Aliyekuwa Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna Tibaijuka anayewania jimbo hilo kwa mara ya pili, jana alishushwa jukwaani kwa kuzomewa na wanachama wake katika kata ya Nshamba wilayani Muleba. Tukio hilo lilitokea wakati akifanya kampeni za kura za maoni
kupitia CCM. Hali ya kuzomewa ilidumu kwa dakika
kadhaa jambo lililofanya mgombea huyo kuomba msaada kwa askari waliokuwa kwe mkutano huo na kumuondosha.
Kwa mara ya kwanza alizomewa juni 8, wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika kata hiyo hiyo. Akiwa na Kinana wananchi walimtuhumu
ufisadi wa fedha za Escrow na kushindwa kutekeleza ahadi ya kuwajengea barabara ya lami.
Source: Mwananchi
Nini maoni yako kuhusu hilo?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni