Jumamosi, 9 Julai 2016

NGONO INAWAZEESHA WASICHANA :KHADIJA KOPA


Malkia wa mipasho Khadija Kopa amefunguka kwa kusema kuwa ngono ni moja kati ya vitu ambavyo vinawazeesha wasichana wengi.

Akiongea katika kipindi cha Ulimwengu wa Filamu kinachoruka TBC 1 Jumamosi hii, Khadija Kopa amesema yeye hazeeki kwa sababu siyo mtu wakuendekeza maswala ya ngono.

“Mimi najitunza sana ndo maana kila siku naonekana bado mbichi,” alisema Khadija. “Unajua wasichana wengi wanaendekeza masuala ya ngono, ngono inazeesha sana, haya makrimu ndo usiseme, ukiweza kukaa nayo mbali basi kila siku utaonekana mbichi,”

Katika hatua nyingine, muimbaji huyo amewataka mashabiki wake wa muziki kusubiria kazi mpya ambazo ataziachia hivi karibuni.

CLINTON NA TRUMP WAZUNGUMZIA MAUAJI MAREKANI



Clinton na Trump

Wagombea wawili wa kiti cha Urais nchini Marekani wametoa maoni yao kuhusu yale yaliyotokea katika mji wa Dallas ambapo polisi watano waliuawa na sita kujeruhiwa.

Hillary Clinton amesema kuwa mauaji hayo yanastahili kumshangaza kila raia wa Marekani.

Amesena kuwa Marekani ni lazima ifanye jitihada zaidi, kuwa na mipangilio kuhusu matumizi ya nguvu kupitia kiasi kutoka kwa maafisa wa polisi na pia kuwalinda polisi.


Maafisa wa polisi mjini Dallas

Naye Donald Trump alitoa video akisema kuwa mauaji hayo yamelitikisa taifa hilo.

Alisema kuwa Waamerika ni lazima waonyeshe uzalendo kwa polisi lakini akaongeza kwa vifo vya wanaume wawili weusi mikononi mwa polisi, vinaonyesha bayana jinsi kazi kubwa inastahili kufanywa kumwezesha kila Mmarekani kuhisi kulindwa.

AFUNGA NDOA NA MDOLI

Senji Nakajima mwenye umri wa miaka 61, amenunua doli na kulifanya kuwa mke wake wa maisha baada ya kuwa mbali na mkewe aliefunga nae ndoa na kuzaa nae watoto wawili.
Hakika, Senji Nakajima, kwa sasa anajivunia kuwa na mahusiano ya kimapenzi na doli lake analoliita Saori- baada ya kumpenda sana kutoka ndani ya moyo huyo mdoli.


Kwa sasa Senji anasema ana mahusiano na doli hilo kwa mda wa miaka sita, baada ya kuwa mbali na mkewe kwa kipindi chote hicho kutokana na kazi.
Miezi michache iliyopita  Mr Nakajima, kutoka Tokyo Japan, alidai kuwa mahusiano ya wawili hao yapo katika ngazi za juu sana.


Kwa upande wake Senji anadai kupata upendo wa uhakika, na anafurahia sana kuwa na mahusiano na Saori. Wawili hawa wanaishi katika nyumba ya pamoja - na pia wanachangia kitanda kimoja. Na anapenda kumchukua na kwenda nae shopping na kumnunulia nguo.


Mr Nakajima alisema:" Hawezi kumsaliti kamwe mrembo wake"
"Anadai amechoshwa na mahusiano ya binadamu. Wengi wao hawana moyo wa huruma.
"Kwa upande wake Senji Saori ni zaidi ya doli kwake.
Anamsaidia sana mpenzi wake na kufurahia maisha kwa pamoja.


Madoli haya kutoka kwa Wadachi, yanazidi kupata umaarufu Asia ambayo yananunuliwa kwa  £4,000.
Yana midomo mizuri, ngozi ya kuvutia kama ya binadamu wa kawaida- kazi kwako tu kuchagua umbo na rangi ya nywele.

HONGERA SHEKHE MKUU KWA KUONYESHA UPENDO



Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dsm amehudhuria ibada katika kanisa la Ufufuo.Akiongea na waumini wa kanisa hilo Sheikh amesema yeye kama mdau wa kamati ya Amani ya Mkoa wa Dsm anayofuraha kuona Tanzania inazidi kuwa nchi ya amani licha ya utofauti wa dini.

Amepongeza utii wa waumini wa Kikristo kwa viongozi wao,juhudi za kanisa katika kutoa huduma za jamii kama elimu na afya.Amewataka waumini wote kuishi kwa umoja na upendo na wenzao Wislam na baadae kusumisha amani na mshikamano wa Taifa.

