Jumamosi, 16 Julai 2016

HUYU NDIE JAMAA MWENYE PUA NDEFU ZAIDI DUNIANI



Pua ni moja ya organ muhimu. Je,ulishawai kufikiria jinsi gani utajisikia ukiwa na uwezo wa kuhisi kila harufu

Shindano la Pua kubwa zaidi Duniani
Watu wanashindana kwa vitu vingi. Na shindano la mwenye Pua ndefu ni bomba la shindano lenye mvuto wa aina yake duniani.Shindano hili lilipangwa Lafgenburk,nchini Ujerumani. Ni desturi ya mda mrefu sasa,michuano hii ilianza karibu miaka 50 iliyopita.Watu kutoka sehemu zote duniani huja katika mji huu kushindana.

Hili uweze kushiriki au kuwa mwanachama wa wenye Pua kubwa inakupasa uwe na pua isiyopungua urefu wa milimeta 60.Iwe imeshiba nene kiasi cha milimeta 40. Mpaka sasa chama chao kina watu zaidi ya 300.Kila baada ya miaka mitano wanafanya shindano la kumpata aliowazidi wote.

Mehment Ozyurek(Mturuki) ni mtu mwenye pua ndefu kuliko wote duniani hadi sasa,ana pua yenye urefu wa 8.8cm

Alhamisi, 14 Julai 2016

SUMAYE KUWANIA UENYEKITI CHADEMA



WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amekubali ombi la viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani, waliomchukulia fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho kanda hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Baadhi ya viongozi hao waliojitokeza kumchukulia fomu Sumaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, Mwenyekiti wa chama hicho Ilala, Dk. Makongoro Mahanga na Mwenyekiti wa mkoa wa Pwani, Baraka Mwago.

Baada ya kuchukua fomu hiyo katika ofisi za Chadema Kanda Kinondoni jana, viongozi hao walielekea nyumbani kwa Sumaye maeneo ya Tondoroni Kiluvya, mkoa wa Pwani, kwa ajili ya kumkabidhi.

Baada ya kupokea fomu hizo, Sumaye alikubali ombi hilo na kuzijaza na kuahidi kurejesha leo katika ofisi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake mara baada ya kukabidhiwa fomu hizo na Waitara, Sumaye alisema ni wakati sasa wa kukipeleka chama hicho hadi vitongojini.

Waziri Mkuu huyo mstaafu alihamia upinzania mwaka jana katika harakati za uchaguzi mkuu akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hivi karibuni aliteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

LULU ATENGENEZA FILAMU YA KIMATAIFA



Baada ya kimya cha muda mrefu, mshindi wa tuzo za Africa Magic, Elizabeth ‘Lulu’ Michael, anakuja na filamu yake mpya iitwayo ‘Ni Noma.’

Filamu hiyo inaingia sokoni Ijumaa hii kwa mfumo wa dijitali ambapo watu watainunua na kuingalia kwenye smartphone zao kupitia app ya Proin Box.

Lulu ameiambia Bongo5 kuwa filamu hiyo imekuja na mapinduzi makubwa kwa kila kitu kuanzia teknolojia na uigizaji. Amedai kuwa yeye na kampuni yake ya Proin, walitaka kuja na kitu tofauti na vilivyozoeleka kwenye filamu za Tanzania.

“Ilitubidi kwa kiasi fulani tutulie, tusome mazingira, tasnia yetu inamiss nini sasa hivi, mashabiki wetu wanahitaji nini sasa hivi,” anasema Lulu.
“Tumejitahidi kufanya production ya tofauti ambayo ina quality nzuri, it needs time, sio kama zamani kwa siku mnaweza mkashoot scene sita, saba, lakini saa zingine production kwa siku tulikuwa tunaweza kushoot scene mbili tu lakini mnahakikisha mnatoka na kitu kizuri,” ameongeza.

Amedai kuwa hata sauti zingine pia ilibidi waziingize upya studio ili kuwa na kitu bora kama ambavyo hufanyika kwenye filamu za Hollywood.

Lulu amesema watu wataweza kununua filamu hiyo kwenye app ya Proin Box kwa shilingi 2,500 tu kwa kupitia huduma za malipo ya simu kama M-Pesa, Airtel Money na zingine huku wale waliopo nje wakiweza kununua kwa credit cards.

Amesema baada ya kuizindua kwa mfumo wa dijitali, filamu hiyo itaanza kuoneshwa kwenye majumba ya sinema na kisha baadaye kuuzwa kwenye DVD. Hata hivyo ameeleza kuwa kwenye DVD hizo kutakuwa na vitu vya ziada kama vile behind the scenes, interview na vitu vingine.

Jumatano, 13 Julai 2016

MZIMU WAAJABU WAITESA MBEYA



WANANCHI wa Kijiji cha Mwela Kata ya Kandete wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya wako hatarini kukumbwa na baa la njaa baada ya kuibuka kile kinachodaiwa ‘mzimu wa ajabu’ ambao umekuwa ukianua unga unapokuwa umeanikwa juani na kupotea hewani katika mazingira ya kutatanisha.

Hali hiyo imejitokeza siku chache baada ya ‘mzimu’ huo kuzuka katika kijiji hicho ikielezwa kuwa unga na mazao mengine yaliyokuwa yameanikwa juani yalipotea hewani.

Kutokana na tukio hilo, imewalazimu wananchi wa Kijiji cha Mwela kutisha mkutano wa halmashauri ya kijiji kujadili na kutafuta suluhu ya hali hiyo.

Akizungumza na mwandishi kuhusu tukio hilo, mkazi mmoja wa kijiji hicho, Hamfrey Mwakitwange, alisema kuibuka kwa mzimu huo kumezua hofu kwa wakazi wa Mwela na maeneo ya jirani.

Alisema mwaka huu kuna hatari ya kutokea ukame na baa la njaa baada ya kuibuka mzimu huo wa ajabu.

“Kwa tukio la kuwapo mzimu huu wa ajabu tumejawa na hofu kubwa na kuna dalili ya kukumbwa na baa la njaa mwaka huu.

“Mzimu umekuwa ukichukua chakula hasa unga na mazao yanayoanikwa juani…tunabaki tunajiuliza, na sasa kimeitishwa kikao cha halmashauri ya kijiji ingawa mtazamo umegawanyika… sasa kuna wengine wanataka hata tuhushishe waganga,” alisema Mwakitwange.

Mjumbe wa Nyumba 10 wa CCM, Matrida Mwaisumbwa, alisema kitendo cha kuibuka mzimu huo ambao umekuwa ukichukua chakula, umeleta sintofahamu kijijini hapo.

Alisema hata wanapokuwa wanapika chakula kama ugali au ndizi, kimekuwa hakina radha na inadaiwa chakula hicho pia kinakuwa kimetembelewa na mzimu huo wa ajabu.

Alisema uongozi umeandaa mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba kukusanya michango kuwasaidia wananchi ambao wamekwisha kuathirika na mzimu huo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwale, Ferki Mwandenga, alisema licha ya kuwapo taarifa za mzimu huo wa ajabu anashindwa kuieleza kwa kina hali hiyo.

“Siwezi kulisema hili jambo maana linachanganya kidogo, sijui ni tukio la kichawi? Ingawa pamoja na hali hiyo, tambua kuwa Serikali haiamini uchawi,” alisema Mwandega.

MAJAMBAZI YAWATOROKA POLISI MBEYA WENGINE WAWILI WAUWAWA





watu wanne waliokuwa na pikipiki wanaodiwa kuwa majambazi waliokuwa wamepanga kupora fedha kutoka taasisi moja ya fedha na maduka ya biashara huko Tukuyu Rungwe Mbeya, hili ni tukio la pili la ujambazi kutokea ndani ya miezi miwili mkoani Mbeya
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya amesema watu wawili waliuwa na polisi katika mapambano hayo na polisi na wawili wametoroka, waliouawa walikutwa na silaha mbili bastola na gobore
Kamanda huyo amesema wote ambao hawajasajili silaha zao mpaka sasa watakuwa na makosa kwa kuwa ndio zinazotumika kufanya uhalifu

ANAYEDAIWA KUHAMISHA SHILINGI MILIONI SABA KWA DAKIKA AFIKISHWA MAHAKAMANI


Mfanyabiashara Mohamed Mustapha (anayeongea na simu) na wenzake, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana kukabiliana na tuhuma za kuibia Serikali kodi ya Sh milioni 7 kwa kila dakika kwa kipindi kirefu.
 **
Hatimaye mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa amekuwa akiibia Serikali takriban Sh7 milioni kwa dakika, amepandishwa kizimbani na wenzake wanne na kusomewa mashtaka 199, wote kwa pamoja.

