuiba,kuacha kazi bila taarifa inakubdi pate taarifa haraka ili uweze kuweka mamb sawa.                                                                                                                                                                                                                                                                                                      5.WAAMBUKIZE WAFANYAKAZI WAKO:

 Simaanishi kuwa unawaambukza magonjwa la hasha namaanisha kuwaambukiza endaji wa kazi,ukubali au ukatae utendaji wa wafanyakazi wako unaakisi utendaji wako wa kazi,mfano ukiwa mzembe watakuwa wazembe tu,ukichelewa kufika ofsini watachelewa zaid yako.


JOHN TERRY LULU YA CHELSEA


Chelsea imetangaza kuwa John Terry amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Antonio Conte amefanya uamuzi wa busara kumbakisha John Terry Chelsea baada ya kufikia makubali ya pamoja na bodi kumpa mkataba wa mwaka mmoja.

Jumatatu, 9 Mei 2016

 JE UNAIJUA SAKOLOJIA YA MWENZI WAKO?

                             

Watu wengi wamekuwa wakiishi na wapenzi wao kwa muda mfupi na kuachana.Wengine wamekuwa wakibadilisha wapenzi kila kukicha hali ambayo ni hatari kwa afya zao.

Katika tafit zilizofanywa na mwandishi wa makala haya amegundua kuwa, wengi wao wamekuwa wakikosa elimu ya saikolojia ya mapenzi inayohusu kumsoma mpenzi wako jinsi alivyo na kujua njia ya kukabiliana na changamoto za kimapenzi.

Hakuna aliye mkamilifu duniani kila mmoja ana mapungufu yake,hata kama ukiwa na busara sana hali inayopelekea kusikilizwa,kuaminiwa ama kukukubalika katika jamii lakini ujue ya kuwa kuna zimwi la mapungufu ambalo linakutafuna.

Watu wengi wamekuwa wakishangazwa na ndoa ambazo zimekuwa zikifungwa leo baada ya wiki mbili kunakuwa na mizozano na migogoro ndani ya ndoa hali ambayo inapelekea mmoja wao kufungasha vilago.

Mara kwa mara tumekuwa tukisikia sauti za ‘ningejua  nisingeolewa’ ama ‘ningejua nisingeoa’hizi ni sauti ambazo huja baada ya wawili kushindwa kujua saikolojia ya mwenzake.
Changamoto za kujua sakolojia ya mpenzi wako imekuwa ikiumiza ndoa na mahusiano  ya watu wengi,sababu kubwa ya kushindwa kujua saikolojia ya mwenzi wako ni kwa sababu ya kukosa elimu ya kutosha kuhusu saikolojia ya mapenzi.

Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini watu wengi wamekuwa na mtandao wa mapenzi?Ama ni kwa nini kumekuwa na  migogoro ya mara kwa mara ya kimapenzi?
Ukweli ni kwamba watu wamekuwa wakijiingiza katika mapenzi bila kujiandaa,napozungumzia kujiandaa sina maana ya kupiga zoezi la kama wacheza mpira ama ndondi la hasha.

Nina maana ya kuchukua jukumu a kusoma vitabu,makala ama kuangalia filamu mbalimbali zinazohusu mapenzi vinavyozungumzia mapenzi na jinsi ya kuishi na watu mbalimbali walio na tabia/hulka tofauti.

Kumbuka kuwa watu tumeumbwa na hulka mbalimbali,lakini wengi wetu wamekuwa wakilazimissha kubadili tabia zao kwa kufuata mkumbo wa marafiki ama makundi mbalimbali ya watu
         Katika mfululizo wa makala haya,nitakuletea tabia/haiba mbalimbali za wanadamu na jinsi ya kukabiriana nazo mfano:: kuishi na mchumba mpole,muongeaji,mlopokaji,mkali n.k uskose kuitembelea blog hii.