Jumanne, 12 Aprili 2016

KUKATA TAMAA NI DHAMBI

Katika shughulli zetu za kila siku tumekuwa tukikumbwa na majaribu mbalimbali,majaribu haya yanaweza kuwa ya nadhalia ama vitendo,watu wengi wanashindwa kugundua siri ya kushinda majaribu ambayo ni uvumilivu. Uvumilivu ni hali ya kustahimili machungu(Maana hii kutokana na kamusi ya Kiswahili sanifu) Lakini tunaweza kusema uvumilivu ni hali ya kuhimili matatizo mbalimbali yanayotukumba katika maisha yetu ya kila siku. Tumekuwa tukikumbwa na kila aina ya matatizo,majaribu na uonevu ambao unapelekea kukata tamaa ama kuamua kufanya jambo ambalo litamuacha mdomo wazi yule aliyekuwa akikuamini,kukuwazia mazuri na aliyekuwa akitegemea msaada wa mawazo ama kifedha. Majaribu haya yamekuwa yakipelekea baadhi yetu kufanya maamuzi magumu ya kujinyonga,kumeza dawa,kutumia madawa ya kulevya ama kupigana,wengine tumekua tukijiapiza kuwa hatutaweza tena kurudia kazi,biashara ama mahusiano ambayo yameleta mpasuko katika moyo wako. Nimekuwa nikisikia kauli nyingi zenye sauti ya kukata tamaa na zilizokuwa na miungurumo ya kukosa uvumilivu huku zikinakshiwa na maamuzi ya kutisha,utasikia ‘Sitafanyi tena kazi hii’ ‘Sitaki kuolewa tena’ ‘Sitarudi tena’Sauti hizi za kukata tamaa na kukosa uvumilivu zilizo na ngurumo ya kukosa neno la Mungu zimekuwa zikitamkwa na watu mbalimbali ambao wamejeruhiwa mioyo yao. Tumesahau kuwa yupo aliyetuumba na anatuangalia katika kauli zetu za kukata tamaa huku tukisahau kumwita Mungu katika shida zetu.Tumekuwa tukilaumu kwa sauti zilizokosa uvumilivu na zilizokata tamaa. Hata tukirejea katika vitabu vya Mungu,mtume Paulo aliweza kuvumilia katika hali ya dhiki,njaa,kupungukiwa na kushiba pia,si huyu tu bali Mungu aliweza kumfanya Ayubu kuwa maskini wa kutupwa wakati alikuwa ni tajiri lakini kwa yote hayo Ayubu alivumilia. Hata wewe pia uliyekata tamaa ya kufanya biashara,kusoma,kufanya kazi kutafuta mchumba eti kwa sababu umeshindwa kufanikiwa katika malengo yako kwa kusikia sauti za “Nimeshindwa mimi sijui kama utaweza”ama utasikia “Kazi hiyo ni ngumu inawafaa akina Fulani”Chukua hatua sasa achana na dhana ya umaskini wa mawazo na ukosefu wa uvumilivu kwa kile unachokifanya,songa mbele huku ikiimba wimbo wa ushindi kwa kila jambo. Uvumilivu ndio unapelekea mtu kufanikiwa kwa kila anachokifanya na kuwa na maisha mazuri katika siku zake za kuishi hapa duniani.Asanteni kwa muda wenu Tuonane katika makal ijayo

HIZI NDIZO NUKUU ZA HOTUBA KALI ZA SOKOINE

"Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu" - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983 "Juu ya suala hili la mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa kupunguza uongezaji wa wataalam wasiohitajika katika Serikali na katika mashirika ya umma mpaka hapo hali yetu ya uchumi itakapokuwa katika hali nzuri" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1982 "Serikali inasimamia bei, lakini Serikali yetu itakwenda mpaka itasimamia bei ya mhogo, dagaa na bei ya kila kitu? Haiwezekani, vitu vingine ni lazima vizalishwe kwa wingi ili bei yenyewe iweze kujirekebisha" - Edward Moringe Sokoine, 24 Septemba 1983 "Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa" - Edward Moringe Sokoine, 4 Oktoba 1983 "Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, 'mali hii umeipata wapi?'" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1983 "Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi" - Edward Moringe Sokoine, 1Februari 1977

HUYU NDIE EDWARD MORINGE SOKOINE

Edward Moringe sokoine alizaliwa 1Augost 1938 katika miji ya Monduli Arusha Tanzania.Alisoma elimu ya msingi Monduli na shule ya sekondari Umbwe katika miaka ya 1948 - 1958.Mwaka 1961 alijiunga na chama cha siasa cha TANU,Alifanikiwa kwenda kuchukua masomo ya uongozi nchini Ujerumani ilikuwa 1962 -1963 baadae alikaa kama afisa mtendaji wa wilaya ya Masai na kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo hilo.1967 alichaguliwa na Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa naibu waziri wa mawasiliano usafiri na kazi 1972 alihamishwa na kuwa waziri wa usalama.1977 alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM mnamo 1977 alichaguliwa kuwa waziri mkuu kisha mwaka 1982 alipumzika katika nafasi hiyo na mwaka 1983 alirudi ofsini kwake akiwa na nembo ya Uwaziri mkuu Mpaka alipofariki 12April 1983,"NDUGU wananchi, leo saa saba mchana; ndugu yetu na kijana wetu. Ndugu Edward Moringe Sokoine; alipokuwa safarini kutoka Dodoma kuja Dar es Salaam, gari yake ilipata ajali. Amefariki dunia.’ mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina"Ilikuwa ni hotuba fupi ya mwalimu JK iliyoacha vilio na simanzi kwa watnzania.

Jumatatu, 11 Aprili 2016

ANNA KILANGO:SINA TAARIFA YA KUACHISHWA KAZI.

Leo taarifa ambayo metrend vya kutosha kwa muda mfupi, ni kuhusu Rais wa J.M wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mama Anne Kilango Malecela katika nafasi hiyo. Mwanasiasa huyu Mkongwe amekumbwa na Panga hili baada ya kutoa taarifa hadharani kuwa, Mkoa wa Shinyanga haukuwa na watumishi hewa. Kauli ambayo ilikinzana na tume rasmi ya uchunguzi iliyotumwa mkoani humo, ambapo iligundua watumishi hewa 45 na bado uchunguzi Zaidi unaendelea. Akiongea na kituo cha radio cha Times Fm,Kilango amedai kuwa hana taarifa juu ya utenguzi wa nafasi hiyo kutoka kwa aliyemteua. “Jamani Mimi sina taarifa sipendi kukizungumzia maana yake sijaambiwa na aliyeniteua, sina la kukwambia.” Alisema na kukata simu. Anne Kilango Malecele amedumu kwenye nafasi hiyo kwa majuma kadhaa, hata mwezi mmoja hajafikisha.
,

MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA ANNA KILANGO MALECELA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anna kilango Malecela kuanzia leo.
Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango Malecela kutungaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea. Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.

PATA MAGAZETI YA LEO 11/04/2016


















PATA MAGAZETI YA LEO 11/04/2016