Mfanyabiashara huyo, Mohamed Mustafa Yusufali na wenzake Alloyscious Gonzaga Mandago, Isaac Wilfred Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif Kabla, walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

 Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka za Serikali, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh15 bilioni.

Katika ya mashtaka hayo, Yusufali maarufu kwa majina ya Mohamedali, Choma au Jamalii anakabiliwa na mashtaka 198 yeye peke yake huku wenzake wakikabiliwa shtaka moja la utakatishaji fedha.

Kutokana na wingi wa mashtaka hayo, waendesha mashtaka wawili; Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai walilazimika kubadilishana ili kuwapa muda wa kupumua.

Kutokana na kukabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na shtaka la kutakatisha fedha, washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu na kulingana na mashtaka yanayowakabili, hayana dhamana.

Baada ya kumaliza kuwasomewa mashtaka hayo, upande wa mashtaka uliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Hivyo, Hakimu Mkazi, Huruma Shahidi anayesikiliza kesi hiyo aliamuru washtakiwa wapelekwe mahabusu hadi Julai 25, kesi hiyo itakapotajwa tena.

Kabla ya kupandishwa kizimbani, Yusufali alitajwa na Rais Magufuli kuwa ana mashine inayotoa risiti za kielektroniki (EFD) nje ya mfumo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuzisambaza kwa wafanyabiashara wengine, hivyo kujiingizia Sh7 milioni kwa dakika.

Rais Magufuli alieleza kuwa mtandao wake unawashirikisha watumishi wa TRA na Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brela), hivyo kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya shilingi.

 Katika mashtaka hayo, Yusufali anakabiliwa na mashtaka 181 ya kughushi, mashtaka 15 ya kuwasilisha nyaraka za uongo, udanganyifu katika kulipa kodi moja, shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh15,645,944,361, huku shtaka moja tu la utakatishaji fedha ndilo likimhusisha na wenzake.

Waendesha mashtaka hao walidai kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa akighushi nyaraka za kampuni mbalimbali, kuonyesha kuwa zimesajiliwa na zinaendesha  shughuli zake nchini kihalali wakati akijua siyo kweli.

Pia, walidai kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa akiwasilisha nyaraka za uongo TRA.

Kuhusu shtaka la kutakatisha fedha, upande wa mashtaka ulidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja kati ya Machi 2011 na Januari 2016, walitakatisha Sh1,895,88500 kwa kujifanya kuwa ni malipo ya  mikopo waliyoipokea kwa watu mbalimbali.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa kati ya Januari 2008 na Januari 2016, mfanyabiashara huyo alifanya udanganyifu katika kuwasilisha kwa Kamishna Mkuu wa TRA taarifa ya uongo ya marejesho ya mapato, hivyo kuikosesha Serikali mapato ya kodi ya VAT zaidi ya Sh15.6 bilioni.

Jumanne, 12 Julai 2016

LINAH : AAHIDI PENZI LAKIFICHO KWA MWENZI WAKE



Msanii Linah Sanga ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya 'Imani' amefunguka na kusema kuwa kwa mambo ambayo tayari yamemkuta kwenye mahusiano hayupo tayari tena kumuweka wazi mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii.

Linah Sanga akiongea kwenye kipindi cha Enews amesema kwamba kwa sasa yeye hayupo tayari kumuweka wazi mpenzi wake kama ilivyokuwa awali kwani jambo hilo kwanza linapelekea watu kuanza kufuatilia maisha yake ya mahusiano na si kazi zake za muziki.

Mbali na hilo Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa wapo watu kwenye mahusiano wanaingia ili kutaka kuonja penzi la mtu na kuona huyo mtu yupoje kwenye mapenzi ila hawana mipango endelevu wala hawaangalii mipango ya baadaye.
Msanii Linah Sanga ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya 'Imani' amefunguka na kusema kuwa kwa mambo ambayo tayari yamemkuta kwenye mahusiano hayupo tayari tena kumuweka wazi mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii.