Jumamosi, 4 Juni 2016

ZITTO NA MDEE WAUNGURUMA

Wakihojiwa na redio moja mkoani Kagera inakosemekana wataanzia ziara hivi karibuni
Zitto amesema hawezi kumjadili naibu spika maana anajua anatumwa. "Huyu simjadili maana najua anatumwa na akiambiwa geuka anageuka, akiambiwa kimbia anakimbia". Alisema yeye anamwambia aliyemtuma apambane na ufisadi na si demokrasia kwani dunia nzima waliogombana na demokrasia wameangukia pua. Amesisitiza ziara inayotarajia kuanza itawazindua watanzania

Mdee: Amesema kiini cha kuzuia matangazo ya moja kwa moja ni kutaka kuwaaminisha kwamba serikali hii ni tukufu kumbe ya kisanii tu. Amewataka watanzania wajitokeze kwa maelfu kwenye mikutano yao ili wadadavuliwe serikali ilivyo ya kidikiteta. "Ndani ya bunge tumeaacha wabunge makini wa kuweza kuibana serikali, nje tuko mashine za kutosha kuiamsha jamii ya watanzania".

Wote wamesema serikali ya Magufuli ina dalili zote za kidikteta na inaliteka bunge makusudi ili kunyamazisha wakosoaji maana huko ndiko Magufuli anaweza kuanikwa. Wamesema madikteta wote hupenda kusifiwa na kuimbiwa nyimbo za kuabudiwa. Walisema

Alhamisi, 2 Juni 2016

HUYU NDIE MWANAMKE WA KUOA

Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.

Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachowezakuwafanya wakapata wachumba niuzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.

Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.

Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.

1. MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.

Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingiutamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.

Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.

Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.

Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.

2. WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja sualana kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya.
Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.

Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.

3. WENYE UCHU NA MAENDELEO
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini.

Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.

4. WASIOPENDA MAKUU
Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?"

Akimuona rafiki yake kanunua simuya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia,"mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.

Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’

Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.

Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leoamemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.

Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitajiupo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulaniwakati inawezekana uwezekano haupo.

5. WAVUMILIVU
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.

Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotokea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?

Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.

Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo kimsingi havikubaliki katka jamii.

Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali

Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.

FISI WAFUKUA MAKABURI SHINYANGA

Shinyanga. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Mika Nyange amesema vimeokotwa vipande vya miili ya binadamu Mtaa wa Butengwa, baada ya makaburi ya Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga kufukuliwa na fisi.

“Baada ya taarifa kupatikana askari walifika eneo la tukio na kujionea makaburi yakiwa yamefukuliwa, hivyo tukawataka wananchi kushirikiana kufukia miili hiyo,” amesema Nyange.

Mjumbe wa Mtaa wa Butengwa, Peter Joseph amesema alipewa taarifa ya kuonekana kwa miili hiyo ikiwa inatafunwa na mbwa.

Mjumbe wa Mtaa wa Mageuzi, Kata ya Ngokolo, Mhoja Pius amelalamikia Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kutosimamia vizuri mazishi ya watu wasiokuwa na ndugu.

UINGEREZA YATANGAZA KUZINDUA NOTI YA PLASTIKI

Benki kuu ya Uingereza imetangaza kuzinduliwa kwa noti za Plastiki za pauni 5.

Noti hiyo ya pauni tano itakuwa ya kwanza katika kipindi cha miaka 100 ambapo sarafu ya nchi hiyo imekuwa ikichapishwa kwenye karatasi.

Plastiki hiyo inayofahamika kwa jina halisi 'polymer' ni nyepesi na itahitaji wino maalum kutumiwa kuchapishwa pande zote mbili.

Hata hivyo Uingereza sio taifa la kwanza kutumia noti za plastiki, mataifa mengine zaidi ya 20 duniani tayari yanatumia noti zilizotengezwa kutokana na plastiki.

Mataifa hayo ni pamoja na Scotland, Australia, New Zealand, na Canada

Benki kuu ya Uingereza inasema kuwa noti za plastiki (Polymer) ni bora kuliko zinazotumika sasa za karatasi kwa sababu zinadumu zaidi na pia hazichafuki.


Aidha noti hizo hazilowi maji haswa pale mtu anaposahau pesa mfukoni kisha nguo zake zikaoshwa.
Benki hiyo pia inasema kuwa ni vigumu mno mtu kutengeneza noti bandia za plastiki.

Pia benki hiyo inasema kuwa noti za plastiki zitapunguza gharama ya kuchapisha noti mpya kila mwaka.

Noti hiyo itaanza kutumika mwezi septemba mwaka huu.

Baada ya majaribio ya noti ya pauni tano, benki hiyo inapania kuzindua noti za pauni 10 mwakani na kisha pauni 20 kufikia mwaka wa 2020.

WALIONDAMANA CHUO KIKUU WAKALIA KUTI KAVU

Dar es Salaam. Wanafunzi walioandamana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakishinikiza malipo yao ya fedha za kujikimu juzi, huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu.

Wanafunzi hao huenda wakaadhibiwa kwa kosa la kukiuka sheria ndogo ya chuo kwa kuandaa mkusanyiko bila kibali cha menejimenti.

Hayo yalisemwa jana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Florens Luoga.

Alisema mamlaka za nidhamu chuoni hapo zinaendelea na uchunguzi kubaini nani aliyehusika katika tukio hilo.

SINA AMANI NIMEKUWA KAMA NIMEUWA - WEMA SEPETU

Msanii wa filamu na mjasiriamali Wema Sepetu amefunguka ya moyoni kutokana na namna mashabiki wake wa Instgram wanavyomchukulia na kumpa maneno ambayo muda mwingine yanamuumiza na kumkosesha amani na kumfanya ajione ni kama mkosaji mkubwa.

Wema Sepetu ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ha hayo yamekuja baada ya watu kuanza kusema maneno mbalimbali kwa kile alichofanya Wema Sepetu kupost picha ambayo ni promo ya kazi mpya ya msanii kutoka WCB.

Baada ya kupost picha hiyo baadhi ya watu walianza kusema kuwa bidada huyo anatafuta kiki, wengine wakisema kuwa Wema Sepetu kwa Diamond Platnum apindui.

"Kitu ambacho nakiona kutoka Instagram, Watu wanapenda sana fujo fujo, Purukushani, mara huyu na huyu hawaongei, flani kamchukulia flani bwana, yule kafumaniwa. Hicho ndiyo mnachokiona kina kick.

 Ila mwisho wa siku ukija kuangalia , ni kweli maana dunia ya leo umbea unauza. Ila jamani ifike muda tukue mimi binafsi kuna vitu vinanichosha actually vimenichosha ifike muda kila mtu aangalie maisha yake na afanye kile kinachomridhisha nafsi yake. kwangu naangalia wat God has to say bout wat im doin... Imekuwa too much tokea nilivyopost uzalendo ikaonekana all sorts of Crazy, But u know wat, I dont care" aliandika Wema Sepetu

"Sasa basi, nitapost ninachotaka nyinyi endeleeni kujudge na kuleta conclusion zenu mnazojua... Iwe nataka attention, iwe natafuta kick, iwe nitokeje, iwe najipendekeza, iwe vyovyote It all comes down to me.

Kuna msemo unasemaga tenda Wema uende zako... Dats how I roll. Na nimekuwa nikifanya hivyo siku zote. Sitegemei na wala sitaki mtu ninae msupport au kumuunga mkono na yeye afanye the same na wala sina haja na kupostiwa.

Niwe sipindui au napindua It doesnt make A difference. Kwanza haya mambo ya kupinduana yameanzaga lini Mungu wangu. Ila instagram mna majungu sana. Mimi siwezi jamani mniachage basi sometimes, sina amani imekuwa kama nimeua" aliongeza Wema Sepetu

Jumatano, 1 Juni 2016

MWANAMKE ALIYEKATAA KUOLEWA ACHOMWA MOTO HADI KUFA

Mwanamke mmoja wa Pakistan aliyechomwa kwa kukataa wito wa ndoa amefariki kutokana na majeraha yake.

Maria Sadaqat ,mwalimu wa shule aliye na umri mdogo alishambulia nyumbani kwake na kundi moja la wanaume siku ya jumapili na kufariki katika hospitali mjini Islamabad siku ya Jumatano.

Familia yake imesema kuwa alikataa kuolewa na mtoto wa mmiliki wa shule ambayo amekuwa akifunza.

Wanakampeni wanasema kuwa visa vya mashambulio dhidi ya wanawake wanaokataa kuolewa ni vingi nchini Pakistan.

Waziri mkuu wa Punjab Shahbaz Sharif alianzisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo.

Babake Maria amesema kuwa mmiliki wa shule hiyo ni mojawapo ya watu waliomshambulia mwanaye.

Polisi wameambia BBC kwamba wanaume hao walimpiga kabla ya kumwagia mafuta ya petroli na kumchoma karibu na eneo la kitalii la Muree,karibu na mji mkuu.