VAT KUWAFUKUZA WATALII




Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye shughuli za utalii iliyoanza mwezi huu, imezishtua nchi 30 za Ulaya ambazo zimeiandikia barua Serikali ya Tanzania zikiomba ifikirie upya au isianze kutumika hadi mwaka ujao.

Kodi hiyo, ambayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali kukusanya mapato ili kuondokana na utegemezi, ilitangazwa kwenye Bunge la Bajeti lililopita na tayari Sheria ya Fedha imeshapitishwa kubariki matumizi yake, licha ya wabunge kuipinga kwa maelezo kuwa itazipa nchi washindani mwanya wa kukuza utalii.

Dk Philip Mpango alisema walipata wazo la kuanzisha kodi hiyo kutoka nchi jirani ya Kenya, lakini wakati akitangaza hayo waziri mwenzake wa nchi hiyo alitangaza kuiondoa baada ya utalii kuathirika kutokana na mashambulizi ya kigaidi.

Wakati sheria hiyo ikianza kutumika nchini, nchi hizo za Ulaya ambazo ni wadau wakuu katika sekta ya utalii zimemwandikia barua hiyo Dk Mpango, naibu wake, Dk Ashatu Kijaji na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe.

Chama cha Kitaifa wa Mawakala wa Usafiri na Wasimamizi wa Utalii (ECTAA) kutoka nchi 30 za Ulaya ndicho kinachoziwakilisha kampuni zaidi ya 70,000 za utalii barani humo. Nchi hizo ndizo zinazotoa asilimia 50 ya watalii wote duniani.

Katika barua yao iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa ECTAA, Michel de Blust, nchi hizo zilieleza wasiwasi wao kutokana na utambulishwaji wa ghafla wa kodi hiyo katika huduma za utalii, zikisema uamuzi huo unaongeza gharama za safari nchini.

“Najua utakubaliana na mimi kuwa kodi ina umuhimu wake na ina madhumuni yake, lakini inaweza kubadili mawazo ya watalii na wakachagua maeneo mengine,” inasema barua ya Blust.

Waziri wa Fedha na Mipango, “Mfano mzuri ni Kenya, utambulishaji wa kodi katika huduma za utalii mwaka jana ulishusha idadi ya watalii kwa asilimia nne na baadaye Kenya waliamua kuachana na kodi hiyo ili kudumisha ushindani wake.”

Barua hiyo inasema kodi hiyo katika huduma za utalii itaathiri waandaaji wa safari za watalii wanaotoa huduma nchini kwa sababu hakukuwa na tangazo la kuwaandaa kabla ya kuanzishwa kwa tozo hiyo.

“Waandaaji wa safari wa Ulaya wanawajibika na sheria inayomlinda mteja, hivyo wanatakiwa wawe wanafahamu bei na kodi mpya kabla. Kwa sasa ni vigumu mno kwa waandaji kubadili bei zao ghafla,” inasema barua hiyo.

Kadhalika, barua hiyo inaeleza kuwa Wakala wa Utalii wa Tanzania uliwasiliana na Wakala wa Ulaya kuhusu kodi hiyo na mawakala wa Ulaya wanatafakari kama wanaweza kuingia gharama hiyo au kujiondoa katika mpango huo.

“Kama kodi hii ikiahirishwa, basi waandaaji wa safari za watalii watajipanga kuingia gharama hizi na kubadili mfumo wote wa huduma hizo Ulaya,” inasema barua hiyo.

Hivi karibuni, Waziri Maghembe alinukuliwa kwenye mkutano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), akisema kuwa Serikali haitabadili msimamo huo.

Alisema Sh7 bilioni wanazotarajia kupata kwa kutoza VAT kwenye huduma za utalii, zitawapa uwezo wa kutangaza utalii nje ya nchi na kuziba pengo la bajeti linalotokana na kushuka kwa utalii wa uwindaji. Alisema VAT itakayokatwa ni asilimia 18 ya kitu kilichonunuliwa na inatozwa wakati wa kununua huduma ya utalii.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi alisema hajaiona barua ya ECTAA, lakini akasema watafanya kikao na Chama cha Wafanyabiashara za Utalii Tanzania (Tato) ili kujadili nini kifanyike ili sekta ya utalii isiyumbe.

“Hili ni suala mtambuka na hii VAT ilipitishwa na kikao cha bajeti, wizara kwa sasa haina la kufanya zaidi ya kutafuta njia mbadala ili sekta isiyumbe,” alisema.

Tovuti kwa ajili ya watalii ya Afrika, Safaribookings.com imeeleza kuwa wamekuwa wakipata barua pepe kutoka kwa wateja ambao wamepewa taarifa kutoka kwa wasimamizi wa watalii kulipa fedha za ziada.

Marc Harris, mkurugenzi wa kampuni ya Tanzania Odyssey inayotoa huduma za kitalii na yenye makazi yake nchini, aliliambia gazeti la Daily Telegraph la Uingereza kuwa kodi mpya ni janga kubwa ambalo halikutarajiwa na wengi.

“Watanzania wanaweza kufanya chochote kuhusu kodi, lakini suala la muda ndiyo tatizo. Wametupa taarifa hizi Juni 23, wiki moja tu kabla ya kodi kuanza kutozwa,” alikaririwa na gazeti hilo.

Alisema gharama kubwa itaonekana kwenye malazi ambayo inaonekana kuongezeka kwa asilimia saba.

“Kinachoshangaza ni kuwa Hifadhi za Taifa hazijasajiliwa VAT, lakini inatoza fedha hizo. Sijui watazitumiaje,” alisema Harris.

Mmiliki wa kampuni ya kitalii ya Safaribooking.com, Wouter Vergeer alisema muda mfupi waliopewa umewashtua.

“Maelfu ya wateja wameshtushwa na chaji hizo ambazo hazikutarajiwa. Wengi hawajapata muda wa kujipanga kwa tozo hizo, hata risiti zenyewe za VAT hatuna,”alisema.

JE UNA TATIZO LA KUWASHWA LIPS?HII HAPA TIBA YAKE




Hili ni tatizo ambalo mtu uhisi kuwashwa na kuwa na hamu ya kujikuna ngozi au kuvimba sehemu za mdomo(Lips). Hii husababishwa na vipodozi, lipsticks, vyakula, mazingira na magonjwa mbalimbali asa malengelenge, magonjwa ya ngozi, chango, saratani, kuchafuka kwa damu, ukurutu, matatizo katika nyongo, ukosefu wa vitamini nk.

MATIBABU YAKE.
Unaweza kujitibu tatizo hili kwa kuepuka aina ya vyakula, vipodozi na lipsticks ambavyo hujawahi kutumia. Pia unaweza kutumia dawa zinazoongeza vitamins kama Multivitamin complex au kula vyakula vyenye vinavyoongeza vitamin mwilini sambamba na kulainisha lips.

Kumbuka kujikuna au kugusa sehemu inayowashwa itakupelekea kukuza tatzo na kuongeza maambukizi mengine.
Kama tatizo haliponi unaweza kufika hospitali au kituo chochote cha afya kwa uchunguzi ambapo dawa kama cetrizene, hydrocortisone, acyclovir, antibiotics kwa njia ya sindano, vidonge au cream huweza kutolewa kutokana na ukubwa wa tatizo.

Alhamisi, 23 Juni 2016

HII NDIO HESABU ITAKAYOKUFIKISHA KWENYE KILELE CHA MAFANIKIO



Ikiwa umeajiliwa au umejiajiri mwenyewe hesabu hii inakuhusu kwa namna moja au nyingine,unatakiwa kujua kiasi ambacho unaingiza kila sekunde,dakika,saa,siku,wiki,mwezi na mwaka.

Hesabu hii imekuwa ngumu sana kwa watu wengi kwani wamekuwa wakipata pesa ya mshahara/faida na  kushindwa kujua ni kiasi gani unachoingiza kila baada ya sekunde,dakika,lisaa,siku,wiki na mwezi.

Unatakiwa kujua ya kuwa muda wako una thamani kubwa,kila sekunde unayoitumia kufanya kazi uliyonayo inakulipa shilingi ngapi.

Mfano wewe ni mfanyakazi ambae unalipwa kiasi cha TSH. 700,000/= kwa mwezi kiasi hiki cha pesa kigawe kwa mlolongo wa sekunde,dakika,lisaa,siku,wiki na mwezi.
Yaani 700,000÷30=23,333.3 kwa siku ambapo ni sawa na 23,333÷12 ya kazi =1,944 kwa saa na unaingiza shilingi 2.7 kwa kila sekunde

Ukiijua hesabu hiyo vizuri unaweza kutathimini mwenyewe ni kiasi gani unalipwa.Je inakutosheleza katika mahitaji yako?Je ni kiasi ganiunataka kuingiza kwa kila sekunde dakika,lisaa,siku,wiki na mwezi?
****KUMBUKA MAFANIKIO YAKO MIKONONI MWAKO AMUA SASA****