Alhamisi, 23 Julai 2015
IRINE UWOYA ATUMBUKIA KWENYE SIASA
Mwigizaji nguli wa Bongo Movie Irine Uwoya Ajiingiza kwenye movie ya mchezo mchafu (siasa) Akitarajia kucheza scene kali ya Viti maalumu akishirikiana na mwongoza muvi maarufu sana nchini na Duniani ambaye ni CCM.Kila la kweli dadaa.
KARIBU OBAMA TULE UGALI,SAMAKI NA MAZIWA!
Shamla shamla za kumpokea Raisi wa Marekani Barack Obama zinazidi kushika kasi katika jiji la Nairobi nchini Kenya.Hii ni picha ya vijana wabunifu wenye kipaji cha uchoraji wamebuni picha nzurii kabisa.
Prof tibaijuka azomewa tena kwa mara ya pili
Prof tibaijuka azomewa tena kwa mara ya pili
Aliyekuwa Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna Tibaijuka anayewania jimbo hilo kwa mara ya pili, jana alishushwa jukwaani kwa kuzomewa na wanachama wake katika kata ya Nshamba wilayani Muleba. Tukio hilo lilitokea wakati akifanya kampeni za kura za maoni
kupitia CCM. Hali ya kuzomewa ilidumu kwa dakikakadhaa jambo lililofanya mgombea huyo kuomba msaada kwa askari waliokuwa kwe mkutano huo na kumuondosha.Kwa mara ya kwanza alizomewa juni 8, wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika kata hiyo hiyo. Akiwa na Kinana wananchi walimtuhumu
ufisadi wa fedha za Escrow na kushindwa kutekeleza ahadi ya kuwajengea barabara ya lami.
Source: Mwananchi
Nini maoni yako kuhusu hilo?
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)